HOTUBA YA MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS WA
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, WAKATI UFUNGUZI WA
KONGAMANO LA VIONGOZI WA DINI KUHUSU MATUMIZI YA
RASILIMALI ZETU ZA GESI ASILIA, MAFUTA NA MADINI KWA
AMANI NA MAENDELEO YA TANZANIA, WHITESANDS HOTEL,
TAREHE 20-22 JANUARI 2014
Waheshimiwa Viongozi wa Dini;
Waheshimiwa Mawaziri;
Waheshimiwa Wakuu wa Mikoa;
Ndugu Makatibu Wakuu;
Wageni Waalikwa;
Mabibi na Mabwana;
Naomba nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema,
kwa kutujaalia uzima na kutuwezesha kukutana hapa siku ya leo kujadili
matumizi
ya rasilimali zetu za gesi asilia, mafuta na madini kwa amani na
maendeleo ya nchi
yetu. Kwa namna
ya pekee nawashukuru viongozi
wa dini kwa
kunishirikisha
kwenye Kongamano hili
muhimu na la
aina yake. Mmenipa
heshima kubwa
ambayo sikuitegemea. Asanteni
sana.
Nawapongeza sana kwa uamuzi wenu wa busara wa kuandaa Kongamano
hili. Mmedhihirisha kwa
vitendo uhodari wenu wa kutekeleza
jukumu lenu la
msingi la kulea taifa letu kiroho na kushiriki kikamilifu katika
masuala mengine
muhimu yahusuyo maendeleo na ustawi
wa Tanzania na watu wake. Ninyi
ni
wazalendo wa kweli. Ni matumaini
yangu na ya Serikali ninayoingoza kuwa ubia
wa aina hii utaimarishwa na kudumishwa kwa faida ya nchi yetu.
Najua mlianza kwa kukereketwa na athari za matumizi
makubwa ya miti
kwa matumizi ya nishati jambo ambalo linachangia sana kuharibika kwa mazingira
duniani. Mmeishia kwenye
Kongamano hili. Lina uwiano kabisa kwani
tunakata
miti kwa ajili ya kuni na mkaa.
Tukitumia gesi itatoa huko. Ni
dhamira yetu hiyo.
Ndugu Viongozi wa Dini;
Kongamano hili linafanyika
katika kipindi mwafaka
kabisa, kipindi
ambacho ugunduzi mkubwa wa gesi tayari umefanyika na dalili za
kugunduliwa
zaidi zipo. Kipindi ambacho
hazina ya madini mbalimbali inazidi kugunduliwa na
makampuni ya utafiti yanatupa moyo kuwa mambo huenda yakawa mazuri
zaidi.
Pia, ni kipindi
ambacho rasilimali zetu za
wanyamapori na misitu
zinatishiwa
kutoweka. Ni kipindi ambacho
wakulima na wafugaji na wafugaji na wahifadhi
wa misitu na wanyamapori wanashindania ardhi ya kufanyia shughuli
zao.
Sasa
hivi ni kipindi mwafaka kabisa kukaa chini na kutafakari jinsi gani
rasilimali hizi
zinaweza kulindwa na kutumika kwa manufaa ya nchi yetu na watu wake
wote
zikiwanufaisha kule ambako rasilimali hizo zipo na hata kule ambako
hazipo.
Ni ukweli usiopingika kuwa Mwenyezi Mungu ameijalia nchi yenye utajiri
mkubwa wa rasilimali za asili.
Ametujaalia ardhi kubwa yenye rutuba, madini ya
aina mbalimbali, misitu na
mbuga za wanyama wa kila aina, hali ya hewa nzuri,
bahari, maziwa makubwa, mito mingi, watu wengi na kadhalika. Rasilimali hizi,
kwa tabia yake,
inatakiwa zitumiwe vizuri
ili kuboresha hali
na maisha ya
Watanzania wote sawia na kwa miaka mingi na hata milele. Vinginevyo rasilimali
hizi zinaweza kugeuka
kuwa chanzo cha
mifarakano, magomvi na
mauaji.
Zinaweza kuwa balaa na kuleta maangamizi nchini
badala ya kuwa baraka na
neema.
Mifano ipo ya nchi mbalimbali
duniani zilizojikuta zina migogoro na vita
vya wenyewe kwa wenyewe kutokana na kugombania utajiri wao wa
rasilimali za
asili. Watu wa nchi hizo
wanajuta kuwa na rasilimali ambazo zimekuwa chanzo
cha kuhatarisha amani, utulivu,
usalama na hata uhai wao. Kwa hapa
Tanzania
tunashukuru Mungu rasilimali hazijageuka kuwa balaa na tunaomba hilo
lisitokee.
Tangu Tanganyika ipate
uhuru na Zanzibar
kufanya Mapinduzi Matukufu
na
hatimaye nchi zetu mbili kuungana
na kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Serikali za awamu
zote zimesimamia kwa
makini rasilimali za
nchi yetu ili
ziwanufaishe Watanzania wote.
Tumetunga sheria na sera mbalimbali kuhakikisha
kuwa lengo letu hilo linatimia.
Hata hivyo, usimamizi
wa sheria hizo na
utekelezaji wa sera
zetu nzuri
umekuwa unakabiliwa na
changamoto mbalimbali kwa
nyakati mbalimbali.
Mpaka hapa tulipofika ni umahiri wa viongozi wetu ndiyo uliotuwezesha
kuzuia
mambo yasiharibike na kugeuka kuwa matatizo makubwa. Tumefanikiwa kiasi
chake ingawaje hatujaweza kuzuia kabisa matatizo yasitokee hapa na
pale. Taarifa
za kugombea rasilimali zimekuwa
zinasikika na nyingine zikiwa zimesababisha
watu kupoteza maisha, kujeruhiwa na mali kuharibiwa. Tutafanya nini kukomesha
hali hiyo isijitokeze, ni jambo ambalo sisi kama taifa, yaani
Serikali, wananchi na
wadau mbalimbali, wakiwemo
viongozi wa dini hatuna, budi kulizungumza
na
kulipatia ufumbuzi.
Ndugu Viongozi wa Dini;
Nimefarijika sana na uamuzi wenu wa kufanya mkutano huu kuzungumzia
rasilimali ya mafuta na
gesi. Juhudi za kutafuta mafuta na
gesi imeanza tangu
ukoloni, zikaendelea katika awamu zote baada ya Uhuru. Shirika la
Maendeleo ya
Petroli (TPDC) lilianzishwa
mwaka 1969 kuongoza juhudi hizo na kusimamia
sekta ya mafuta nchini kwa manufaa ya Watanzania wote. Hatujajaaliwa kupata
mafuta mpaka sasa lakini tumefanikiwa kupata gesi. Ugunduzi wa kwanza wa gesi
asilia ulifanyika Songosongo mwaka 1971 na baadae Msimbati, Mtwara mwaka
1982. Utafutaji na ugunduzi huo
uligharimiwa na Serikali yetu na hivyo gesi hiyo
ni mali ya Serikali. Baada ya
ugunduzi huo makampuni binafsi yalipata shauku ya
kutafuta mafuta na gesi nchini.
Mwaka 1980 ikatungwa Sheria ya Utafutaji wa Uzalishaji wa Mafuta kwa
nia ya kuweka masharti na utaratibu wa makampuni kushiriki katika
utafutaji na
uzalishaji wa mafuta na
gesi nchini. Pia unatoa mwongozo wa mgawanyo wa
mapato baina ya
makampuni na Serikali.
Sheria hiyo imeendelea
kufanyiwa
maboresho kwa nyakati
mbalimbali kulingana na
mahitaji ya wakati
husika.
Kuanzia mwaka 2007 shughuli za utafutaji wa mafuta na gesi asilia
ziliongezeka
kwa nguvu na
kasi kubwa. Juhudi
hizo zilizaa matunda
mwaka 2010 kwa
uvumbuzi wa kwanza
wa gesi katika
Bahari Kuu uliofanywa na
Kampuni za
Orphir na British Gas. Baada ya
hapo ugunduzi umeendelea hadi kufikia futi za
ujazo trilioni 46.5 za rasilimali ya gesi nchini mpaka sasa. Utafiti unaendelea na
matumaini ya kupata gesi zaidi
yapo. Kufuatia ugunduzi huo, Tanzania
sasa ni
moja ya nchi zimazohesabiwa kuwa na gesi nyingi duniani na ni nchi
inayovutia
wawekezaji wengi katika sekta
ya gesi. Kwa sababu hiyo, tukaamua
kuifanyia
mapitio Sheria ya
Utafutaji na Uzalishaji
wa Mafuta na
Gesi. Mwaka 2013
tumetunga Sera ya
Gesi na kurekebisha
masharti ya Mkataba
wa Kugawana
Mapato yatokanayo na gesi
(Production Sharing Agreement) na
kuongeza mgao
wa Serikali.
Ndugu Viongozi wa Dini;
Sera ya Gesi
Asilia iliyopitishwa mwezi
Oktoba, mwaka jana
(2013)
imeeleza wazi, tena
kwa lugha nyepesi,
kuwa gesi ya
Tanzania ni mali
ya
Watanzania wote na itatumika kwa manufaa ya Watanzania wote – wa
kizazi hiki
na kijacho. Katika
matumizi ya gesi, kipaumbele kitakuwa matumizi ya ndani.
Msingi wa hoja yetu ni ule ukweli kwamba ukiuza nje gesi yote, unapata mapato
peke yake lakini unakosa faida nyinginezo. Ukiitumia ndani unapata mapato na
faida nyingine nyingi, kwa mfano, uzalishaji wa umeme, matumizi ya
majumbani,
kwenye magari na
viwandani kuzalisha bidhaa
mbalimbali. Hivyo basi
mnapoitumia ndani gesi inakuwa kichocheo kikubwa cha maendeleo ya nchi
yetu.
Vilevile tupo katika mchakato
wa kuandaa sera
ya kuwashirikisha zaidi
Watanzania (Local Content Policy) ili wanufaike zaidi na
rasilimali yao ya gesi.
Kwa sasa nimewaagiza
TPDC wajiandae kushiriki
katika utafutaji wa
gesi,
uzalishaji wake mpaka
inapofika sokoni. Wasiwe
wagawaji vitalu tu
pekee.
Katika sera hiyo
mpya pia tunaangalia
shughuli zinazoweza kufanywa
na
Watanzania ili tuone njia bora
ya kuwawezesha kushiriki. Kwa sasa
tunadhani
wanaweza kushiriki kwa urahisi katika
utoaji wa huduma
kwa kampuni
zinazofanya utafiti na
uzalishaji wa gesi
na mafuta. Wapo
walioanza na
wanafaidika. Nia yetu ni kuona
idadi yao inaongezeka.
Mabibi na Mabwana;
Tumeanza pia mchakato
wa kuiboresha TPDC ishiriki
katika uwekezaji
kwenye sekta ya mafuta na gesi kwa niaba ya Watanzania. Katika utaratibu huo,
baadaye TPDC itauza hisa zake kwenye Soko la Mitaji ili Watanzania
washiriki
moja ka moja katika kumiliki rasilimali hii muhimu.
Ndugu Viongozi wa Dini;
Mambo yote hayo yanafanyika ili kuhakikisha masilahi ya taifa
yanalindwa
na Watanzania wote
wananufaika na rasilimali
zao kwa usawa.
Changamoto
kubwa tunayoiona kuhusu ushiriki wa Watanzania kwenye utafutaji na
uzalishaji
wa mafuta na gesi ni uwezo
mdogo wa fedha, utaalamu na teknolojia tulionao.
Fedha zinazohitajika kwenye shughuli ya utafutaji mafuta na gesi, kwa
mfano, ni
nyingi mno na Watanzania wenzetu hawanazo na hakuna uhakika wa benki
iliyo
tayari kumkopesha mtu asiyekuwa nacho.
Namna nyingine ni
kuwapa maeneo ili
wao watafute wabia
wawekeze.
Lakini, mnapokuwa mnasheria
inayoshirikisha ubia baina
ya Serikali na
mwekezaji, kuamua kuacha
Serikali ili badala yake apewe Mtanzania binafsi si
uamuzi rahisi sana kuufanya. Mtu binafsi ananufaika mwenyewe wakati
Serikali
inanufaisha wengi. Ninachokiona
nafuu kufanya ni kutumia mwanya wa ushiriki
wa TPDC ili tuone baadhi ya hisa ziuzwe kwa Watanzania. Hapa kunakuwa na
ubia wa TPDC na wananchi upande mmoja na Serikali upande mwingine.
Jambo lingine tunalolifanya
ni kuhakikisha kuwa
rasilimali ya gesi
inatumika vizuri, kwa manufaa ya kizazi cha sasa na vizazo
vijavyo. Tutaanzisha
mfuko maalum wa kuhifadhi mapato ya gesi na kuwekewa masharti ya
matumizi
yake. Tutatunga sheria maalum
kwa ajili hiyo na tutafanya hivyo kwaka huu.
Mabibi na Mabwaba;
Kwa upande wa rasilimali
ya madini mabadiliko makubwa ya kiuchumi
yaliyoanza miaka 1980 katikati, Serikali ilijitoa katika uwekezaji na
ikabaki kuwa
mhamasishaji na kuweka
mazingira mazuri ya
uwekezaji. Kufuatia hali
hiyo
wawekezaji wengi walianza kuja kuwekeza katika maeneo mbalimbali
pamoja na
utafutaji na uchimbaji wa madini.
Serikali ikaweka Sera (1997) na Sheria (1998)
ya madini kusimamia sekta hiyo.
Ni kweli mapato ya Serikali na fedha za kigeni
ziliongezeka kutokana na uzalishaji wa madini. Lakini palikuwa na manung’uniko
mengi kutoka kwa wananchi kuwa hawafaidiki sana na rasilimali zao.
Kamati mbalimbali ziliundwa
kuangalia tatizo lipo wapi ili
jawabu lake
litafutwe.
Nilipochaguliwa kuwa Rais
wa nchi yetu
mwaka 2005 niliyakuta
manung’uniko hayo na kuamua tuyatafutie jawabu. Mwaka 2006 nikaunda Kamati
ya Jaji Bomani
ili ichambuwe mapungufu
yaliyopo na kutoa mapendekezo ya
hatua za kuchukua. Matokeo ya
taarifa ya Kamati ile ni Sera Mpya ya
Madini
(2009) na Sheria Mpya ya Madini (2010). Sera
na Sheria hii inalenga kuongeza
faida zaidi kwa Serikali na jamii, bila kuwasahau wale wanaozunguka
migodi.
Faida hizo ni
pamoja na kuhimiza
kampuni za uchimbaji
wa madini
kufungamanisha uchumi kati ya sekta ya madini na nyingine. Vilevile tumewataka
waongeze nafasi ya ajira kwa Watanzania na ununuzi wa huduma na bidhaa
nchini.
Aidha, tumeamua Serikali
iwe inapata hisa
katika migodi mikubwa
itakayoanzishwa siku za usoni.
Ndiyo maana tunaendelea kufanya mazungumzo
na kampuni zitazochimba uranium na
nickel. Hatujamaliza lakini
tunakwenda
vizuri.
Halikadhalika, Sheria na Sera vimeweka mkazo wa kuendeleza wachimbaji
wadogo ambao ni
Watanzania tu. Katika
kutekeleza hilo, tumeanza
kutenga
maeneo kwa ajili yao.
Changamoto kubwa inayowakabili ni
ukosefu wa mitaji,
vifaa na utaalamu. Kuhusu fedha,
tumeanzisha mfuko wa kuwasaidia na mwaka
huu wa fedha tumewatengea jumla ya shilingi bilioni 2.5. Vile vile tunakamilisha
taratibu za kuanza kuwakodisha vifaa kupitia ofisi zetu za madini za
Kanda.
Jambo lingine kubwa ambalo tunajiandaa kulifanya ili kunufaisha
wananchi
na nchi yetu
ni kutunga Sheria
itakayohakikisha kuwa madini
mengi
yanayochimbwa nchini yanaongezewa
thamani hapahapa nchini.
Hatua hii
itachangia sana kuongeza mapato na fursa ya ajira kwa watu wetu.
Nduvu Viongozi wa Dini;
Nimeyasema haya yote
kuwaonesha kuwa Serikali
haina mchezo katika
usimamizi wa rasilimali zetu za asili.
Tunafanya hayo kwa vile tunafahamu kuwa
zinaweza kutuletea maendeleo ya haraka. Lakini pia zinaweza kusababisha nchi
yetu kuingia kwenye dimbwi la migogoro inayotokana na rasilimali. Yote mawili
yanaweza kutokea kutegemea tutasimamiaje na kuzitumiaje rasilimali
zetu.
Jambo la muhimu
ni kusaidiana kuelimisha jamii
ya Watanzania namna
tulivyojipanga kusimamia rasilimali
zetu za gesi
asilia, mafuta na
madini.
Waelewe kuwa utajiri
huu ni mali
yao na hivyo
ni haki yao
kunufaika nao.
Wafahamu kuwa ni wajibu wao kulinda na kuzitunza rasilimali hizo ili
zisipotee.
Ninyi mnayo dhamana ya kuelimisha jamii waelewe nia hiyo njema ya Serikali.
Pia napenda kusema kuwa siyo kweli kwamba Serikali haijali rasilimali
za nchi au
haitaki Watanzania wafaidike nazo; siyo kweli eti Serikali inapendelea
wawekezaji
wageni kuliko wazawa na hakuna mkoa au eneo linapuuzwa au kubaguliwa. Mimi
na Serikali ninayoiongoza
tutakua watu wa
mwisho kupuuza wazawa
na
kupendelea wageni au kupuuza watu wa maeneo ambako rasilimali zinapatikana
au hazijapatikana.
Ndugu Viongozi wa Dini;
Naomba muendelee kutekeleza jukumu lenu la msingi la kulea taifa
kiroho.
Mhimize waumini wenu wawe waadilifu na wazalendo. Waache kujihusisha na
vitendo viovu vya wizi,
ubadhilifu, matumizi mabaya ya madaraka na rushwa.
Mkifanikiwa hilo, rasilimali zetu zitakuwa salama. Vile vile muendelee kuhubiri
upendo miongoni mwenu, miongoni mwa waumini wenu na miongoni mwa watu
wote. Watu wakumbushwe kuwa
sisi wote ni viumbe wa Mungu na mbele yake
sisi wote ni
ndugu na inabidi kuheshimiana
na kuvumiliana kwa
tofauti zetu.
Tukifaulu kwenye hili nchi yetu itabaki salama daima milele.
Nafahamu kuwa wapo
baadhi ya watu
ambao wanafanya vitendo
vya
kuhujumu rasilimali zetu. Wapo wanaoingia mikataba isiyozingatia
maslahi ya
taifa katika uvunaji
wa rasilimali zetu.
Wapo wengine wanaokula njama
na
wawekezaji ili Serikali
ipunjwe mapato yake. Watu wa aina
hiyo wapo katika
jamii ye yote ile na sisi kuwa nao si ajabu. Napenda mfahamu kuwa Serikali
inapinga vitendo vya aina yoyote vya kuhujumu rasilimali zetu.
Ndiyo maana
watu wa aina
hiyo wanapobainika, wanachukuliwa
hatua na vyombo
vinavyohusika. Ninyi pia
msichoke kuwafichua, wapo miongoni mwa waumini
wenu.
Mabibi na Mabwana;
Kabla ya kumaliza,
napenda kumshukuru Waziri wa
Nishati na Madini,
Profesa Sospiter Muhongo na timu yake Wizarani kwa kushirikiana na
viongozi
wa dini katika jambo hili
muhimu. Naamini hatua hii ya kuwapa taarifa sahihi
viongozi wa dini
kuhusu matumizi ya
rasilimali zetu hususan
gesi na madini
itasaidia kuongeza uelewa
wa waumini wenu
na wananchi kwa
jumla.
Watafahamu fursa zilizopo na jinsi ya kuzitumia ili wafaidike
nazo. Nakushukuru
pia kwa kusimamia vizuri utekelezaji wa sera na mipango ya Serikali
katika sekta
ya nishati na madini. Kazi yenu
nzuri inaonekana na sisi wote ni mashahidi.
Mwisho, nawashukuru viongozi
wa dini kwa
kunishirikisha kwenye
Kongamano lenu. Naamini mkitoka
hapa mtakuwa mabalozi wazuri wa kueneza
ujumbe kuwa rasilimali za Watanzania zipo kwenye mikono salama.
Baada ya
kusema hayo, napenda kutamka kuwa Kongamano la Viongozi wa Dini
kujadili
matumizi ya rasilimali
zetu za gesi
asilia, mafuta na
madini kwa amani
na
maendeleo ya nchi yetu limefunguliwa rasmi. Nawatakia kila la heri na mafanikio
katika mwaka huu wa 2014.
Asanteni sana kwa kunisikiliza.
No comments:
Post a Comment