Jeshi la Polisi lakamata vitu vilivyoibiwa Kanisa la KKT Mbagala.

Jeshi la Polisi  Mkoa wa Temeke limefanikiwa kukamata watuhumiwa wanne wanaohusishwa na kufanya vurugu katika kituo cha Polisi Mbagala wakiwa na baadhi ya vitu vilivyoibiwa kufutiwa uvamizi wa makanisa katika eneo la Mbagala Wilaya ya Temeke, Jijini Dar es Salaam.

 Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) David Misime aliwataja watuhumiwa hao ni Kambi Hajidi, Hamadi Salehe, Shabani Hamisi na Majebele Elias wote ni wakazi wa Mbagala na Mtoni Mtongani.

 Kamanda Misime alivitaja vitu hivyo ni komputa moja, keybodi pamoja meza moja ndogo, vitu hivyo vyote vimetambuliwa kuwa ni mali ya Kanisa la Kkkt Mbagala, Jijini Dar es Salaam.
 Aliongeza kuwa watuhumiwa hao wote watafikishwa mahakamani baada ya taratibu za Upelelezi kukamilika ili sheria iweze kuchukuwa mkondo wake.

Mbali na mambo mengine amewataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa zitakazowezesha kupatikana kwa vitu vyote vilivyoibiwa pia kutokubali kununua vitu vitu kiholera.

No comments:

Post a Comment