Akizungumza na waumini wa kanisa hilo Dayosisi ya Mount Kilimanjaro,wakati wa ibada ya shukrani baada ya kumalizika kwa mgogoro uliokuwa unaikumba kanisa hilo, Dk. Mokiwa alisema imeibuka tabia kwa baadhi ya viongozi wa kanisa kuogopa kuwakemea watu wenye uwezo mkubwa kifedha hata kama wanakiuka sheria za kanisa.
Aidha, kiongozi huyo pia amewataka watendaji wa kanisa hilo kutokubali kupokea fedha za muumini yeyote zitakazobainika kuwa hazikupatikana kihalali.
Dk.Valentine Mokiwa |
“Itakuwa dhambi kubwa kwa viongozi wa madhehebu ya dini kuwatetemekea na kuwaweka mbele watu wenye fedha na kushindwa kuwakemea pale wanapokwenda kinyume na kufanya hivyo ni kwenda kinyume na maelekezo ya kanisa na maelekezo ya Mungu.”
Askofu Mokiwa pia amewaonya waumini wanaodhani kuwa kwa kutumia fedha zao watapata nafasi ya kuyavuruga madhehebu ya dini na kuwataka viongozi wa madhehebu ya dini kuwa macho na makundi ya watu wa aina hiyo ambayo amedai yamekuwa yakiongezeka siku hadi siku.
Akizungumza katika ibada hiyo, Askofu wa Dayosisi ya Mlima Kilimanjaro Stanele Hotay, pamoja na kuwashukuru waumini wa kanisa hilo kwa mshikamano walioonyesha wakati wote wa mgogoro, aliwawataka kuendeleza msimamo huo.
Aidha, Askofu huyo ameiomba serikali kuendelea kushirikiana kwa karibu na viongozi wa madhehebu ya dini katika nyanja mbalimbali zikiwemo za kiuchumi na kukabiliana na umaskini unaoendelea kuikabili jamii.
Wakiwasilisha salam za serikali, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Rehema Nchimbi, walisema serikali itaendelea kushirikiana na viongozi wa madhehebu ya dini na kuhakikisha kuwa uhuru wa kuabudu unadumishwa kwa mwananchi wote.
Dk. Nchimbi amewataka waumini wa madhehebu ya dini wanaopambana na viongozi wao kuacha mara moja utaratibu huo kwani licha ya kuwa hauna tija utawasababishia kupata laana toka kwa Mungu.
No comments:
Post a Comment