Kanisa lateketezwa kwa moto Biharamulo

 Kanisa la TAG, katika kijiji cha Nihongola Kata ya Nyakahura wilayani Biharamulo, mkoani Kagera limeteketezwa kwa moto na kusalia majivu, usiku wa manane wiki iliyopita na watu wasiojulikana, huku wachomaji wakiacha ujumbe mkali uliojaa  matusi.
 
Akiongea na chanzo cha habari hii, Mchungaji wa kanisa hilo, Samwel Baguma, alisema tukio hilo, lilitokea wakiwa wamelala, lakini walishtushwa na mwanga uliosababishwa na moto uliokuwa ukiteketeza viti na meza zilizokuwa ndani ya kanisa hilo.

Mchungaji Baguma alieleza kuwa, walipoona moto umepamba moto huku ukiwa umekwisha kuharibu kila kitu, walitoka nje na kuita watu ambao walitoka na kuzima licha ya kuwa ulishafanya uharibifu wa kutosha.
“Ilikuwa majira ya saa nane hivi, tulihisi kuna kitu kinachoungua kanisani, tulipokurupuka na kutoka nje ndipo tukaona moto mkubwa ukimalizia kuunguza jengo la kanisa na vitu kadhaa vilivyokuwemo ndani,” alisema na kuongeza: 

“Tulipiga kelele na watu walitoka kutusaidia kuuzima ingawa ulikwisha teketeza vitu karibu vyote, baada ya kumaliza kuuzima huku kukiwa kumepambazuka niliona tofali moja likiwa limeegesha karatasi nyeupe na nilipoichukua na kuiangalia nilishtushwa na ujumbe wake.”Alisema alipoisoma ilikuwa imeandika maneno ya kumtukana vikali yakiambatana na vitu vilivyoashiria ushirikina kwa kumtaka aache eneo hilo alilojenga kanisa kwa madai lina wenyewe.

 Alisema, barua hiyo amekwisha iwasilisha Polisi, huku akieleza kuwa ana vielelezo vya kutosha juu ya upatikanaji wa eneo hilo la kuabudia ambapo alibainisha kwamba aliuziwa kihalali na sheria zote zilizingatiwa.
 “Kwa sasa tunaabudia kwenye boma letu lingine, hatuna mpango wowote wa kuogopa kile kilichotendeka, siwezi kushtushwa na mambo ya kichawi kwa kuwa Yesu ni zaidi ya wachawi wote, tutaendelea kukaa hapa hadi Yesu anarudi,” alisema. 

 Aidha alilaani kitendo hicho, kwa kuwa kinarudisha nyuma maendeleo, huku akibainisha kwamba ni vema kama mtu ana jambo akaliweka mezani, watu wakalijadili kuliko kufanya uharibifu ndani ya nyumba ya Mungu.

 Akiongea na chanzo cha habari hii Askofu wa Jimbo la Kagera, Julius Bibuhinda alidhibitisha kutokea kwa tukio hilo na kulaani kitendo hicho, huku akieleza kuwa wameiachia Polisi kuwasaka wahusika.
 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, ACP Philipo Karange, akiongea na chanzo cha habari hii alidhibitisha kutokea kwa tukio hilo nyakati za usiku mnene na kuongeza kuwa, wameshawakamata watu watatu na upelelezi bado unaendelea.

“Hii ni kesi ya jinai, waliokamatwa hadi sasa ni watu watatu wakiwemo ndugu wawili, Bw. James Bugarukanyi na Fabian Bugarukanyi, waliouza kiwanja hicho kwa Mchungaji muda mrefu.Kamanda huyo alimtaja mtuhumiwa mwingine  kuwa ni Rinus Nikodemo, na watafikishwa mahakamani.

 Katika siku za hivi karibuni, kumekuwepo na matukio ya uchomwaji moto wa nyumba za kuabudia, kushambuliwa kwa watumishi na hata kumwagiwa tindikali,Hayo yanatokea, wakati zipo juhudi kubwa ambazo zimekuwa zikifanywa na viongozi wa dini kuleta suluhu baina yao.

Askofu Mkuu wa Kanisa la TAG Dk. Barnabas Mtokambali asifu Njombe kuonyesha Mfano

Askofu Mkuu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) Dk. Barnabas Mtokambali, ametoa rai kwa maaskofu nchini, kuiga mfano wa ujenzi wa chuo cha kupanda makanisa kilichopo Njombe ili kutimiza mpango mkakati wa “Miaka Kumi ya Mavuno Tanzania kwa Yesu.” Dk. Mtokambali alitoa nasaha hizo wakati wa mahafali na uzinduzi wa chuo cha kupanda makanisa kilichopo Mkoa wa Njombe, chini ya Askofu wa Jimbo hilo, Patrick Luhwago, sanjari na semina elekezi ya viongozi iliyomalizika Juni 28, 2013. Askofu huyo alinasihi watumishi kujituma na kukamilisha ujenzi wa vyuo vyao vya kupanda makanisa, vilivyomo majimboni mwao ili kupata watenda kazi wengi walioandaliwa kiufanisi katika shamba la Bwana. Akihutubia katika uzinduzi huo, Dk. Mtokambali alieleza sababu za msingi za kuanzisha vyuo hivyo vya kupanda makanisa kote nchini kuwa ni pamoja na Kanisa kuongezeka kiidadi kupitia watendakazi wengi walioandaliwa vya kutosha na vyuo hivyo.
Alitaja sababu nyingine kuwa ni Kanisa la TAG kukua kijografia, kiasi cha kufikia maeneo ambayo hayajafikiwa na injili, hivyo kulifanya kukua kwa kasi kama ilivyokuwa enzi za kanisa la Matendo ya Mitume ambalo Yesu aliliacha duniani. “Kuna ulazima mkubwa kwa kanisa letu kukua kijiografia hata kuwafikia watu ambao hawajawahi kufikiwa na injili,” alisema Dkt. Mtokambali. Alieleza sababu zingine za kuanzisha vyuo hivyo kuwa ni pamoja na kuliwezesha kanisa kukua kiufanisi na kwa ubora kama Neno la Mungu linavyoagiza. “Mshirika yeyote wa kanisa la mahali pamoja, mwenye wito wa kufanya kazi ya Mungu ni vema akapitia chuo cha kupanda makanisa na kupata cheti cha utendakazi, huku akiwa na elimu nzuri na mafunzo sahihi. Itamrahisishia kutenda kazi kiufanisi wakati wa huduma mahali popote tofauti na hapo awali,” alisema Dkt. Mtokambali na kuongeza: “Watu walikua wanaenda kutumika kabla hata ya kupata mafunzo ya utumishi na hatimaye kupata watu ambao wanaenda kinyume na misingi ya Neno la Mungu.” Kutumia vema rasilimali ya Kanisa la TAG, ni miongoni mwa sababu aliyoitaja huku akiongeza kuwa, kwakua kila kanisa la mahali pamoja hutoa asilimia 5, kila mwisho wa mwezi kwa ajili ya kutegemeza vyuo hivyo vya Biblia. Aliongeza kuwa, asilimia 75 hutoka makao makuu kwaajili yakutegemeza vyuo hivyo, na kusema TAG imewekeza kwa watumishi wake wote wanaopitia vyuo vya Biblia nchini Tanzania; huku akisisitiza kwa wale ambao wanasoma vyuo hivyo na kutoingia shambani kwaajili ya utendaji kazi, hawawatendei haki washirika wa TAG wanaojitoa kwa mali zao. Sanjali na hayo, Dkt. Mtokambali aliongeza sababu zingine kuwa ni kufanya jimbo kuwa na kituo chake kwa ajili ya shughuli za kijimbo, hapo ndipo patakua sehemu sahihi ya kufanyia mikutano, semina, makambi na mambo yote yahusianayo na jimbo kuliko kukodisha kumbi sehemu zingine. Aidha Askofu alisisitiza kuwa kuna vijiji vingi ambavyo bado havijafikiwa na injili, huku kanisa la Bwana likiwa limeridhika kwa kazi za pale kanisani tu, bila kupeleka injili mahali ambapo bado hapajafikiwa ambapo alihoji: “Kwanini vinywaji vya soda kama vile cocacola, pepsi na vinginevyo vimefika?. Hata vyama vya siasa huko ambapo injili bado haijafika vyenyewe tayari vimeshafika, kwanini kanisa tumelala na kutokuthamini kusudi la Mungu alilotuokoa kwalo?” alihoji kwa uchungu na kuongeza: “Kama vinywaji vimefika pamoja na vyama vya siasa, basi Yesu wetu ni zaidi ya hivyo vyote, jina lake lastahili pekee kusikika Tanzania yote.” Kwa upande wa mgeni kutoka nchini Marekani, Mch. David Willington aliwaasa watumishi kutokukata tamaa, kuvunjika moyo, kujikinai kwa yale wanayopitia na badala yake watambue kuwa katika changamoto zote wanazozipitia bado Mungu yu pamoja nao, na kuwa vita vya huduma zao si wao watakaopigana bali Mungu aliyewaita.

Kwaya ya Shalom yapeleka Albam sokoni

Kwaya ya Shalom ya Kanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania, (EAGT) Magomeni, linaloongozwa na Mchungaji Imani Mwakyoma, siku chache zimepita imezindua albam yake  ya nyimbo za injili yenye nyimbo nane iitwayo USILIELIE ambayo sasa iko sokoni ikipeleka habari njema za Injili hata kwa wale wasiofika kanisani wala kuhudhuria mikutano ya Injili.

Uzinduzi huo ulifanyika kwenye ukumbi wa CCM Mkwajuni, Kinondoni Dar es Salaam, ambapo watu wengi walijitokeza kushuhudia tukio hilo, uliosindikizwa na Kwaya mbalimbali wakiwemo waimbaji binafsi wa nyimbo za injili.

Mgeni rasmi katika uzinduzi huo, alikuwa Mkurugenzi wa Shirika la wakimbizi Tanzania, Bi. Judith Mtawali ambaye aliwakilishwa na Bw. Fredrick Mwakalukwa kutoka ofisi za wakimbizi Kigoma.Bw. Mwakalukwa akiongea kwenye uzinduzi huo, aliipongeza Kwaya ya Shalom kwa juhudi kubwa ya kuandaa albamu nzuri na iliyojaa nyimbo zenye upako na zenye kuleta mabadiliko makubwa katika jamii.

Akisoma risala maalum mbele ya mgeni rasmi, iliyoandaliwa na Kwaya ya Shalom, mmoja wa wanakwaya hao, alisema hitaji lao kubwa kwa sasa ni vyombo vya injili pamoja na basi ndogo (costar) ambalo litasaidia kufanya huduma na kusafiri kwa urahisi kwenda kuhubiri Neno la Mungu ndani na nje ya Tanzania.

Mbali na hilo alisema kuwa, wanamshukuru Mungu kwa kuwawezesha kufika hapo walipofikia kwa kuwa, baadhi ya wanakwaya hawana ajira na ndiyo sababu inayowafanya washindwe kufanya maendeleo ya Kwaya kwa kasi kubwa,  aliongeza kwamba gharama za ununuzi wa vyombo hivyo vya injili pamoja na basi ndogo vitagharimu Tsh. milioni 49.

Aidha kwa upande wake mwakilishi wa mgeni rasmi, Bw. Mwakalukwa aliwataka wanakwaya kuongeza juhudi ya kumtafuta Mungu na kufanya kazi kwa bidii, kwani hawana haja ya kuajiriwa sehemu nyingine, kama watafanya bidii katika miradi yao ya Kwaya.

“Miradi ya Kwaya inaweza kumlipa kila mtu mshahara wake kila mwezi, endapo mtafanya bidii, tena mkifanya kwa bidii wala hatakuwepo miongoni mwenu ambaye hatakuwa na maendeleo katika familia yake na mtafanya kazi ya Mungu kwa bidii,” alisema na kuongeza:

“Watu watastaajabu ukuu wa Mungu juu ya maisha yenu ya mwilini na rohoni.”
Bwana Mwakalukwa alimshukuru Mungu kwa ajili ya Kwaya hiyo na kumuomba Mungu aendelee kuwatumia wanakwaya hao katika maisha yao yote.

Wakionekana kujawa na furaha, Mchungaji wa Kanisa la EAGT Magomeni, Mwakyoma, pamoja na mkewe Salome Mwakyoma, walisema wanamshukuru Mungu kwa huduma aliyoweka ndani yao, pia kwa ajili ya kwaya ya Shalom ambayo wameweza kuizindua albamu yao ya kwanza ya nyimbo za injili.
“Mungu awafanikishe mipango yenu yote, pia awape umoja miongoni mwenu, pia namshukuru mgeni rasmi kwa kuhudhuria uzinduzi huu, sitalisahau kutambua uwepo wenu watu wote mliohudhuria uzinduzi huu na nawaombea baraka kwa Mungu,” alisema

Katika Mpya imependekezwa kuwa na kipengele chenye kuzitambua siku za ibada.


Mapendekezo hayo yalitolewa na wajumbe wa mabaraza ya kata wa Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe Vijijini wakati wa kikao kilichofanyika kwa siku tatu cha kuchambua na kujadili rasimu ya katiba iliyotolewa na Tume ya mabadiliko ya katiba.
Maoni hayo, kutoka Kijiji cha Kwagunda Wilayani hapa, alisema kwa kuwa ibara ya 31 katika eneo la Uhuru wa Imani ya Dini inasema kila mtu anao uhuru wa mawazo, imani na uchaguzi katika mambo ya ya imani ya dini, imani yake au kutokuwa na imani na dini.
Kipengele kisemacho kazi ya kutangaza dini, kufanya ibada na kueneza dini itakuwa ni huru na jambo la hiari kwa mtu binafsi ili mradi asivunje sheria za nchi ni wazi kuwa mfanyakazi ambaye ni muumini wa dini ya flani atakapoamua kuondoka kazini siku ya Ibada kwenda kanisani au msikitini atakuwa anavunja sheria.

“Kwa hiyo ili kumuondoa katika hofu hiyo ni vyema katiba iwe na kifungu chenye kueleza juu ya kutambua siku za ibada na ziwe tatu badala ya mbili kama ilivyo kwa sasa,” alisema mzungumzaji.
Mjumbe huyo alipendekeza katiba mpya iwe na kipengele chenye kutamka siku za ibada kwamba ni tatu ambazo iwe Ijumaa, Jumamosi na Jumapili ili waumini wa Dini ya Kikiristo,Kiislamu nao wakitoka nyumba za Ibada  wasiwe ni wenye kuvunja sheria za nchi.
Wajumbe wa Tume ya mabadiliko ya katiba waliopo mkoani Tanga ni Ussi.Khamisi Haji na Riziki Shahri Mngwali ambao wameanza kupokea maoni katika Wilaya ya Korogwe na leo Jumatatu watakuwa Wilayani Muheza.
Kabla ya maoni hayo ya wajumbe wa mabaraza ya katiba, Watanzania, wamekuwa wakishiriki ibada mbalimbali katika siku za Jumapili kwa baadhi ya madhehebu ya dini, za Kikristo,  huku madhehebu mengine ya dini hiyo, yakifanya ibada zao siku ya Jumamosi na Waislamu wamekuwa wakifanya ibada za Ijumaa.
Kama pendekezo hilo litakubaliwa na baadaye kuingizwa kwenye Katiba, siku hizo za ibada zitakuwa zimetambuliwa na katiba hivyo kuzifanya ziwe za mapumziko tofauti na sasa ambapo hakuna sheria yeyote inayozitambua siku hizo kama za mapumziko.

Afisa wa Zimbabwe afariki ziara ya Obama Maaskofu, wachungaji jijini Dar wamlilia

Afisa wa Serikali ya Zimbabwe, Bw. Amos Mushanyinga, aliyetua nchini kushuhudia ziara ya rais wa Marekani, Barack Obama kwa mwaliko maalum na serikali ya Tanzania, amefariki baada ya kuugua ghafla na kukimbizwa katika Hospital ya Aghakhan ambapo madaktari walijitahidi kuokoa maisha yake bila mafanikio.

Afisa huyu aliyefariki Julai pili mwaka huu, aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali nchini humo, na alikuja nchini Tanzania akiwa na wazimbabwe kadhaa kushiriki ujio wa Rais Obama.

Akizungumza na chanzo cha habari hii, Askofu Mkuu msaafu wa Kanisa la TAG, Dk. Ranwell Mwenisongole, ambaye ni Mchungaji Kiongozi wa kanisa la Upanga, City Christian Centre (CCC), lililotumika kumuaga afisa huyo alisema kuwa marehemu alifikwa na mauti Jumanne iliyopita jijini Dar es Salaam.
Askofu Mkuu msaafu wa Kanisa la TAG, Dk. Ranwell Mwenisongole, ambaye ni Mchungaji Kiongozi wa kanisa la Upanga, City Christian Centre (CCC)
Aliongeza kuwa, marehemu Mushanyinga aliwasili nchini Tanzania akitokea nchini Zimbabwe, akiwa mzima kwa lengo la kushiriki mkutano wa Rais Obama na wafanyabiashara, katika ziara yake nchini Tanzania.

Mchungaji huyo aliongeza kuwa, hali ya   Mushanyinga ilibadilika ghafla hivyo kukimbizwa katika hospitali ya Aghakhani ya jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya matibabu, ambapo ili bainika kuwa alikuwa akisumbuliwa na tatizo la inni.

Mbali na hilo alisema, jitihada za madaktari hospitalini hapo, hazikuzaa matunda ambapo mauti ilimfika wakati akihudumiwa.

Dk. Mwenisongole alisema, ni jambo la kusikitisha kuona marehemu alifika nchini akiwa mzima lakini akarudi akiwa katika sanduku,  akawataka watanzania na Wakristo kwa ujumla, kukaa vizuri kwa Mungu na kuacha michanganyo kwani wakati wowote historia inaweza kufungwa.

Mtumishi huyo wa Mungu, Dk. Mwenisongole aliendelea kubainisha kuwa, kifo cha Mushanyinga kinapaswa kuwa fundisho kwa watu wote, kwa kile alichosema kwamba hakuna ajuae lini Bwana atahitaji roho yake, hivyo kuwa tayari wakati wowote, ili kuwa na maishi milele mbinguni.

Naye Mkurugenzi wa Idara ya Uanafunzi na Maandiko ya kanisa hilo, Mchungaji Elingarami Munisi, ambaye alikuwa rafiki wa marehemu wakati wa uhai wake, akizungumza alisema kuwa amesikitiswa na kifo cha mheshimiwa huyo.

Mbali na hilo, aliwataka watanzania kudumisha upendo na mshikamano, huku akiwashukuru kwa kujitokeza kumuaga na kumsindikiza marehemu kusafirishwa kwenda nchini Zimbabwe kwaajili ya kuupumzisha mwili wake.

Sambamba na hilo, aliwasihi wakristo kuzidi kumpenda Mungu na kumtumikia, ikiwa ni pamoja na kuiandaa mioyo yao kwa habari ya maisha yao.

Ibada hiyo maalumu ilihudhuriwa na Balozi wa Zimbabwe nchini Tanzania, ambapo alisema Marehemu alikuwa kiongozi bora nchini Zimbabwe katika masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na uchumi.

Habari zingine zinasema kuwa Afisa huyo alizungumza na Mchungaji Munisi siku mbili kabla ya kufariki dunia na aliahidi kuwa angeenda kuonana naye katika kanisa la TAG Kawe, Faith and Miracle Centre jumapili iliyopita, lakini hakupata nafasi hiyo baada ya kuugua.

Siku chache zilizopita Mchungaji Munisi alienda Zimbabwe kufundisha katika semina maalumu iliyoandaliwa na kansia ambalo marehemu alikuwa akisali na walipata nafasi ya kuzungumza na akamhudumia kiroho, mtumishi huyo wa umma ambaye pamoja na mambo mengine alikuwa mchumi.

Askofu KKKT atahadharisha uanzishwaji vikundi vya ulinzi

Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Dodoma, Amon Kinyunyu, amesema kitendo cha viongozi wa vyama vya siasa ya kuamua kujianzishia vikundi vya ulinzi wa kujilinda kwenye vyama vyao, ni ishara tosha ya kuhatarisha amani ya Taifa.

Askofu Kinyunyu amesema viongozi wa siasa wanaoanzisha vikundi vya namna hiyo ni kuashiria jinsi gani walivyokosa heshima kwa Mungu na kwa mamlaka ya serikali ambayo ina ulinzi na usalama unaolinda nchi kwa ujumla.
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Dodoma, Amon Kinyunyu.
Alitoa kauli hiyo wakati wa hafla ya uzinduzi wa miradi ya mifumo ya miundombinu ya watoto ikiwamo ya maji, madarasa na vyoo vya kisasa iliyodhaminiwa na shirika la Compassion International Tanzania kwa kushirikiana na washirika wenza kutoka kwenye Makanisa ya Huduma ya Mtoto iliyofanyika katika viwanja vya Kanisa la Tag Miyuji mjini hapa.

Askofu Kinyunyu alisema kitendo cha vyama hivyo kuanzisha vikundi vya kujilinda, ni ishara ya kuleta machafuko ya amani ya nchi.

Pia alisema kitendo hicho kitawafanya vijana waliopo katika vyama hivyo kuendelea kuchukiana badala ya kupendana.

Alisema viongozi wa kisiasa hawana budi kutambua kuwa kwa kuanzisha vikundi hivyo ni kuzidi kujenga uhasama mkubwa utakaoiumiza jamii isiyohusika wakiwamo watoto, wanawake, wazee na walemavu.

“Hapa wanatakiwa kujua kuwa kitendo hicho ni ishara tosha inayoashiria kuanzisha vita ambayo washirika wakubwa ni vijana tunaowategemea kushika madaraka mbalimbali ya kiserikali na ya kisiasa,” alisema.

Askofu Kinyunyu amewataka viongozi wa vyama vya siasa kuheshimu amani iliyopo iliyobarikiwa na Mungu tangu kuumbwa kwa ulimwengu.

Kwa upande wake,  Mkurugenzi wa Compassion Intenrational Tanzania (CIT) hapa nchini, Mchungaji Joseph Mayala, alisema kitendo hicho ni sasa na uwekezaji kwa vijana wawe na roho ya ukatili badala ya upendo na amani.

Source:Nipashe

Dk Malasusa: Nchi haitakuwa na amani kwa kuongeza idadi ya Polisi

Kiongozi Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT ), Askofu Dk.Alex Malasusa amesema nchi haitakuwa na amani kwa kuongeza idadi ya polisi bali amani itapatikana kutokana na Watanzania kuheshimiana.

Askofu Malasusa aliyasema hayo jana alipokuwa akiweka jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Faragha na maombi katika Kijiji cha Chasimba wilayani Bagamoyo kitakachojengwa kwa ushirikiano wa Usharika wa Dayosisi ya Kariakoo.
 Askofu Dk.Alex Malasusa

“Nchi haiwezi kuwa na amani kwa kuongeza idadi ya polisi njia pekee ni kuheshimiana na kuheshimu madhehebu mengine ili kuendeleza amani,” alisema Dk.Malasusa.

Aidha, alisema kituo hicho kitajengwa kumbi za kisasa za mikutano, zahanati, chuo cha ufundi, maktaba na nyumba ya faragha kwa ajili ya maombi na viwanja mbalimbali vya michezo.

Katika ibada hiyo mgeni rasmi alikuwa ni Makamu wa Rais Dk.Gharib Bilal, lakini aliwakilishwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa rais Mazingira Dk.Theresia Huvisa.

Akizungumza kwa niaba ya Makamu wa Rais Dk.Huvisa alisema serikali itashirikiana na taasisi mbalimbali zikiwamo za kidini kusaidia kuendeleza maendeleo.

Ofisi yake ilichangia Shilingi milioni mbili katika harambee iliyofanyika kwa lengo la kupata milioni 200 kuendeleza ujenzi huo.

Katika harambee hiyo iliyoshirikisha viongozi mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi Mchungaji Daniel Thabita kutoka Botswana alichangia Sh.milioni 1.5.

Source:Nipashe

Tanzania Gospel Singers Breakfast - Episode IV


Wanawake Watumishi wa Kikristo (WWW) Mbalizi watoa Pikipiki kwa Waangalizi

Wanawake Watumishi wa Kristo (WWK), Sehemu ya Mbalizi, wiki iliyopita ilitoa zawadi ya usafiri wa pikipiki kwa viongozi waangalizi wa sehemu hiyo, ili kuiwezesha kazi ya Mungu kusonga mbele zaidi pasipo kukwama kwa namna yoyote ile.

Akizungumza wakati wa tukio hilo, katika kongamano la siku mbili la WWK Sehemu ya Mbalizi, Mkurugenzi wa wanawake hao, Sevelina Mwasile alisema kuwa, wao kama wanawake wa kanisa la TAG wameona watoe vyombo hivyo vya usafuri ili kuondoa usumbufu kufika wasikoweza kirahisi.

Aidha Bi. Sevelina alisema, viongozi hao wamekuwa wakitumia baiskeli kwa muda mrefu na wakati mwingine walikuwa wakitembea kwa mguu kwenda kuifanya kazi ya Mungu mbali, jammbo ambalo limekwamisha kazi ya Mungu kwa kiwango kikubwa.

Mkurugenzi huyo alisema kuwa, miongoni mwa zawadi walizojadili, walifikia muafaka wa kununua Pikipiki tatu ili kila kiongozi apate usafiri wake kuliko kununua gari moja ambayo kila mmoja atakuwa akiitegemea.

Kiongozi huyo wa wanawake, aliwataja viongozi waliopewa zawadi hizo kuwa ni pamoja na ; Watson Mwanjoka, ambaye ni Mwangalizi wa Sehemu ya Mbalizi, Eliya Mukuku, Makamu Mwangalizi na Furahisha Ngofyela, katibu Mbalizi.

Akishukuru kwa tukio lililofanywa na wanawake hao, Mwangalizi Mwanjoka alisema ameshangazwa na kitendo kilichofanywa na wanawake hao kwani hakutengemea kupata usafiri.

Mwangalizi huyo alisema kuwa, wanawake hao wamekatisha kilio chake cha muda mrefu, huku akiweka wazi kuwa, kazi ya Mungu inahitaji uharaka ili kuiendeleza.

Naye Makamu Mwangalizi wa Sehemu hiyo, Mchungaji Eliya Bukuku, alisema wametembea kwa baiskel kwa muda mrefu hata kufika hatua ya kuchoka, lakini Mungu amejifunua kwa kuwahurumia kupitia wanawake hao.

Alitoa wito kwa Wakristo kuwaombea kwa bidii wanawake ili Mungu ayatumia maono waliyo nayo katika kazi yake.

Mbali na kutoa zawadi kwa Viongozi wao, WWK Sehemu ya Mbalizi walichangisha zaidi ya milioni nne kujenga vibanda vya kufanyia biashara, ili kutunisha mfuko ndani ya mji huo mdogo wa Mbalizi.

Akizungumzia tukio hilo, Mkurugenzi wa WWK Mbalizi, Bi. Mwasile alisema, kujengwa kwa vibanda hivyo, vya biashara vitasaidia kuongeza pesa na michango ya akina mama itapungua kwani mara baada ya vibanda hivyo kukamilika vitapangishwa na kodi zitakazo lipwa zitaingizwa moja kwa moja kwenye mfuko wa akina mama.

Alisema maono yao ni kupata milioni 50 kwaajili ya ujenzi na vibanda hivyo, ili kukamilisha ujenzi katikati mji huo wa Mbalizi unaosifika kibiashara mkoani Mbeya.

Mtangazaji wa Radio Wapo Mission avamiwa, Kuporwa na Kukatwa Kisu Kooni

 
 
Katika hali ambayo inaashiria kwamba usalama wa watu na mali zao katika uwanja wa taifa hususan siku za matamasha hautoshi, mtangazaji na fundi mitambo wa WAPO Radio FM, Filemon Rupia, maarufu kama Father Filemon Rupia, amevamiwa usiku wa tamasha la matumaini na watu wasiojulikana, ambapo walimpora vitu kadhaa ikiwemo simu zake, pesa na kisha kumkata na kitu kinachosadikiwa kuwa ni kisu kwenye koo lake.
Tukio hilo linasemekeana kutokea majira ya saa mbili usiku, ambapo Filemon Rupia na wafanyakazi wenzake wakitokea kwenye ibada ya ujazo wa Roho Mtakatifu maeneo ya Mbezi Beach inayofahamika kama Oparesheni Takasika, walifika maeneo ya uwanja wa taifa, ambapo Father Rupia aliamua kurejea nyumbani kutokana na uchovu, ambapo wenzake walimuacha kwenye lango la kuingia uwanjani - ambapo alianza kutafuta usafiri wa kurudi nyumbani kwake.
Laiti kama angejua kilicho mbele yake, hakika angeingia na wenzake uwanjani, lakini mwanadamu ni mwanadamu tu. Kilichotokea wakati akitafuta usafiri ndio hiki tunachozungumza sasa, kuvamiwa, kuporwa, na kukatwa na kisu kwenye koo lake, ambapo haijajulikana lengo hasa la wavamizi hao kufanya hivyo ilikuwa ni nini.
Hata hivyo Mungu ashukuriwe, kwani kwa hivi sasa Filemon Rupia anaendelea vizuri baada ya kupatiwa huduma kwenye hospitali ya Kairuki, amapo alishonwa nyuzi kadhaa kwa ndani na nje ya koo. Tutakufikishia taarifa zaidi pindi ambapo tutazipokea kutoka kwenye vyanzo vyetu. Kwa hivi sasa anahitaji maombi yako kuvuka hali aliyonayo.

Maelezo ya Rupia
Hatimaye baada ya kufanya mawasiliano na Rupia, anaeleza kuwa akiwa anataka kuchukua bodaboda eneo la uwanja wa taifa, ndipo hapo dhahama lilitokea.

Bodaboda mbili zilikataa kwa maelezo kuwa kuna mtu anasubiriwa, bodaboda ya tatu ikadai kuwa haiwezi kwenda mbali. Ndipo hapo akalazimika kusogelea bodaboda za mbele zaidi ili apelekwe nyumbani, kilichofatia hao ni roba ya mbao, na kuvamiwa na vijana kadhaa ambapo katika purukushani, walitoa kisu na kuanza kumkata kooni, ambapo kisu kilikata ubao na kumchana eneo la kidevu na shingo. Na kama sio ubao kuwepo katikati, basi yangekuwa mengine kwa hivi sasa.
Mara baada ya ya hapo, ikafuata kuzirai kwa dakika kadhaa, na alipozinduka, ndio akasogea hadi getini kuomba msaada, ambapo walikwenda hadi kituo cha Polisi kabla ya kuelekea hospitali ya Temeke (ambapo huduma zilikuwa hafifu) na baadae kurudi nyumbani kwa ajili ya kwenda hospitali ya Kairuki.
Wakati haya yote yanatokea, alikuwa akizungumza na mfanyakazi mwenzake, Joyce Mathew, ambaye baada kufuatilia tukio lote kupitia simu kuanzia wanamkaba na hadi kuiba mali zake, aliwasiliana na wakubwa zake, ambapo msaada ulifanikiwa kupatikana kwa wepesi zaidi.
Pamoja na yote haya, hapa ndipo tunakumbushwa kuwa kila mara jua likizama na tukalala na kuamka salama, basi sifa na utukufu tukumbuke kumrejeshea Yesu Kristo anayetawala muda wote.
 
source:gospelkitaa

Jeans & Tshirt yaliyojili Katika Picha siku ya Jana.

Jeans & Tshirt ni Event ya Gospel yenye madhumuni ya kuwakutanisha vijana waliookoka na wasiookoka kwa lengo la kujumuika katika kile kinachoendelea katika event hiyo.Event hiyo huwa inafanyika kila Jumapili ya kwanza ya mwezi ikiwa ni kitu cha wendelezo,Wakati kindi hiki ikiwa na dhima inayosema Christ In Action (CIA )

Siku ya jana ilifanyika Makumbusho ya Taifa mkabara na Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) ambapo kulikuwa na vitu mbalimbali vilivyofanyika kama Dance R.I.O.T Dancers,Drama,Poetry,Bupeh alikuwepo na wengine wengi.

Mmeba maono Pastor Isaac Mallonga akizungumza jana katika Event hiyo alisema Jeans & Tshirt ni Event kwa lengo la Kuwaleta vijana kwa Yesu,siku ya Jana Vijana Kadhaa walipata kumpa Bwana Yesu maisha yao na wengine uhusiano wao na Mungu kurejea.

Imeonekana kuwa Event hiyio imekuwa msaada sana kwa vijana wa mjini maana Jeans & Tshirt event iliudhuliwa na vijana wengi na kupata muda wa Kuimba na Kucheza katika uwepo wa Mungu

Mwezi ujao Jeans & Tshirt Event itafanyika palepale Makumbusho ya Taifa mkabara na Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) 




















Yaliyojii Tamasha la Usiku wa Matumaini Uwanja wa Taifa.


Raisi Kikwete akifungua Tamasha hilo
Ambwene Mwasongwe akiwa na Mwasabwite
Enock Jonas akiwa fanya vitu vyake
Mama Mchungaji Martha Mwaipaja
Jesca Honore wa Magupa alikuwepo kuhudumu katika Tamasha hilo
Flora Mbasha na Mme wake wakiingia kufanya vitu vyao
Sara K alikuwepo kutoka Kenya akiwakilisha

Raisi JK akiwa tayari kupuliza kipenga kuashilia kuanza kwa mechi kati ya wabunge wa Simba na Yanga
Waziri wa Vijana,Habari Utamaduni na Michezo akiwa jirani na Mh.JK
Erick Shigongo mmoja wa waandaaji wa Tamasha la Usiku wa Matumaini.
Waziri wa Vijana,Habari Utamaduni na Michezo Dr. Fenella Mukangara akizungumza
Wabunge wa Simba
Wabunge wa Yanga