BILLY GRAHAM:Mungu asipoipiga Marekani awaombe radhi Sodoma na Gomora;Asema wamekithiri kwa uovu.

“If God doesn’t punish America, He’ll have to apologize to Sodom and Gomorrah.”
Mwinjilisti wa kimataifa, Billy Graham (95), amesema ikiwa Mungu hatashuka kuihukumu Marekani kutokana na kufanya uasi wa kila namna bila ya kuwa na hofu, basi itampasa aiombe radhi Sodoma na Gomora miji ambayo aliangamizwa kwa moto.

Rai hiyo aliitoa wiki chache zilizopita katika sherehe ya kuzaliwa, kwake ‘birthday’ iliyofanyika wiki iliyopita na kushuhudiwa na maelfu ya watu ambapo alisema kuwa wamarekani wamekuwa wakifanya dhambi kwa namna ya kutisha na sasa imefikia hatua mbaya, hawana tena hofu ya Mungu.
Billy Graham Mwinjilisti wa Kimataifa
Mtumishi huyo ambaye amekuwa akihubiri watu zaidi ya bilioni mbili kwa wakati mmoja kwa kutumia vyombo vya habari alibainisha kwamba, Marekani ni taifa kubwa na watu wengi duniani wamekuwa wakiiga kila wanachofanya hivyo uovu wao haubakii kwao peke yao bali unaharibu sayari yote.

Alibainisha kwamba Mungu ni mwingi wa rehema, na kuwa ikiwa watamaanisha kutubu na  kuziacha dhambi zao ni dhahiri kwamba atawasamehe na kuwarehemu, lakini wakishupaza shingo wataangamia kabisa.

Mwinjilisti huyo alisema ili kuikimbia ghadhabu ya Mungu, Wakristo wote nchini humo na mataifa jirani kama Kanada,wanapaswa kukusanyika kwenye majumba yao na marafiki, majirani na  ndugu zao ili kushiriki ibada kwa pamoja kupitia Luninga zao aliyoiita “Living Room Crusade” kwa muda wa siku 40 kuanzia September 28 hadi November 6 kabla ya Uchaguzi Mkuu wa nchi hiyo.

Alisema amekuwa akihubiri kupitia Tovuti zake, na hilo ndilo litakalofanyika wakati wa kuomba msamaha, huku akibainisha kwamba, itapangwa siku maalum kwa ajili ya tukio hilo, ili kila mtu apate muda wa kushiriki; aweze kutubu, kumwomba Mungu awasamehe maovu yao ambayo ni zaidi ya Sodoma na Gomora.

Mwinjilisti huyo wa kimataifa ambaye amekuwa akimtumikia Mungu kwa miongo kadhaa sasa, alibainisha kuwa, katika kukusanyika pamoja kwenye majumba ya Wakristo, kila mmoja atapata wasaa wa kueleza uovu wake mbele za Mungu, huku akichanganua kuwa suala la utoaji wa mimba limekuwa kubwa.

Mbali na hilo, mtumishi huyo ambaye amekuwa akiwapa ushauri wa kiroho marais mbalimbali waliowahi kuitawala Marekani, akisisitiza juu ya hilo; alitolea mfano wa mji wa Ninawi  ambao ulikithiri kwa dhambi, lakini Yona alipoingia na kuwaambia kutangaza kuwa utaangamia baada ya siku 40 walisikia na kutubu.

“Ninaamini msamaha walioupata wana wa Ninawi, unaweza kutokea na kwetu, Yona alipopita na kutangaza, waliitana na kutubu,” alisema Mwinjilisti Graham.

Miongoni mwa watumishi nchini humo waliounga mkono kauli hiyo ya Graham, ni pamoja na Mwenyekiti wa ‘American for Jesus’ Anne Gimenez ambaye siku hiyo ya kutubu atakusanya watu zaidi ya laki moja huko Philadelphia, alieleza kwamba, jambo kama hilo liliwahi kutokea kipindi cha nyuma Marekani na mataifa ya Ulaya baada ya kuibuka kwa mmomonyoko wa maadili na mambo ya kiroho.

“Nadhani wazo la Billy Graham ni sahihi, taifa hili linakuwa na watu wengi wasioamini, na jambo hilo linavyokuwa kwa kiasi hichi giza huingia, lakini kama tukiomba, basi nuru itaingia,” alisema.
Mwingine ni Mwandishi wa vitabu nchini humo, Rabbi Jonathan Cahn, kwa upande wake alieleza kwamba Mwinjilisti huyo wa kimataifa amekuwa Mchungaji kwa marais na watu maarufu kwa miaka mingi, na hilo analolisema sasa ni onyo linalopaswa kuangaliwa na kutendewa kazi.

“Haijalishi ni giza la namna gani lililopo, bado lipo tumaini na wokovu pia, lakini ni pale tutakapotubu na maombi ya watu wa Mungu, unajua akisema Marekani ina shida tunatakiwa kutubu,” alisema.
Mkurugenzi Mtendaji wa Awakening America Alliance, Billy Wilson, alisema kwa upande wake atakusanya makanisa ya kipendekoste na Charismatic zaidi ya 300 na kwamba wamefurahia jambo hilo lililoletwa na Billy Graham.

Tangu mwaka 2002 mtoto wa Billy Graham, na mjukuu wake Will Graham, wamekuwa wakifanya uinjilisti katika mataifa kama 50 ya Ulaya, Afrika, Asia, Latini na Mashariki ya Kati na miongoni mwa makanisa yanayoshiriki ni zaidi ya 305,000 na kwa msingi huo watu wapatao milioni 10 wameweza kumgeukia Kristo.

Imeelezwa kwamba makusanyiko ya kusikiliza ujumbe wa Graham, yatayofanyika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kwenye majumba ya kupata kahawa, na maduka yanafananishwa na mtoza ushuri nyakati za Biblia, kuwa baada ya kutubu dhambi aliamua kuita watu na kuwarudishia kile alichokuwa akitwaa kinyume na taratibu.

Wakati huo huo Askofu E. W. Jackson, mtaalamu wa mambo ya Maji na sheria kutoka chuo cha Harvard, nchini Marekani, amewataka Wakristo nchini humo, kutokichagua chama cha Democratic, katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika November, 2012 kwa kuwa kina imani potofu.

Mwandishi Paul Stanley, wa gazeti la Kikristo nchini humo anaripoti kuwa, hivi karibuni Askofu huyo alieleza kwamba chama cha Demokratic kinawaingiza utumwani baadhi ya waamerika.
“Waachieni watu wa Mungu waende,” alisema Jackson akiwaambia Wakristo kupitia mawasiliano ya simu ni wazi kuwa Democratic ni chama cha Mpinga Kristo katika nchi hii. Wameikataa Biblia na kile Wakristo wanachokiamini, na kuhamasisha kile watakacho wao kinyume na maadili ya familia. Hii ni mbaya kwakuwa wanalimomonyoa taifa na Mungu wetu,” alisema.
Askofu Jackson alinyooshea kidole habari za hivi karibuni kutoka kwa Waliberali waliomshambulia kwa maneno mwanamichezo wa Olympic, Gabrielle Douglas, mwenye umri wa miaka 16, aliyeshinda medali ya dhahabu huko London 2012 na kusoma Biblia, lakini wapenzi wa chama hicho wakamjia juu ya kuwa haikuwa sahihi.
Baada ya ushindi wa mwanariadha huyo alisoma maandiko kwenye Warumi 12:19, yasemayo: “Wapenzi, msijilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu, maana imeandikwa kisasi ni juu yangu mimi, mimi nitalipa, anena Bwana.” Mwanadada huyo mahiri aliazimia kumpa Mungu utukufu kwa ushindi wake,” alisema katika taarifa yake ya kimaandishi.

Viongozi wa dini wameombwa kuelimisha wananchi juu sensa ya watu na makazi.

Viongozi wa dini mkoani Tabora wameombwa kuelimisha wananchi umuhimu wa kushiriki katika sensa ya watu na makazi itakayofanyika nchini Agosti, 26, 2012 ili kuisaidia serikali kupata takwimu sahihi kwa ajili ya mipango endelevu ya maendeleo ya taifa.

Mwenyekiti wa kamati ya sensa Mkoa wa Tabora, Bi. Fatma Mwassa alitoa ombi hilo kwa viongozi wa madhehebu ya dini wiki iliyopita mkoani humo ambapo aliwasihi kutumia nafasi zao wanapokuwa kwenye madhabahu kuwakumbusha waumini wao kushiriki kikamilifu katika zoezi la sensa.  
Alisema viongozi wa dini wana nafasi nzuri katika kuwahamasisha waumini wao, pindi wanapokuwa katika ibada zao, hivyo wamewahimiza kutumia nafasi hizo katika kutoa elimu ya sensa ambayo baadae itasaidia serikali kupata kupanga mipango yenye maendeleokwa wananchi wake.
Mwenyekiti huyo alisema, kutokana na ushawishi mkubwa walionao viongozi wa dini kwa wafuasi wao, wanamchango mkubwa katika kuwaelimisha umuhimu wa sensa.

Sambamba na hilo alibainisha kwamba, ushirikiano mkubwa kati ya viongozi wa dini na wananchi kwa ujumla wakati wa zoezi la sensa utaleta mafanikio makubwa na kuiwezesha  serikali kufanya maamuzi sahihi na kupanga mipango endelevu ya maendeleo ya wananchi wake.

Hata hivyo aliongezea kuwa, takwimu sahihi ya idadi ya wakazi wa Mkoa wa Tabora italiwezesha taifa kutenga fedha za kutosha kwa maendeleo mkoani humo kulingana na idadi ya wakazi wa kila Wilaya.

Alisisitiza kuwa, suala la msingi ni kuhakikisha kila mtu atakuwepo nchini tarehe Agosti 25 na 26 mwaka huu anahesabiwa mara moja.
Nao viongozi wa dini walioshiriki kwenye mazungumzo hayo, walimuahidi mkuu huyo kushirikiana kwa karibu ili kuhakikisha kuwa zoezi la sensa linafanikiwa ikiwa ni pamoja na kujua umuhimu wa sensa kwa kushiriki kikamilifu.

Akizungumza kwa niaba ya mwenzake, Askofu wa Kanisa la Anglikan Dayosisi ya Tabora, Mchungaji Elias Chakupewa alisema, viongozi wa dini watatumia vizuri nafasi walizonazo ili kuhakikisha waumini wao wanapata elimu ya sensa kwa ufasaha.

Kadhalika alibainisha kuwa, viongozi wa dini ni watu muhimu katika zoezi hili la sensa kwani,wanaamini kuwa kupitia madhabahu yao waumini wengi watapata kufahamu muhimu wa sensa na kisha kuona umuhimu kwa kushiriki na hivyo kuisaidia serikali kupata takwimu kwa ajili ya kupanga maendeleo ya taifa.

Mbali na hilo, Askofu Chakupewa amewaomba waumini wa madhehebu yote kushiriki zoezi la sensa kwani,hii itasaidia serikali ya Mkoa na taifa kwa ujumla kupanga mambo mbalimbali.


Safari ya kinabii Misri na Israeli chini ya kampuni ya Gombo Tour

Siku chache zilizopita  Safari ya kinabii Nchini Misri na Israeli iliyokuwa ikiongozwa na Askofu Gamanywa chini kampuni ya Gombo Tours ilirejea nchini ikitokea Israeli katika safari nyingine maalumu iliyoongozwa na watumishi wa Mungu, waliojifunga mkanda kumlilia Mungu aliponye taifa lao.


 Maeneo yaliyoonekana kuwa kivutio na kufanya watu kupiga picha katika maeneo hayo 
  
 Askofu Mkuu wa Huduma ya Kimataifa ya BCIC, Sylvester Gamanywa aliongoza kundi la Wakristo wa Tanzania kwenda nchini Israeli pamoja na mambo mengine kuiombea nchi.Akielezea safari hii Mkurugenzi Mtendaji wa Gombo, Bw. Willy Kulola alisema: “Safari yetu ya kinabii ilianzia Misri, tulifika salama na Mungu alikuwa pamoja nasi.Tukatembelea kila eneo kama lililopangwa, isipokuwa Gosheni kutokanana mabadiliko ya ratiba za ndege. Tulivuka bahari ya Shamu eneo walilovuka wana wa Israel wakiongozwa na Musa pakiwa pakavu! Maeneo yote ya Jangwa la Sinai walimoishi wana wa Israel miaka 40 wakirejea nyumbani, tulilala St. Catherine jirani kabisa na Mlima Sinai, ambapo siku iliyofuata tulifika katika kichaka cha Musa ambacho kiliwaka moto, bila kuteketea! Kipo mpaka leo na kinatoa majani ya kijani kibichi hadi sasa! Tulifika eneo la Haruni mahala ambapo wana wa Israel walitengeneza ndama na kumwabudu.
Baadhi ya team ya watu waliokwenda katika picha mmoja wao akiwa na Askofu Gammanywa  
Hakika Mungu aliukubali msafara huu maana ulikuwa kwa utukufu wake.Tulielekea nchi takatifu kupitia mpaka wa TABBA. Tuliporuka tu kila mmoja alionekana kujawa na furaha kubwa sana nyimbo zilitawala ndani ya basi letu! Watu waliimba kwa shangwe na furaha kukanyaga ardhi takatifu nyumbani kwetu.Msafara uliweka kambi katika mji mzuri sana wa bahari kuu ya nchi 4,yaani Israel Jordani, Misri na Saudia. Huduma ilikuwa nzuri sana, vyamwilini walivipata na kuvikubali na siku hiyo tulikuwa na ibada nzuri sana usiku.
Safari yetu ilianzia katika maeneo ya Tarbenacle, lililopo eneo la kumbukumbu ya mfano wa hema ya kukutania, hakika kila mmoja alishangazwa, na hata Askofu Mkuu Gamanywa alisikika akisema:“Nimepata picha mpya isiyoweza futika katika ufahamu wangu wa utumishi.”
Tulipita Masada, dead Sea na tukaenda Jericho, jirani kabisa na mlima wa majaribu ambao Yesu alikaa huko akiomba na kufunga kwa siku 40, na hata shetani kumjaribu. Tulilala Jerusalemu katika Hoteli nzuri,tulipata chakula kizuri sana, vyumba vizuri kiwango cha juu sana kila mmoja alikiri HAKIKA HII NI NCHI YA ASALI NA MAZIWA.

Askofu Gamanywa na Mtume Nyaga walipokuwa Israel 
Apostle Nyaga alitamka wazi kuwa ufahamu wake umebadilika kwa vile alivyoelewa mwanzo na alivyoona sasa.Tumefika katika jumba la makumbusho ya mauaji ya Wayahudi milioni 6,wakiwamo watoto Milioni 1.5 haya kama jasiri ukifika mahala hapo lazima machozi yatatiririka tu! Tumetembea Galicantu eneo ambalo Yesu Kristo alifikishwa kwa Kayafa na Petro kumkana mara tatu. Tumefika Golgotha alikosulubiwa Yesu Kristo akafa na kufufuka, wapendwa waliingia ndani ya kaburi la Yesu na kuliona na baadaye kufanya ibada nzuri sana. Pia meza ya Bwana iliyoongozwa na Mkuu wa msafara Askofu Sylvester Gamanywa na kumalizia kwa kutoa sadaka kubwa nzuri ya kuibariki Israeli na kusaidia kulitunza eneo hilo. Tulienda pia chumba cha juu mahala ambapo Yesu alikula chakula cha mwisho na wanafunzi wake na mahala walipojazwa Roho Mtakatifu kwa mara ya mwisho MAOMBI YA NGUVU.

Mtendaji wa Gombo Tours, Bw. Willy Kulola aliyekuwa mratibu wa safari nzima,akiwa katika kibao kinachaoonesha njia inayokwenda katika mlima ambao Yesu alijaribiwa na shetani.   
Katika eneo hili “upper room” chumba cha juu! Ni mahala ambapo watu walimlilia Mungu kwa nguvu zote, hata ikawafanya wazungu wa makundi kutoka mataifa mbalimbali kushangaa jinsi watanzania walivyokuwa wamejiachilia mbele za Mungu. Maombi yaliwafanya wazungu hao kushindwa kukaa eneo hilo maana tayari ulikuwa ni mpasuko wa anga, Roho Mtakatifu alikuwa ameshuka isivyo kawaida.
Maombi mengine ya kushtua ambayo mpaka viongozi wa Dini ya Kiyahudi naaskari wa ulinzi na Wayahudi walistaajabu ni katika ukuta wa maombi na maombolezo! (Wailing wall) Apostle Nyaga na Mchungaji Amasi walinena kwa lugha za mbinguni, kwa utukufu mkubwa sana, nguvu ya maombi na kunena iliwashukia kiasi Wayahudi walikuwa wanashangaa na kujikusanya wakiwazunguka kushangaa ni kitu gani, maana kwa kipindi kirefu haijatokea.Ilikuwa safari ya kipekee.

Baadhi ya watu aliokwenda wakiwa kwenye maombi.        

Gombo Tours – Experience The wonder of God!
gombotours@hotmail.com
SIMU: 0713 -304984; 0767 -  304984; 0717 – 798991; 0754 – 333125.
TUPO KARIAKOO ROUND A BOUT jijini Dar es Salaam.

Kituo cha Sheria watoa elimu ya Katiba Kanisani

Kituo  cha Sheria na Haki za Binadamu, kimetoa elimu ya katiba katika kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG), Ubungo Christian Centre la jijini Dar es Salaam ili waumini waweze katika mchakato wa kutoa maoni yao katika mchakato wa marekebisho ya uundwaji wa katiba mpya.

Elimu hiyo ilitolewa na wanasheria wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, kwa muda wa siku mbili kanisani hapo, ambapo walibainisha kuwa, wakristo wamekuwa wakikutana na changamoto mbalimbali ambazo wanaweza kutoa maoni na wakaweza kupata kile wanachokitaka pasipo kuvunja sheria.

Logo ya Kituo  cha Sheria na Haki za Binadamu

Anna Henga, mmoja wa wanasheria wa Kituo hicho cha Sheria na Haki za Binadamu chenye makao makuu yake Kijitonyana jijini Dar es Salaam, alisema Ibara ya 19 inayozungumzia uhuru wa kuabudu, alieleza kwamba wakristo wanapaswa kutoa maoni yao ili kuondoa dukuduku na ukiritimba unaohusu vibali vya kuhubiri Injili, ambavyo vimekuwa vikilalamikiwa na wachungaji kwamba vinawanyima uhuru.

Akitilia msisitizo juu ya hilo alichanganua kwamba, Katiba iliyopo ambayo ni ya tano ina viraka vingi ambavyo kwa sasa vina mapungufu yanayohitaji maoni ya watu wa Mungu ili kuandikwa katiba mpya; alivitaja vichache, kwamba ni pamoja na masuala ya dini kutoingiliwa na serikali kabisa kwa kuwa uhuru wa kuabudu unapaswa kuwekwa katika haki za binadamu; ukiheshimiwa na usiotakiwa kuguswa .

Mbali na hilo alieleza kwamba, wakristo wengi wanafikiri kuomba tu na kukaa kimya ndiyo jibu la matatizo yao, huku akibainisha kwamba hata mtume Paulo alipopelekwa kwa Pilato ingawa aliomba lakini ilipofika wakati wa kujitetea alisema na yeye ni Mrumi wa kuzaliwa na hilo lilimfanya kuachiwa huru.

Kama hilo halitoshi alibainisha kwamba, wakristo wengi wamekuwa na kigugumizi juu ya kuwepo kwa mahakama ya Kadhi nchini, ambapo alieleza kwamba kwa maoni yao kunaweza kuleta mahakama moja kwa watu wote, kwa haki zote hupatikana mahakamani na katiba ndiyo sheria mama.

“Ikiwa mtanyamaza basi mtaiona ikianza kufanya kazi,’ alisema Bi. Anna.

Kuhusu mfumo wa Serikali; alieleza kwamba, yapo mambo ambayo yanalalamikiwa mara kwa mara na wananchi ambayo ni kuhusu Tume ya uchaguzi, ambapo alisema inabidi kuwepo kwa tume huru; isiyoundwa na chama kimoja wakati huu wa vyama vingi. 

Mwonekano wa Katiba ya Tanzania kwa juu.
Akitaja baadhi ya udhaifu uliopo ndani ya katiba iliyopo alisema kuwa ni; madaraka makubwa aliyo nayo rais, haki za binadamu kuwekwa wazi kuhusu Afya, elimu na walemavu, Jaji Mkuu asiwe wa chama kimoja, hukumu ya kifo iliyopo si haki kuondoa uhai wa mwingine, vyombo nyeti kama Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali na Spika wa bunge asitoke katika chama fulani.

Aliendelea kueleza kwamba udhaifu mwingine ni; Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa, tume ya maadili ya viongozi, pia mihimili mikuu mitatu: Mahakama,  Bunge na serikali iwe huru, isiingiliwe au kupata shinikizo kutoka upande wowote.

Pia aliongeza kwa kushauri kuwa ni vyema Muungano wa Tanzania na Zanzibar uangaliwe upya, pia Tume ya Uchaguzi kuwa huru.

“Tanzania ni nchi isiyoongozwa na dini inayofuata mfumo wa kisekula, haifungamani na dini yoyote jambo ambalo limeifanya nchi kuwa shwari bila kuwa na vita vya kiudini; hivyo katiba isiingize masuala ya imani ya mtu au watu,” alisema.

Akiwashukuru waalimu hao; Mchungaji Paulo Mulokozi wa TAG Ubungo Christian Centre (UCC) alihimiza Wakristo kushiriki kutoa maoni yao katika mchakato wa kupata katiba mpya ya taifa na pia kushiriki vyema katika sensa inayotarajiwa.

“Tumekuwa tukiliombea taifa letu kila mara, lakini hiyo haitoshi lazima tushiriki kikamilifu kutoa maoni yetu katika mchakato wa kuunda Katiba mpya, kushiriki sensa na kuchukua fomu za uongozi inapobidi,” alisema Mchungaji Mulokozi, na kuongeza: “Tutakuwa hatutendi vyema kama watu wa Mungu tusiposhiriki kikamilifu kama watanzania.”
  
Mchungaji aliwapongeza na kuwashukuru wawezeshaji hao kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu; Bi. Flaviana Charles na Anna Henga, na kusisitiza Wakristo wengi kujitokeza ipasavyo katika kutoa maoni, na hata katika kupiga kura; pia kushiriki kwenye kura na sensa.


Love Tanzania Festival kuacha historia Tanzania

Love Tanzania Festival imeweka historia katika Nchi ya Tanzania Baada ya kumalizika kwa kufanya maajabu katika Festival hiyo katika viwanja vya Jangwani Jijini Dar es salaam.

Love Tanzania Festival ilikuwa imeandaliwa na mtumishi wa Mungu  Andrew Palau imeshilikisha wachungaji kutoka makanisa mbalimbali Nchini,Mtumishi wa Mungu Andrew Palau katika event hiyo alihubiri na idadi kubwa ya Watanzania kuokoka na kumpa Yesu Maisha yao.

Love Tanzania Festival pia ilitawaliwa na Massanja Mkandamizaji wa Original Comedy kwa kile alichofanya kwa kuushuhudia umati wa watu kuwa ameokoka na Yesu ni Bwana katika maisha yake

Pia wanamuziki wa Tanznia waliojumuika katika Love Tanzania Festival ni Christina Shusho,Upendo Kilahiro,Pastor safari na team aliyokuwa anaiongoza.

Kwa upande wa wa waimbaji wa Kimataifa alikuwepo Don Moen,Dave Lubben na Nicolle C Mullen 
ambao katika event hiyo walikuwa wakishilikiana na umati wa watu ulikuwa ukiimba pamoja nao kutokana na idadi ya kubwa ya watu kuwa wanajua nyimbo zilizokuwa zikimbwa katika tamasha hilo.
Andrew Palau Mwinjilisti wa Kimataifa na mwandaaji wa Love Tanzania Love Festival

Andrew Palau Akihubiri katika Love Tanzania Love Festival

 Dave Lubben


                                                                         Don Moen


Watu na hawakusita kutumia simu na Ipad zao kuchukua kumbukumbu za Don Moen




 
Nicole C Mullen


Christina Shusho na  Upendo Kilahilo wakiwakilisha kwa stage
Watu wa  Mataifa mbalimbali walijitokeza kumtukuza Mungu katika Love Tanzania Festival
Maelfu ya watu walimpokea Yesu kama Bwana na Mwokozi wa Maisha yao
Massanja Mkandamizaji wa Original Comedy hakusita kuushuhudia umati wa watu kuwa ameokoka na  aliyotendewa na Yesu katika maisha yake.
The Voice na Don Moen
Christina Shusho na  Upendo Kilahilo wakibadilishana mawazo na Nicole C Mullen



TAG Uchaguzi mkuu Dodoma katika picha

Uchaguzi Mkuu wa Kanisa la TAG kumchagua Askofu Mkuu na viongozi mbalimbali wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God(TAG) uliofanyika wiki iliyopita katika ukumbi wa Chimwaga Dodoma,haya ni baadhi ya matukio ya uchaguzi huo katika picha.
Baadhi ya viongozi wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God walihudhulia uchaguzi huo uliofanyika katika ukumbi wa Chimwaga Dodoma.
Katika Uchaguzi huo  Dk. Barnabas Mtokambali ndiye aliyeapatikana mshindi kuwa Askofu mkuu wa TAG na upande wa katibu Mkuu Ron Swai ndiye aliye ibuka mshindi.

Askofu Dr. Mtokambali akifuta Machozi ya furaha baada ya ushindi huo.

Katibu Mkuu Ron Swai akitoa Neno la shukrani kwa wajumbe kwa kumchagua kuwa Katibu Mkuu wa Kanisa hilo.

Baadhi ya viongozi wa Kanisa la TAG walioudhulia uchaguzi huo wa kwanza kulia ni Askofu Mkuu wa Kwanza wa TAG Emmanuel Lazaro, Askofu Mkuu wa wapili wa TAG Ranwell Mwanisongole na Viongozi wengine.

Baadhi wa wajumbe wa uchaguzi huo wakimpongeza Askofu Dk. Barnabas Mtokambali

Wajumbe wa uchaguzi huo wakifurahia ushindi uliopatiaka

Wazee na Viongozi mbalimbali wa TAG wakiwaweka wakfu Dk. Barnabas Mtokambalina katibu Mkuu Ron Swai baada ya uchaguzi huo.


Love Tanzania Festival yaanza siku ya Jana kwa Viwanja vya Jangwani kuwekwa wakfu.

Love Tanzania Festival imeanza jana kwa Viwanja vya Jangwani kuwekwa wakfu,Pia watendakazi kupewa madara namna ya kuhudumia watu,Idadi ya watu inayotegemewa kuwepo ni kubwa sana ikidhaniwa kuwa haijwahi tokea Tanzania.
 Love Tanzania Festival imekutanisha watumishi wa makanisa mengi nchini na kusahau tofauti zao za kidini kwa ajili kuujenga mwili wa Kristo.



Andrew Palau akihubiri jana wakati wakiweka wakfu viwanja hivyo.
Jukwaa linalo tumika katika Love Tanzania Festival likiwa limetoka Nchi ya jirani zetu Uganda na Sound system kwa Ajili ya Ubora wa Event hiyo.
Pona,Sam na wengine wakifanya mazoezi kwa ajili ya Sound check siku ya jana kakika viwanja vya Jangwanai
Christina Shusho,Upendo Nkone na Pastor Safari wakifanya mazoezi kwa ajili kuhakikisha kila kitu kina kuwa sawa.

Watendakazi wakipewa darasa jinsi watakavyo hudumia watu katika Event hiyo



Pastor Safari na Obedi wa The Voice wakiteta jambo baada ya majaribio

Upendo Nkone akisalimiana na Baadhi ya Viongozi wa Makanisa waliokuwepo viwanjani hapo,kwa mbali Christina Shusho naye alikuwepo.



Wanamziki wakisikiliza Neno kwa makini kutoka kwa Mtumishi wa Mungu Andrwe Palau








Upendo Nkone na Christina Shusho mara wakutana na camera ya Blogger

Dk. Barnabas Mtokambali aibuka mshindi katika uchaguzi Mkuu wa Kanisa la TAG uliofanyika Dodoma.

Katika kile kilicho kuwa kinasubiliwa kwa mda katika swala Uchaguzi Mkuu wa Kanisa la TAG kumchagua Askofu mkuu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God(TAG), ambao unafanyika kila baada ya miaka minne unaoambatana na uchaguzi wa viongozi wa ngazi mbalimbali uliofanyika mkoani Dodoma.Hivi sasa matokeo yaliopatikana kwa masaa machache yaliyo pita ni kwamba Dk. Barnabas Mtokambali  aliyekuwa ameshika kiti hiko kwa muda wa miaka minne aibuka tena kidedea kwa asilimia 93 baada ya kuwa ameamua kukitetea kiti hicho kwa mara nyingine tena,Hivyo atakuwa Askofu mkuu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) kwa miaka minne tena.

Dk. Barnabas Mtokambali
 

Ushindi huo ambao ameupata mara baada ya wachungaji 20119 kuandika majina ya kumpendekeza atakayegombea nafasi hiyo ili aweze kupigigiwa kura ambapo kabla haijafika katika mchakato huo wa kura hatimaye aliibuka kidedea kutokana na jina lake kurudia mara 1969 ambapo ni sawa na asilimia 93 kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi wa Viongozi katika Kanisa hilo.

Awali kabla ya mchakato huo kuanza Askofu Dk. Mtokambali alitoa hotuba kali ya wachungaji kuacha kuenenda ki binadamu na kwamba waache kupiga kampeni na kutoa, kupokea Rushwa.

Pia kwa nafasi ya Makamu Askofu ndio hatua iliyofuata baada ya kumpata Askofu Mkuu ambayo ilikuwa ikigombewa na wachungaji kadhaa lakini hatua zilivyozidi kusonga walikuwa wakijitoa hadi mwisho kubaki wawili.Waliowania nafasi hiyo ambapo Magnus Muhiche na Raulent Kameta ndio walio wania kiti hicho,Magnus Muhiche kuibuka Mshindi kwa kura 1398 na Raulent Kameta kupata kura 618 hadi anapatikana mshindi inasemekana imerudiwa mara nne (4),walikuwa hawafikii asilimia zilizokuwa zinamfanya mtu kuwa mshindi,
Ron Swai ndiye aliyeibuka mshindi katika nafasi ya Katibu Mkuu wa Kanisa.Chanzo cha habari kikizungumza na blog hii katika kubainisha hayo!

Maandalizi ya Mpinga Kristo........., Umoja wa Dini 5O wazua Balaa!

Papa Benedict, Lutheran wahusika,Makanisa Mengine yajiweka kando pia Quran na Biblia zasomwa kwa pamoja

Wakati wengine wakiendelea kubishania uhalali wa ibada za mafuta na vitambaa, hatua kubwa ya kufikia umoja wa kidini yaani United Religious, utakaokuwa na nguvu kuzidi Umoja wa Mataifa (UN) imefikiwa hivi karibu, baada ya dini zaidi 50 kuandaa ibada siku ya Jumapili na kutumia Bibilia na Qura’n.

Taarifa iliyonukuliwa na Gazeti la New York Times, ilisema: “Mihimili mikuu mitatu kuelekea mfumo mpya wa dunia ambayo ni Umoja wa kiuchumi duniani, Serikali moja na Dini moja. Masikio ya wengi yameelemea kwenye mihimili miwili zaidi kuliko ule wa tatu ambao wameupuuzia. Lakini huu wa tatu ambao ni dini ya pamoja (kwa maana ya imani moja) ndio usukani na sasa unakaribia kufikiwa. Huu ndio unaojulikana kama ‘Interfaith.’ 
Papa Benedict XVI
 Makongamano na mikutano inaendelea kuongezeka kwa kasi siku hadi siku duniani, huku viongozi wakuu akisisitiza kuwepo kwa ushirikiano wa pamoja. Imani ya kuwa na dini moja "Interfaith" imekuwa ikisisitizwa kote duniani na viongozi wa dini mbalimbali wakitumia mashirika (NGOs), mashirika ya misaada, na taasisi mbalimbali, wanasisasa wakubwa wametumiwa kuipa msukumo kwa fedha nyingi katika sayari hii.”
Kisha taarifa hiyo iliongeza: “Hivi karibuni baadhi ya makanisa katika Amerika yamekwenda mbali zaidi katika suala hilo. Juni 26, mwaka huu, Kathedral ya Kitaifa (National Cathedral) katika Jiji la Washington D.C. iliandaa ibada ya pamoja  na zaidi ya makanisa 50 yalishiriki kusoma Quran wakati wa Ibada ya Jumapili.”
Wachambuzi wa siasa dini wanaeleza kuwa hiyo ni hatua katika mkakati mkubwa wa kuundwa kwa shirikisho kubwa la kidini katika kipindi cha mpito kuelekea kuzaliwa rasmi kwa umoja wa kidini  ulimwenguni, ukishinikizwa kwa kipengele cha haki za Binadamu.
Somo kuu katika Jumapili hiyo lilikuwa “Kushirikishana imani, Kushirikiana maombi na kuelewana.” Lengo likielezwa kuwa ni kuonesha upendo wa Wakristo kwa Waislamu waishio Amerika.
Miongoni mwa makanisa yaliyoshiriki ni: Christ Church lililopo jijini New York City,
All Saints Church lililopo Pasadena California, Park Hill Congregational huko Denver,
Hillview United Methodist lililopo Boise, Idaho First United Lutheran, katika mji wa San Francisco, St. Elizabeth's Episcopal Church, huko Honolulu, Makanisa makubwa (dini mbalimbali) yapatayo 26 katika Amerika yamehusika na mpango huo.
Interfaith logo
Imeelezwa kuwa usomaji huo wa Quran ni mpango maalumu wa kulainisha dini zenye misimamo mikali ili kuonesha kuwa upo uwezekano wa kufanya ibada pamoja na kumaliza tofauti zilizowatenga zamani.
Mpango huo mkubwa unatarajiwa kua endelevu ukijumuisha Wakristo, Wayahudi na Waislamu kwa njia ya kusikia na kusoma aya kadhaa, za Qur'an mara kwa mara ili watu wazoee kuwa pamoja na mwisho waunganishe mioyo yao pamoja na kuabbudu pamoja.
Kwa mujibu wa waandaaji wa mpango huo, Interfaith, Waamerika wana uhuru wa kusoma Quran popote wanapotaka. Lakini kwa Wakristo hawana nafasi ya kusoma na kujifunza kitabu hicho, hivyo kuwepo kwa utaratibu wa kuisoma kila Jumapili wanapokutana kanisani kwenye Ibada na kutawafanya waielewe na kuwa na ‘umoja’ na Waislamu na kuonyesha kutowabagua; jambo ambalo linaonesha dalili ya kuzaliwa kwa kitu kipya duniani.
Wakati huo huo, baadhi ya viongozi wa Kikristo duniani hawako radhi na muendelezo huo. Brannon Howse, mmoja wa viongozi mashuhuri alisema: “Watu hao wamekana uungu wa Yesu Kristo; wamekana ukweli wa maandiko matakatifu; wamekana uvuvio wa Biblia, ni vipi tushirikiane nao na kusoma kitabu chao kwenye ibada zetu?”

Qur'an

Kisha aliendelea: “Inasikitisha, hii siyo mara ya kwanza. Ukweli ni kwamba umoja huo umepata nguvu miongo kadhaa na baadhi ya wakuu wa dini ulimwenguni wamehusika.
Kwa mfano; habari zilizopatikana kupitia CNS zinaeleza kuhusu muungano mkubwa ‘interfaith’ wakati Papa alipotembelea jiji la Washington 2008.”
Alisema kuwa wakati Papa Benedict XVI alipofika kituo cha, Pope John Paul II Cultural Center kilichopo Washington kwa mkutano wa jioni wa dini zote ‘interfaith’ zilikuwepo dini mbalimbali ambazo hapo awali isingekuwa rahisi kukutana na kuabudu pamoja. Waislamu, Wahindu, Wayahudi na dini nyingine zilipata nafasi zilishiriki; isipokuwa Assemblies of God,hii haikuthubutu hata kusogelea.
Viongozi wa Dini kubwa katika Amerika wanahusika sana na umoja huo "Interfaith movement," kwa mfano; Brian McLaren, mmoja wa viongozi wa juu wanaoendesha umoja huo, inasemekana kuwa mwaka 2009 alisherehekea Ramadhan na hata kuvaa mavazi yanayovaliwa na wahusika.
Katika sherehe hiyo; Rick Warren, mshirika wa Baraza la Uhusiano wa Nje, alikuwa Mgeni rasmi na mnenaji kwenye Kongamano la kitaifa la Waislamu huko Amerika ya Kaskazini, (Islamic Society of North America).
Baadhi ya viongozi wa makanisa wakiwemo Rick Warren, Robert Schuller, Brian McLaren, Richard Cizik na Bill Hybels walitia sahihi barua kwa Jumuiya ya Kiislamu iliyokuwa na kichwa kisemacho;  ‘Kumpenda Mungu na jirani yako’
Barua hiyo iliweka bayana kuwa viongozi wa Kikristo wanamtambua Allah kuwa sawa na Mungu wa Wakristo.
Barua hiyo ilisema:“Kabla hatujashikana mikono; katika kukubaliana na barua yetu, tuwatake radhi kwa kuomba msamaha kwa Muumba wa wote. Kwa Waislamu muumbaji ni Allah.
Kwa barua hii, baadhi ya viongozi wa Kikristo wanamuomba na wanatubu kwa jina la Allah, na wanamtambua kuwa ndiye Mungu.”
Kama tulishindwa kurejesha amani na kuwa pamoja, sasa tumesahihisha mawazo yetu na kwamba tunaweza sasa kutakasa nafsi zetu.”
Barua hiyo ndiyo iliyozua hofu duniani kuwa  huenda wakati sasa umewadia wa baadhi ya viongozi kudhihirisha hali ya vuguvugu  na kukosa msimamo wa kiimani.
“Kwa kweli  huu ni usaliti wa hali ya juu, kuandika barua na kueleza kuwa Allah ndiyo Mungu anayeabudiwa na Wakristo  ni mwanzo wa kuelekea katika  dini moja na utawala wa Mpinga Kristo,” alisema Mchungaji Jonathan Emmanuel, wa Nigeria.
Alisema kuwa anautazama mwelekeo huo kama jambo la hatari kwa kuwa Biblia katika  kitabu cha
Yohana 14:6 , Yesu anasema: “...Mimi ndimi njia, na kweli na uzima; mtu haji kwa baba ila kwa njia ya mimi.”
Kiongozi huyo alisema kuwa ukweli wa ki-Biblia uko wazi na wala hauna kificho kuwa Yesu ndiye njia pekee ya kufika mbinguni. Ikiwa unaamini hivyo  ni vipi uandike tena barua ya hatari kama hii ya  kumhusisha Allah na ufalme wa Mungu?
Kisha aliongeza: “Katika amri kumi; awali kabisa tunakutana na maandiko yasemayo; “Usiwe na miungu mingine ila mimi. Usifanya sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu chochote kilicho juu mbinguni , wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia. Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, BWANA, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukizao, nami nawarehemu maelfu  wanipendao, na kuzishika amri zangu.”
 (Kutoka 20:3-6) 

Source Jibu La Maisha

Kanisa lagomea mashoga kununua nyumba wengine wapigwa mawe hadi kufa.

WATU wawili wa jinsia moja (mashoga), walioonyesha azma yao ya kutaka kuishi pamoja kama mume na mke, wiki iliyopita walijikuta katika wakati mgumu baada ya kukataliwa kununua nyumba huku mmiliki wa Bakery akigoma kuwauzia keki ya harusi yao na wengine kupigwa mawe hadi kufa nchini Kenya.

Hayo yalitokea wiki iliyopita nchini Marekani, baada ya watu hao, waliokuwa kwenye uhusiano wa siri kwa miaka miwili kuamua kuudhihirishia ulimwengu kwamba wao ni mume na mke, kinyume na mpango halisi wa Mungu ambao ni ndoa ya muke na mume.




Sakata lenyewe lilikuwa hivi; Kanisa moja lilikuwa likiuza nyumba yake (mansion), tangazo likachapishwa kwenye mitandao na watu wakajitokeza kutoa ofa, lakini miongoni mwao walikuwemo mashoga wawili.

Katika kuchekecha nani wa kununua nyumba hiyo, kanisa likafikia muafaka kwa mashoga hao ambapo awali hawakuwatambua kama ni mume na mke, wenye mahusiano haramu.

Baada ya kubaini uchafu huo, huku watu hao wakiwa na pesa kamili, ghafla waliambiwa na wauzaji ambao ni kanisa kwamba, wanasikitika hawatoweza kuuza jumba hilo kwa watu ambao ni mashoga, kwa kuwa matumizi yake yataendana na wahusika.

Mashoga hao ambao ni; Bw. Alain Beret na mkewe Bw. Jim Fairbanks, baada ya kuambiwa habari hizo, huku wakijiandaa kufanya sherehe ya kukata na shoka, mara waingiapo ndani ya Mansion hilo, walinga’aka.

“Huku ni kunyanyapaliana, jambo kama hili kufanyika katika uso wa dunia mapema kiasi hiki ni mbaya, ni lazima likomeshwe,” alisema huyo anayeitwa mume (Beret) na kuongeza:

“Kwa kweli siamini hiki ninachokiona, tuko katika karne hii ya 21, lakini bado tuna kitu cha ubaguzi.”

Hata hivyo msemaji mmoja wa kanisa hilo akiongea na mashoga hao aliwaambia: “Nimeongea na Askofu juu ya nia yenu ya kununua jumba hili, nilimueleza nyie ni watu wa namna gani, kwa msingi huo tunasikitika kutoendelea mbele kuhusiana na jambo hili, hofu yetu ni kuhusiana na matumizi yake.”

Jumba hilo la kifahari lilijengwa mwaka 1890 ambalo pia ni la kihistoria.

Sambamba na hilo, mmiliki wa duka moja maarufu kwa kuandaa keki za sherehe nchini humo mjini Colorado, Bw. Jack Phillips amekataa kuwauzia keki mashoga wawili waliotaka kufunga ndoa wiki iliyopita.

Duka hilo lilijulikana kwa jina la Masterpiece Cake Shop, imeelezwa kwamba lilipokea oda ya kutengeneza keki, lakini lilipobaini kuwa mashoga ndio walikuwa katika shamra shamra za kufunga ndoa wakagoma kuikamilisha.

Katika mkasa huo, Bw. Dave Mullin na Bw. Charlie Craig,waliambiwa na mmiliki  wa duka hilo kuwa  asingeweza kuuza bidhaa zake kwa watu wanaotaka kufanya mambo kinyume na mpango wa Mungu, lakini watu hao walidhani alikuwa akiwatania, ndipo siku ya harusi ilipowadia na kwenda kuchukua keki wakakutana na ujumbe ule ule.

Baada ya jambo hilo, ambalo waliliona ni udhalilishaji; waliingia kwenye mitandao ya kijamii na kutoa maoni yao yaliyosomeka namna hii: “Tumekuwa kwenye mahusiano kwa muda mrefu, tukaamua sasa kuwa kitu kimoja kwa kufunga ndoa, lakini cha ajabu tulipoenda kwa muuzaji maarufu wa keki mambo yakawa mamabaya.” 

Kisha aliendelea: “Tulitarajia kuchukua muda mwingi kuelezea namna tunavyotaka keki yetu iwe, lakini haikuwa hivyo, neno langu la kwanza lilikuwa, tunataka kuoana na akatukatiza hapo hapo, tulishangaa.”

Hata hivyo baada ya maoni ya Dave Mullin na Charlie Craig kutundikwa katika mitandao hiyo ya kijamii, (Facebook) watu zaidi ya 1000 walikasirishwa na kitendo hicho, huku wengine  wakiamua kwenda moja kwa moja hadi kwa mmiliki kupinga alichokifanya muuza keki huyo.

Miongoni mwa waandamanaji waliokwenda moja kwa moja hadi Masterpiece Cake Shop,  ni Bw. Cate Owen aliyeeleza kwa uchungu kuwa, wamekuwa wakisapoti biashara za wazawa, lakini ikiwa naye anatoa huduma kwa ubaguzi basi na wao hawatakuwa radhi kumuunga mkono.

Wakati hilo likifanyika huko Marekani, nchini Kenya nako mashoga wawili walijikuta mikononi mwa kundi kubwa la watu wenye hasira kali baada ya kubambwa kona wakivunja amri za Mungu katika maeneo ya Kayole, ambapo walipigwa mawe na mmoja kufa papo hapo, mwingine akifanikiwa kukimbia, lakini mwisho wa siku mwili uliacha roho kama mwenzake.

Mashoga hao ambao walikuwa ni baba lishe (food venders), inadaiwa kwamba walikuwa wakifanya mchezo huo mchafu kwa miezi kadhaa.

Inaeleza kuwa siku ya tukio walikubaliana kukutana karibu na majengo ya Kanisa Katoliki, eneo linalobainishwa kwamba lina msitu kiasi fulani, wakiwa hapo huku giza likinyemelea walianza kazi iliyowapeleka na ndipo mtu mmoja alipowaona na kuita watu na zoezi zima likachukua nafasi yake.


Wakati zoezi hilo likiendelea mmoja aliweza kukimbia, huku akimuacha mwenzake aliyetambulika kwa jina moja la Kamau akishambuliwa vikali.

Baada ya mauaji ya Kamau, kundi hilo lilimtupa kwenye dampo ambalo lilikuwa karibu na walipokuwa wakifanya ushenzi huo.

Hivi karibuni Rais wa Marekani, Barrack Obama alitamka hadharani kutambua ndoa za jinsia moja, jambo lilipokelewa kwa vifijo na wachache na wengi hasa watumishi wa Mungu kupinga vikali, huku wachambuzi wa masuala ya siasa wakichanganua kuwa hilo limekuja ili kumng’arisha katika medali za siasa, hasa ikizingatiwa wanatarajia kuwa na Uchaguzi Mkuu wa urais mwezi Novemba 2012.