Dr Alex Malasusa Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania |
Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dr Alex Malasusa amewahamasisha wakristo kote Nchinikujihusisha na ujenzi wa Makanisa na Kuhudhulia Ibada na na kupunguza uharifu katika jamii.
Mkuu wa Kanisa hilo wakati wa harambee ya ujenzi wa Kanisa la Usharika wa Sumbawanga mjini na mkoani Rukwa,ambapo alifafanua kuwa endapo kuwa jamii itajihusisha na ibada ipasavyo Serikali haitakuwa na haja ya kuwa na magereza mengi.
Kwa Upande wake mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya alisema kuwa kujenga kanisa ni kuwekeza katika kufanya kwa hiari ili jamii iweze kuwa salama na kuweza kupata kumwabudu Mungu zaidi.
Chimbuko la Kujenga Kanisa lililotokana na ongezeko la idadi ya wauminui na uchakavu wa Kanisa la zamani lililojengwa mwaka 1982 hivyo kutokidhi mahiutaji ya waumini hufikia 400 tofauti na awali.
No comments:
Post a Comment