Pastor Vijana Wanaohudumu Kazi Full Time

Baadhi ya Watumishi 10 Vijana Ambao wanamtumikia Mungu katika Kizazi Hiki.
 Watu Wanaokaribia Kustaafu wengi Walikuwa ndio Wanaokimbilia Kazi Ya Utumishi Wa Mungu.

Miaka Michache Iliyopita Kumekuwa na Wachungaji Wengi Sana Vijana Ambao Wameamua Kuwa Full Time Ministers Kwa Maana ya Kuchunga Makanisa na Wengine Kuwa na Huduma Kabisa ambazo zimekuwa zikiandaa Makongamano na Mikutano Ya Nje Kwa ajili ya Injili.

Watumishi hawa ni full time Worker kwenye Ufalme wa Kitumishi. Gonga hapa



 Pastor Justine Caleb ni Pastor wa Goshen Christian Miracle Centre ambao Kanisa liko Pale Ilala Boma.

 Pastor Isaac Mallonga, ambaye anahuduma yake Tehillah Ministry akiongoza Ibada za Kila Ijumaa pale Tehillah Mbezi Tangi Bovu pia huwa anahuduma za nje hasa kwa mashule ya secondari na Vyuo..
 
  Pastor Matthew. Pastor Matthew pichani akiwa ni Mke wake Rebecca Walianza Kazi Morogoro from Zero, na Kwa sasa Yuko Mkoani Mbeya akisimamia Radio Ya TAG na Pia Kufanya Huduma Vyuoni, Kwa Vijana na Kwenye Makanisa Mbalimbali, Pia ni Director Wa Friends On Friday Mbeya.

 Apostle Daniel Musokwa, Ni Miongoni mwa founder wa Tehillah Ministry. Daniel ni Senior wa Tehillah Mkoani Mbeya.

Pastor Daniel yuko Arusha anamtumikia Mungu Kama Youth Pastor. 

 Pastor Philip Kimaro Wa Calvary Arusha Pastor Philip Kimaro ni Mchungaji. Kati Ya Ma-Pastor ambao Wamesababisha Kanisa la Calvary kusifika kwa Praise and Worship hasa ile ya Kila Mwezi basi Pastor Philip ni nguzo mojawapo.

Ministry Of Jesus Christ" John Sembatwa.huduma ya Mafundisho Ya Neno la Mungu na Maombezi eneo la Kimara.
 Pastor Wanza Temu. Wakati Tehillah Dar inaanza hawa ndo walikuwa Waasisi, Mungu akamvuta huyu Jamaa kufanya kazi na Christ Embassy Tanzania. Wanza ni Pastor wa Christ Embassy hapa Tanzania eneo la Mbezi Makonde.
 Uliza Mwanza town utaambiwa Mwanza International Community Church utaambiwa. Alinza kama Muimbaji lakini aka-Catch fire, sasa hivi anaongoza Kanisa Mwanza Town. Pastor Zakayo Nzogere. Kanisa lake ni Mojawapo ya Makanisa ambayo vijana wengi sana pamoja na wanafunzi wanasali. Anapiga Neno si Mchezo, Prayers ndo usiseme, Kuimba mule mule, nakumbuka mwaka 2009 Uwanja wa Taifa akiwa Mc wa Campus Night alishika Kipaza kwenye wimbo wa "Storm Is Over Now". Kati Ya Message zako zooote nilizowahi Kuzisikia ambayo mpaka kesho sijaisahau "Strengthening Yourself In The Lord"-2010. Unaweza Mpata Facebook kama utakuwa unaenda Mwanza.
Huyu amevuka Border, Pastor Freddy Okello, Alipokuja Tanzania na Kusema Mungu amemwambia aje kutumika Tanzania niliona ni kati ya watu wa ajabu, from Uganda to Tanzania. Pastor Freddy ni Mchungaji wa Upper Room Ministry Kanisa Lake liko Opposite na Mlimani City Dar-es-Salaam. 

Ninaamini Kuna Wachungaji Vijana ambao hawajaolodheshwa hapa maana nafasi isingetosha wamejitoa kikamilifu kwa ajili ya Utumishi Wa Mungu. Mungu awabariki wao na Kazi yao Pia.







Source : http://samsasali.blogspot.com

No comments:

Post a Comment