Pastor Carlos Kirimbai Manna Tabernacle Bible Church |
Naona
siku hizi kumezuka sana kutamkiwa baraka na mema ambayo inaambatana na
kutakiwa kusema amen na kulike na mengineyo kama hayo. Mimi am just
curious. Kutamkiwa baraka ni sawa na kutamkiwa kinabii or which ever
other way ni sawa pia. Ila sasa:
2 PET. 1:20-21 SUV
Mkijua neno hili kwanza, ya kwamba hakuna unabii katika maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani tu. Maana unabii haukuletwa po pote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu.
Huwezi kutabiri au kutamka utakavyo wewe bali unasema yale ambayo Mungu anakupa kusema.
Kutamka au kudecree ninavyoelewa mimi huja baada ya neno kuvuviwa alafu ukisha kutafsiri anavyokuongoza Roho unalitamka kwa mamlaka ya kudecree juu ya msikilizaji. Kwangu na uelewa wangu mdogo, nabii wa agano jipya ni mtu anayefundisha na kuhubiri kwa uvuvio huku akiziweka wazi siri na mafumbo ya Mungu katika maandiko. Neno la Mungu ndo msingi wa kila decree.
2 PET. 1:19 SUV
Nasi tuna lile neno la unabii lililo imara zaidi, ambalo, mkiliangalia, kama taa ing’aayo mahali penye giza, mwafanya vyema, mpaka kutakapopambazuka, na nyota ya asubuhi kuzuka mioyoni mwenu.
Ili niweze kutoa matamko kiusahihi inabidi kwanza nidake alichosema ndipo niweze nami kusema.
AMO. 3:8 SUV
Simba amekwisha kunguruma, ni nani asiyeogopa? Bwana MUNGU amenena, ni nani awezaye neno ila kutabiri?
EBR. 13:5-6 SUV
Msiwe na tabia ya kupenda fedha; mwe radhi na vitu mlivyo navyo; kwa kuwa yeye mwenyewe amesema, Sitakupungukia kabisa, wala sitakuacha kabisa. Hata twathubutu kusema, Bwana ndiye anisaidiaye, sitaogopa; Mwanadamu atanitenda nini?

No comments:
Post a Comment