Rais Kikwete alipotembelea Makanisa yaliyoharibiwa katika vurugu za waisalam Mbagala,Atoa pole kwa waumini na kusema sheria lazima ifuate mkondo wake kwa wote waliohusika.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete alipotembelea kuangalia uharibifu mkubwa ulikiofanywa katika makanisa mbalimbali na mali huko Mbagala jijini Dar es salaam wakati wa vurugu za Waislamu Ijumaa iliyopita kufuatia habari kuwa kuna mtoto amekojolea Msahafu,
Makanisa kama la TAG na KKKT na la Wasabato ni miongoni mwa makanisa yaliyofanyiwa uharibifu huo.Pia atoa pole kwa waathilika na kusema lazima sheria ifuate mkondo wake kwa wote walio husika katika vurugu hizo.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akishuhudia uharibifu ndani ya kanisa akiwa ameongozana na viongozi wa serikali na pia viongozi wa Dini walioathirika na vurugu hizo katika makanisa yao huko  Mbagala jijini Dar es salaam wakati wa vurugu za Waislamu Ijumaa iliyopita.
 Mchungaji Alkwin Mbawi akimwonesha Rais Jakaya Mrisho Kikwete uharibifu mkubwa uliofanywa wa uvunjaji wa viti,meza na vitu vingine kanisanai hapo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akioneshwa na Mchungaji  uharibifu mkubwa uliofanywa kwenye magari yaliyokuwa yameegeshwa ndani ya kanisa Mbagala jijini Dar es salaam wakati wa vurugu za Waislamu Ijumaa iliyopita kufuatia habari kuwa kuna mtoto amekojolea Msahafu.





No comments:

Post a Comment