TAMASHA kubwa la kwanza la kusifu na kuabudu kwa mwaka 2014 Lafana .
TAMASHA kubwa la kwanza la kusifu na kuabudu kwa mwaka 2014 Lafana .Tamasha hilo ambalo hufanyika kila jumapili ya mwisho mwezi lilifanyika jumapili iliyopita (26.01.2014) pale Dar es Salaam Pentecoste Church ( DPC) .
Lilijumuisha wasanii kadhaa wa nyimbo za injili akiwemo John Lisu na kwaya ya rivers of life ya DPC .
Pata habari zaidi kwa njia ya picha .
Imetayarishwa na Erasmus Augustine.
Lilijumuisha wasanii kadhaa wa nyimbo za injili akiwemo John Lisu na kwaya ya rivers of life ya DPC .
Pata habari zaidi kwa njia ya picha .
Mc Boniface & Joyce M wa DPC :
Picha kwa hisani ya DPC na Worshipers family Tanzania
Sehemu ya kwaya ya Rivers of life wakiwa jukwaani .
Picha kwa hisani ya DPC na Worshipers family Tanzania
Picha kwa hisani ya DPC na Worshipers family Tanzania
Picha kwa hisani ya DPC na Worshipers family Tanzania
Picha kwa hisani ya DPC na Worshipers family Tanzania
Askofu Polycarp Kardinali Pengo anahitaji maombi yako.
Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo |
Taarifa ya kuugua kwa Kardinali Pengo, kiongozi wa kiroho anayeaminika kwa kukosoa uovu unaofanywa kwenye jamii, imetangazwa na Askofu Msaidizi wa kanisa hilo jimboni humo, Mhashamu Titus Mdoe.
Mdoe, alitoa taarifa hiyo wakati wa misa takatifu iliyofanyika jana kwenye kigango cha Nzasa, parokia ya Temboni jimboni humo.
Misa hiyo ilikuwa mahususi kwa ajili ya ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi na huduma za kiroho kwa kigango hicho kinachotarajiwa kupandishwa hadi ili kiwe parokia.
Mhashamu Mdoe hakutaja ugonjwa unamsumbua Kardinali Pengo, lakini aliwataka Wakatoliki na watu wenye mapenzi mema, kuendelea kumuombea ili apate nafuu.
Alisema ugonjwa wa Kardinali Pengo unaweza kuchangiwa pia na hali ya kuelekea katika uzee, ingawa sababu hiyo haijafikia kuwa chanzo kikuu cha kumfanya augue.Katika hatua nyingine, Askofu Mdoe alisema utumishi wa umma ulio bora unapaswa kuelekezwa katika kutatua umasikini na kero zinazoikabili jamii, hivyo kufikia tarajio la kuwa maisha bora.
Pia alikosoa tabia ya baadhi ya viongozi hususani watawala, kupiga picha zenye mwelekeo wa kushiriki na kutatua kero za jamii, huku lengo likiwa ni kupata nafasi kwenye vyombo vya habari.
Alisema miaka 52 ya Uhuru ilitosha kwa kutatua umasikini na kero nyingine zinazoikabili nchi.
Badala yake, alisema walio katika dhamana ya kufanikisha azma hiyo, wameshindwa kufikisha tumaini la maendeleo kwa wananchi hasa wa vijijini, licha ya ukweli kwamba maendeleo mijini yanakua kwa kasi.
Mhashamu Mdoe, alisema watu kama maafisa kilimo ambao damu zao zipo kwa kuwatumikia watu, hawapaswi kukaa maofisini wakiwa wamevaa suti, bali kuhakikisha wantekeleza wajibu wa kuwahudumia wakulima.
Alisema kuna maeneo mengi ya nchi yasiyofikiwa na mahitaji muhimu kwa jamii kama umeme, maji, afya na elimu bora, hivyo kuwafanya wasinufaike na matunda yanayotokana na Uhuru na rasilimali za nchi.
\
CHANZO: NIPASHE
Mwalimimu Lilian Ndegi akamia Kuukomboa Uzao wa Mwanamke
Mwalimimu Lilian Ndegi
Wito umetolewa kwa Wanawake Wajawazito,Wakina Mama walio katika Malezi pamoja na Mabinti kusoma kitabu cha MUNGU NA UZAO WANGU kilichoandikwa na MWL. LILIAN NDEGI wa Kanisa la Living Water Centre chini MTUME ONESMO NDEGI lililopo Kawe jijini Dar-es-salaam nchini Tanzania.
Akitoa wito huo katika uzinduzi wa kitabu hicho hivi karibuni, Mwalimu huyo wa Neno la Mungu Lilian Ndegi amesema kuwa, kitabu hicho ni msaada mkubwa kwa wakinamama wajawazito kwani watapata maarifa ya Ki-Mungu yatakayowasaidia kuwaondoa katika uharibifu wa mimba tangu inapotungwa,inapolelewa,pamoja na wakati wa kujifungua mtoto na kwamba hiyo inawahusu pia na mabinti ili kuwasaidia kuwa na uzazi mwema hapo baadae. Akifafanua zaidi amesema Serikali ya Tanzania imeweka utaratibu mzuri wa kujenga vituo vya Afya kuwasaidia wakina mama wajawazito, Mila na Desturi nazo zina kanuni zao, lakini wakati umefika kwa Kanisa kujihoji Mungu anasema nini juu ya uzao wa Mwenye Haki na kwamba litembee katika Kanuni zipi ili kuweza kupata ushindi mkubwa katika Uzazi. Aidha amesema kitabu hicho kimebeba Ujumbe Wa Mungu wenye kusudi maalum juu ya maisha ya kiroho na kimwili, utakaofungua ufahamu wa watu na kuliona Pendo Kuu la Mungu juu ya maisha yao na Uzao wao maana Mungu anaanza kushughulika na uzao wa Mweye haki kizazi hata kizazi. Mwl. Lilian Ndegi ameongeza kuwa kama ambavyo ilikuwa kwa Ibrahim kupitia kitabu hicho cha MUNGU NA UZAO WANGU,Wazazi na Walezi kwa ujumla watajifunza mambo muhimu ambayo Mungu anawaagiza kufanya, kama sehemu ya wajibu wao kwa mfano; Mume kumtunza mkewe siku zote ,kuwalea na kuwatunza watoto pamoja na kuziona athari za kinywa katika ulimwengu wa roho zinavyoweza kuathiri maisha ya uzao wao kutokana na kuwanenea maneno au kuwapa majina yasiyofaa kama vile kumwita Mtoto Mateso na nk. Kwa upande wake Mgeni Rasmi ambae ni Mkuu wa Makanisa ya Living Water Center nchini Tanzania Mtume Onesmo Ndegi Mume wa Lilian Ndegi,amewaasa Wanaume kuwa chachu ya mabadiliko katika ndoa zao, badala ya kujifanya wana misimamo isiyobadilika, na kuwataka kubadilika wao kwanza katika mitazamo yao juu ya wake zao na ndipo itakapo kuwa chachu za wake zao kubadilika kitabia na mienendo katika ndoa. Aidha ametoa wito kwa vijana wa kiume kuwa na Mungu zaidi katika ujana wao ili kumpata Mke Mwema atokae kwa Bwana atakaeweza kuwa msaidizi wa kweli katika maisha kiroho na kimwili huku akimshukuru Mungu kwa ajili ya Mke wake Lilian alie mtaja kuwa wa Maana Sana katika maisha yake na kwamba amefanyika baraka na msaada tosha katika Huduma yake na Familia kwa ujumla. Hata hivyo amewataka wanaume wote kuiga mfano huo wa kuwasifu wake zao na kuwashukuru pamoja na kuomba msamaha wanapokosea ili ndoa zao zijengwe katika misingi ya urafiki na penzi la kweli na sio ubabe kama ilivyo miongoni mwa wanajamii wengi. Kitabu cha MUNGU NA UZAO WANGU kimezinduliwa Jumapili iliyopita ambapo pamoja na mambo mengine Mwl. Lilian Ndegi ameelezea kwa kina juu ya Uzao wa Mwenye Haki,Nalikujua kabla ya Mimba Haijatungwa Tumboni mwa Mama Yako,Nafasi ya Mwanamume Wakati wa Ujauzito Mpaka Malezi,Magonjwa na Mateso Mengineyo Katika Kipindi cha Ujauzito,Mtazamo wa Wazazi juu ya Uzao Wao,Mtazamo wa Mungu juu ya Uzao wa Mwenye Haki,Mwanamke anahitaji ujasiri Mwingi wakati wa Kujifungua pamoja na uzazi wa Mpango ndizo sura 8 za kitabu hicho Hiki ni kitabu cha pili kikitanguliwa na kitabu chake cha kwanza JE UNASAMEHE? Ambavyo vyote vinapatikana madukani jipatie nakala yako. kwa jumla na rejareja simu nambari 0754465578 au 0655465578 barua pepe lilyonesmo@gmail.com web: www.lwc.or.tz. Story:Ritha Chuwalo |
Living Waters walihudumu siku hiyo |
Ilikuwa furaha sana kwa kwa upande wa akina mama siku hiyo |
Watumishi wa Mungu mbalimbali wakitamka Neno na kukiweka wakfu kitabu hicho |
Mzee Ernest Tarimo,Mmoja wa watu waliotoa mchango katika uandishi wa kitabu hicho akipokea bahasha ya shukrani siku hiyo |
Mmoja wa watu waliotoa mchango katika uandishi wa kitabu hicho ni Dr kwa tahaluma akipokea bahasha ya shukrani siku hiyo |
Apostle Ndegi na Mke wake Lilian Ndegi wakikata keki |
Lilian Ndegi akimlisha keki mme wake Apostle Ndegi kumshukuru lakini pia kumpongeza kwa kazi kubwa ya kumtia moyo katika kipindi cha uandishi wa kitabu cha MUNGU NA UZAO WANGU |
Mtumishi wa Mungu Rose Mushi alikuwepo katika Uzinduzi huo akiwa ni mmoja wa watu waliohusika katika kitabu hicho kukamilika. |
Ritha Chuwalo Mtangazaji wa Wapo Redio FM akilishwa keki baada ya kununua kitabu siku hiyo ya uzinduzi wa kitabu hicho cha MUNGU NA UZAO WANGU |
Grace Kakiziba akilishwa keki baada ya kununua kitabu siku hiyo ya uzinduzi wa kitabu hicho cha MUNGU NA UZAO WANGU |
Edna Luvanda Mke wa Antony Luvanda MC maarufu nchini akilishwa keki baada ya kununua kitabu siku hiyo ya uzinduzi wa kitabu hicho cha MUNGU NA UZAO WANGU |
Hadson Kamoga akimmiminia Apostle Ndegi Champagne ikiwa ni katika kujipongeza baada ya kuzindua kitabu cha MUNGU NA UZAO WANGU |
Wamama wa Living Water Centre na Lilian Ndegi |
Mwalimu wa Vijana mwandishi wa Vitabu Rose Mushi akiwa na Mwalimimu Lilian Ndegi |
Watumishi wa Mungu kutoka huduma na Makanisa mbalimbali waliokuwepo kuhudhulia uzinduzi huo wa kitabu cha MUNGU NA UZAO WANGU |
Islamic Extremists in Nigeria Attack Christians at Sunday Worship Every Week in January
JOS, Nigeria – Islamic extremists have attacked villages in three states in Nigeria every Sunday this month, killing at least 15 Christians.
Christian leaders in the Agatu Local Government Area of central Nigeria's Benue state said ethnic Fulani herdsmen were responsible for raids on two villages that left seven Christians dead on Sunday morning (Jan. 19), though a Fulani spokesman said the assailants must have come from elsewhere as there are no Fulani herdsmen known in the area.
The previous Sunday (Jan. 12) in northeastern Nigeria's Borno state, Christian leaders said terrorists from the Islamic extremist Boko Haram group attacked Sabon Gari village in the Gwoza Local Government Area, killing eight Christians. In Kaduna state the Sunday before that (Jan. 5), churchmen in the Manchok area mobilized in time to repel attacks by Fulani herdsmen, Christian leaders told Morning Star News.
The Rev. Yakubu Gandu Nkut of the ECWA in Zankan village, near Manchok. |
In the Benue state attacks, Fulani herdsmen raided Oweto and Utuluewu villages at about 10 a.m., destroying homes and maiming and killing Christian residents, two Christian leaders said.
"They killed seven of our community members in Oweto and Utuluewu villages in Agatu, while many others were injured in the attack," John Ngbede told Morning Star News. "There was sporadic shooting in these two Christian communities in the early hours of Sunday, at about 10 a.m., when they were in their churches. This incident has forced Christian surviving residents of the two communities to flee their villages."
Ngbede said the names of the slain Christians were not immediately available.
"However, I am sure of the casualty figure of those killed by the Fulani herdsmen," he said. "Seven of them were killed in the attack."
Sule Audu, another Christian community leader in the area, told Morning Star News by phone that a relative, 60-year-old Isah Onum, was among the seven killed.
"I do not understand the rationale behind these incessant killing of our people and the destruction of their homes," Audu said.
Daniel Ezeala, police spokesman for the Benue State Command, confirmed that seven Christians were killed in Sunday's attacks in Agatu. Five soldiers were also killed in the course of intervening.
The state secretary of the Myetti Allah Cattle Breeders Association of Nigeria, Garus Gololo, reportedly said the assailants must have come from outside the area as he was not aware of any herdsmen in the Idoma-speaking areas of Agatu.
"I'm so sad over the killings in the area," he said. "I'm also told that the soldiers fell in the middle of the crossfire between the Agatu and Fulanis. The killers should be arrested and prosecuted."
In the attacks that killed eight Christians in Borno state, Boko Haram Islamists stormed Sabon Gari village in the Gwoza Local Government Area the night of Jan. 12, according to area Christian leader Peter Biye Gumte. The onslaught came after Boko Haram members destroyed a Church of the Brethren in Nigeria building in Bzuba village on Jan. 8.
Boko Haram insurgents last month attacked four predominantly Christian villages in the Gwoza, Damboa and askira-Uba Local Government Areas, leading to death of at least 26 Christians and destroying about 40 homes. The attacks in Bdagu, Izge, Hartsa and Yazza villages took place from Dec. 8 to Dec. 11.
In Plateau state, Fulani herdsmen in the Langtang North Local Government Area on Jan. 16 killed three Christians and wounded four others in Nwore and Yokdara villages, an area res
"The attackers were Fulani herdsmen, Muslims," Nanpon Miri told Morning Star News. "They attacked the two villages during the morning hours, at about 10 a.m."
Repelling the Fulani
In Kaduna state, the attempt by churchmen to defend themselves against armed Fulani herdsmen on Jan. 5 escalated into clashes in a cluster of villages, killing at least five of the assailants and leaving one Christian wounded.
Christian leaders in Manchok in the Kaura Local Government Area said they were thankful to God that Catholic parishioners leaving worship at about 11 a.m. caught sight of two vehicles full of invading ethnic Fulani gunmen – unknown to area Fulanis – in time for churchmen to mobilize to repel them. They said the Fulani herdsmen sought to kill Christians during Sunday worship.
"The gunmen shot indiscriminately at Christians who prevented them from gaining entrance into churches," the Rev. Yakubu Gandu Nkut of the Evangelical Church Winning All (ECWA) in Zankan village, near Manchok, told Morning Star News. "All churches in Manchok, Zankan, Sabon Gari, Fadan Attakar, Gizagwai, Zangang, and in surrounding villages were forced to end their worship services abruptly because of the early morning invasion by these Fulani gunmen."
The Fulani began shooting at crowds of Christians that had gathered to confront them by a church in the Sabon Gari area of Manchok, he said."A member of my church was shot by the gunmen and was injured," said Nkut, also chairman of the local chapter of the Christian Association of Nigeria.
Eyewitnesses told Morning Star News that some of the armed attackers were killed in the fracas as they attempt to gain access to churches in Manchok. Kumai Badu, chairman of the Kaura Local Government Council, said five people died in the thwarted attack on area churches but declined further comment.
"It is true that some gunmen were here to attack churches, and this led to a clash between some Christians and Fulani herdsmen, which led to the killing of five persons this morning," Badu said on Jan. 5. "There was a quick intervention from the military stationed here, and everywhere is calm."
A Fulani herdsman in Bungen village, near Manchok, 23-year-old Hashimu Pati, told Morning Star News that some Muslim Fulani gunmen unknown to area herdsmen came to Manchok and caused problems between them and Christians with whom they had been living peacefully.
"Yes, some Fulani armed gunmen were seen in Manchok town – they have brought problems between us and our Christian neighbors," Pati said. "I appeal to the government to help us by assisting to rebuild some of our houses destroyed in the aftermath of the aborted attack on churches."
Christian leaders said the incursion resulted in chaos and confusion in Manchok and all surrounding villages, and houses and vehicles were destroyed in clashes between assailants and Christians.Services at Baptist, Catholic, Church of Christ in Nations, Pentecostal and ECWA churches were cut short, Nkut said.
Bwayan Silas, a Catholic leader in Bungen village, near Manchok, said the raid stopped his worship.
"We were in the church here, the St. Peter's Catholic Church, when we heard sounds of gun shots," Silas said. "We all ran out of the church and found that some Fulani gunmen had invaded the town of Manchok and other communities around. Scared about what was happening as we saw gunmen rushing into our village, we all took to our heels in different directions."
A resident of Manchok said the gunmen left a note in the town threatening further attacks on Christian communities in the area since the Jan. 5 attack was thwarted."The Fulani gunmen yesterday [Jan. 8], dropped a letter in the town warning Christians to be prepared for a total war in the coming weeks," Solomon Musa told Morning Star News
Viongozi wa dini wataka gesi inufaishe Watanzania
Viongozi wa dini kutoka madhehebu mbalimbali nchini wameitaka serikali kuhakikisha kwamba rasilimali ya gesi asilia inawanufaisha kwanza wazawa kabla ya kupelekwa nje.
Maombi hayo kwa serikali yalitolewa na viongozi hao wa dini mbele ya Rais Jakaya Kikwete katika kongamano lao lililofanyika jana jijini Dar es Salaam kujadili matumizi ya rasilimali za madini, gesi na mafuta kwa ajili ya manufaa ya Watanzania na taifa kwa ujumla.
“Pamoja na serikali kufungua milango kwa wawekezaji lakini iweke kipaumbele cha kwanza kwa wawekezaji wazalendo ili waweze kunufaika na rasilimali za nchi yao kisha iwatazame wawekezaji wa nje,” alisema Sheikh Abubakar Zubeir, aliyewasilisha maombi hayo kwa serikali kwa niaba ya Baraza la Waislamu Tanzania (Bakwata).
Sheikh Zubeir aliongeza: “Pamoja na kuwa makini na mikataba inayowekwa iwe ni kwa maslahi zaidi kwa nchi na wananchi wake na kuwalinda na athari mbaya zinazoweza kusababishwa na uwekezaji usiozingatia taratibu, sheria na kanuni na kuisababishia nchi kuingia kwenye matatizo.”
Viongozi hao waliongeza kuwa serikali haipaswi kusema kuwa Watanzania hawana mtaji wa kuvuna rasilimali hizo ikiwamo gesi asilia kwani kwa kufanya hivyo kunatoa mwanya kwa mataifa ya kigeni kunufaika nazo badala ya wazalendo.
“Kusema Watanzania hawana mtaji wa kuvuna rasilimali hizi ni sawa na kufumbwa macho, na ni mtazamo potofu kwani wageni wanatumia udhaifu huo huo kwa ajili ya kuja kutawala rasilimali zetu kwa kusema kwamba wao wenyewe wamesema, hatuwezi kuvuna gesi kwa kuwa hatuna mtaji,” alisema Dk. Padri Charles Kitima, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (Saut).
Aliitaka serikali kuwapa wazawa uhuru wa kutafakari na kupendekeza maamuzi juu ya manufaa ya rasilimali za nchi na kwamba umiliki wa rasilimali hizo ndiyo unaofanya nchi husika kusonga mbele kiuchumi badala ya kusema inakusanya kodi huku wageni wakiendelea kunufaika nazo.
Padri Kitima pia aliwataka viongozi wa dini waliohudhuria kongamano hilo kuwafunda viongozi wa serikali ili wabadilike na kuwa waadilifu katika matumizi sahihi ya rasilimali hizo.
Pia, waliwataka Watanzania kutokubali kutumiwa kuhujumu rasilimali za nchi na kwamba wanapaswa kuwa na moyo wa uzalendo kwa kutambua kuwa rasilimali yoyote inapopatikana katika maeneo yanayowazunguka siyo yao pekee, bali kwa wananchi wote ili kulinda maslahi ya utaifa.
Kadhalika, waliitaka serikali kuweka taratibu nzuri za kulinda rasilimali za nchi ili ziwanufaishe wote sambamba kuundwa kwa taasisi zenye uadilifu.
Vile vile, viongozi wa dini waliitaka serikali kuwa makini na baadhi ya wanasiasa na wanaharakati wanaotumia nafasi zao kuipotosha jamii na kuleta mafarakano na machafuko kwa ajili ya manufaa yao.
KAULI YA RAIS KIKWETE
Akizungumza kwenye kongamano hilo lililokusanya viongozi wa dini takribani 120 kutoka mikoa mbalimbali nchini, Rais Jakaya Kikwete alisema serikali itahakikisha sehemu kubwa ya gesi asilia itakakayovunwa inatosheleza kwanza mahitaji ya nchi kabla ya kuuzwa nje. Alisema haiwezekani gesi ikaanza kuuzwa nje ikiwa nchi bado haijanufaika vya kutosha kwa ajili ya maendeleo ya viwanda vikubwa.
Kuhusu ushiriki wa wazawa kwenye rasilimali za nchi, Rais Kikwete alifafanua kuwa, serikali haijaizuia kampuni yoyote, wala mtu au mbia yeyote kwenda katika ofisi za Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kununua fomu ya kuomba kutafuta rasilimali hiyo.
Kwa mujibu wa Rais Kikwete, kinacholeta malumbano makubwa kuhusu gesi ni kwa kampuni husika kutaka kupewa upendeleo na kutengewa eneo maalumu kwani utafutaji wa rasilimali hiyo hadi kuipata ni kama mchezo wa kubahatisha.
Aliongeza kuwa, rasilimali za nchi zisipolindwa vizuri zitaleta maangamizi badala ya neema kwani kuna nchi nyingi duniani ambazo zimeendelea kuteseka na matumizi mabaya ya utajiri wa rasilimali hizo.
Akitolea mfano wa mitambo ya kisasa iliyojengwa baharini kwa ajili ya kutafuta gesi, alisema utafutaji wake una gharama kubwa kwani unahitaji kampuni kubwa zenye fedha zake ambazo ni zaidi ya maelfu ya bajeti ya serikali ya Tanzania.
Rais Kikwete pia aliliagiza TPDC kujiandaa kuchukua leseni kwa ajili ya kuanza utafutaji wa gesi kama kampuni zingine zinazojitegemea badala ya kusimamia tu na kutangaza tenda.
Aliongeza kuwa kwa sasa serikali inataka kulifanya jiji lote la Dar es Salaam kuanza kutumia nishati ya gesi lengo ni kuokoa mazingira pamoja na kupunguza ukataji wa miti ovyo kwa ajili ya kupata mkaa wa kupikia.
Alisema serikali inatarajia kupata umiliki wa gesi wa asilimia 65 hadi 70 kutoka kampuni za ndani wakati kwa kampuni za nje itapata umiliki wa asilimia 70 huku asilimia 30 ikienda kwa kampuni husika.
Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo, alisema, rasilimali ya gesi ndiyo itakayowatoaWatanzania katika wimbi la umaskini kwani shughuli za uvuvi wa samaki na biashara ambayo ilianza enzi za utumwa, lakini hazijaweza kuwaondoa wananchi kutoka katika wimbi hilo.
Jumuiya za dini zilizowakilishwa ni Bakwata, Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Jumuiya ya Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (CPCT), Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) na Kanisa la Wasabato Tanzania (SDA).
Maombi hayo kwa serikali yalitolewa na viongozi hao wa dini mbele ya Rais Jakaya Kikwete katika kongamano lao lililofanyika jana jijini Dar es Salaam kujadili matumizi ya rasilimali za madini, gesi na mafuta kwa ajili ya manufaa ya Watanzania na taifa kwa ujumla.
“Pamoja na serikali kufungua milango kwa wawekezaji lakini iweke kipaumbele cha kwanza kwa wawekezaji wazalendo ili waweze kunufaika na rasilimali za nchi yao kisha iwatazame wawekezaji wa nje,” alisema Sheikh Abubakar Zubeir, aliyewasilisha maombi hayo kwa serikali kwa niaba ya Baraza la Waislamu Tanzania (Bakwata).
Sheikh Zubeir aliongeza: “Pamoja na kuwa makini na mikataba inayowekwa iwe ni kwa maslahi zaidi kwa nchi na wananchi wake na kuwalinda na athari mbaya zinazoweza kusababishwa na uwekezaji usiozingatia taratibu, sheria na kanuni na kuisababishia nchi kuingia kwenye matatizo.”
Viongozi hao waliongeza kuwa serikali haipaswi kusema kuwa Watanzania hawana mtaji wa kuvuna rasilimali hizo ikiwamo gesi asilia kwani kwa kufanya hivyo kunatoa mwanya kwa mataifa ya kigeni kunufaika nazo badala ya wazalendo.
“Kusema Watanzania hawana mtaji wa kuvuna rasilimali hizi ni sawa na kufumbwa macho, na ni mtazamo potofu kwani wageni wanatumia udhaifu huo huo kwa ajili ya kuja kutawala rasilimali zetu kwa kusema kwamba wao wenyewe wamesema, hatuwezi kuvuna gesi kwa kuwa hatuna mtaji,” alisema Dk. Padri Charles Kitima, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (Saut).
Aliitaka serikali kuwapa wazawa uhuru wa kutafakari na kupendekeza maamuzi juu ya manufaa ya rasilimali za nchi na kwamba umiliki wa rasilimali hizo ndiyo unaofanya nchi husika kusonga mbele kiuchumi badala ya kusema inakusanya kodi huku wageni wakiendelea kunufaika nazo.
Padri Kitima pia aliwataka viongozi wa dini waliohudhuria kongamano hilo kuwafunda viongozi wa serikali ili wabadilike na kuwa waadilifu katika matumizi sahihi ya rasilimali hizo.
Pia, waliwataka Watanzania kutokubali kutumiwa kuhujumu rasilimali za nchi na kwamba wanapaswa kuwa na moyo wa uzalendo kwa kutambua kuwa rasilimali yoyote inapopatikana katika maeneo yanayowazunguka siyo yao pekee, bali kwa wananchi wote ili kulinda maslahi ya utaifa.
Kadhalika, waliitaka serikali kuweka taratibu nzuri za kulinda rasilimali za nchi ili ziwanufaishe wote sambamba kuundwa kwa taasisi zenye uadilifu.
Vile vile, viongozi wa dini waliitaka serikali kuwa makini na baadhi ya wanasiasa na wanaharakati wanaotumia nafasi zao kuipotosha jamii na kuleta mafarakano na machafuko kwa ajili ya manufaa yao.
KAULI YA RAIS KIKWETE
Akizungumza kwenye kongamano hilo lililokusanya viongozi wa dini takribani 120 kutoka mikoa mbalimbali nchini, Rais Jakaya Kikwete alisema serikali itahakikisha sehemu kubwa ya gesi asilia itakakayovunwa inatosheleza kwanza mahitaji ya nchi kabla ya kuuzwa nje. Alisema haiwezekani gesi ikaanza kuuzwa nje ikiwa nchi bado haijanufaika vya kutosha kwa ajili ya maendeleo ya viwanda vikubwa.
Kuhusu ushiriki wa wazawa kwenye rasilimali za nchi, Rais Kikwete alifafanua kuwa, serikali haijaizuia kampuni yoyote, wala mtu au mbia yeyote kwenda katika ofisi za Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kununua fomu ya kuomba kutafuta rasilimali hiyo.
Kwa mujibu wa Rais Kikwete, kinacholeta malumbano makubwa kuhusu gesi ni kwa kampuni husika kutaka kupewa upendeleo na kutengewa eneo maalumu kwani utafutaji wa rasilimali hiyo hadi kuipata ni kama mchezo wa kubahatisha.
Aliongeza kuwa, rasilimali za nchi zisipolindwa vizuri zitaleta maangamizi badala ya neema kwani kuna nchi nyingi duniani ambazo zimeendelea kuteseka na matumizi mabaya ya utajiri wa rasilimali hizo.
Akitolea mfano wa mitambo ya kisasa iliyojengwa baharini kwa ajili ya kutafuta gesi, alisema utafutaji wake una gharama kubwa kwani unahitaji kampuni kubwa zenye fedha zake ambazo ni zaidi ya maelfu ya bajeti ya serikali ya Tanzania.
Rais Kikwete pia aliliagiza TPDC kujiandaa kuchukua leseni kwa ajili ya kuanza utafutaji wa gesi kama kampuni zingine zinazojitegemea badala ya kusimamia tu na kutangaza tenda.
Aliongeza kuwa kwa sasa serikali inataka kulifanya jiji lote la Dar es Salaam kuanza kutumia nishati ya gesi lengo ni kuokoa mazingira pamoja na kupunguza ukataji wa miti ovyo kwa ajili ya kupata mkaa wa kupikia.
Alisema serikali inatarajia kupata umiliki wa gesi wa asilimia 65 hadi 70 kutoka kampuni za ndani wakati kwa kampuni za nje itapata umiliki wa asilimia 70 huku asilimia 30 ikienda kwa kampuni husika.
Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo, alisema, rasilimali ya gesi ndiyo itakayowatoaWatanzania katika wimbi la umaskini kwani shughuli za uvuvi wa samaki na biashara ambayo ilianza enzi za utumwa, lakini hazijaweza kuwaondoa wananchi kutoka katika wimbi hilo.
Jumuiya za dini zilizowakilishwa ni Bakwata, Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Jumuiya ya Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (CPCT), Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) na Kanisa la Wasabato Tanzania (SDA).
Sorcce:Nipashe
Mahusiano yako na Mungu ni ya Muhimu zaidi kuliko Mahitaji yako Kujibiwa, naye na Mungu hutumia sana uhitaji wetu kuimalisha mahusiano yake nasi
Carlos Ricky Wilson Kirimbai |
Swala la mahusiano yako na Mungu ni la muhimu zaidi kwa Mungu kuliko swala la kujibu maombi yako kwa hiyo Mungu anapenda sana kama una uhitaji au changamoto, wewe mwenyewe uende mbele zake na hitaji lako kuliko kuwaambia wengine tu wakuombee. Ukienda mbele za Mungu na uhitaji wako itatoa fursa ya vitu viwili vikubwa kutokea.
1. Kuimarika kwa mahusiano yako na Mungu maana siku zote mazungumzo kati ya wawili huimarisha mahusiano kati yao.
2. Uhitaji wako kujibiwa na Mungu na hivyo kukufanya wewe kukua katika kumjua kwako Mungu.
Zaburi 103: 7
7Alimjulisha Musa njia zake,
Wana wa Israeli matendo yake.
Usiwe mtu tu wa kutamani kuyajua matendo ya Mungu uwe mtu anayetamani kuzijua na njia zake pia.
Wana wa Israeli waliyajua tu matendo ya Mungu maana kila wakipata changamoto walikuwa wanamfuata Musa. Utakuwa mpendwa anayejua tu matendo ya Mungu kama kila unapopata changamoto wewe ni mbio kwa mchungaji wako, au mtumishi fulani wa Mungu au watu wengine wao wakuombee.
Musa alijua njia za Mungu kwa sababu kila akipata changamoto alikuwa akienda kwa Mungu na hakuwa na mtu wa katikati wa kumwendea.
Tamani kuwa kama Musa na sio wana wa Israel.
Ayubu anatuambia kwenye Ayubu 22: 21.
21 Mjue sana Mungu, ili uwe na amani;
Ndivyo mema yatakavyokujia.
Ukimjua sana Mungu utakuwa na amani. Amani ni neno Shalom linalomaanisha hakuna kilichopungua na hakuna kilichovunjika. Ukimjua Mungu hakuna kitakachopungua na hakuna kitakachokuwa kimevunjika maishani mwako na mema yatakujia.
Kwanini usitamani kumjua Mungu ili uwe na amani na mema yakujie? Kwanini Mchungaji wako amjue Mungu zaidi kupitia changamoto zako wewe?
Daudi anatuambia kwenye Zaburi 34: 10.
10Wana-simba hutindikiwa, huona njaa;
Bali wamtafutao BWANA hawatahitaji kitu cho chote kilicho chema.
Tafuta kumjua Mungu. tafuta kumsogelea wewe na sio mwingine amsogelee kwa niaba yako.
1. Kuimarika kwa mahusiano yako na Mungu maana siku zote mazungumzo kati ya wawili huimarisha mahusiano kati yao.
2. Uhitaji wako kujibiwa na Mungu na hivyo kukufanya wewe kukua katika kumjua kwako Mungu.
Zaburi 103: 7
7Alimjulisha Musa njia zake,
Wana wa Israeli matendo yake.
Usiwe mtu tu wa kutamani kuyajua matendo ya Mungu uwe mtu anayetamani kuzijua na njia zake pia.
Wana wa Israeli waliyajua tu matendo ya Mungu maana kila wakipata changamoto walikuwa wanamfuata Musa. Utakuwa mpendwa anayejua tu matendo ya Mungu kama kila unapopata changamoto wewe ni mbio kwa mchungaji wako, au mtumishi fulani wa Mungu au watu wengine wao wakuombee.
Musa alijua njia za Mungu kwa sababu kila akipata changamoto alikuwa akienda kwa Mungu na hakuwa na mtu wa katikati wa kumwendea.
Tamani kuwa kama Musa na sio wana wa Israel.
Ayubu anatuambia kwenye Ayubu 22: 21.
21 Mjue sana Mungu, ili uwe na amani;
Ndivyo mema yatakavyokujia.
Ukimjua sana Mungu utakuwa na amani. Amani ni neno Shalom linalomaanisha hakuna kilichopungua na hakuna kilichovunjika. Ukimjua Mungu hakuna kitakachopungua na hakuna kitakachokuwa kimevunjika maishani mwako na mema yatakujia.
Kwanini usitamani kumjua Mungu ili uwe na amani na mema yakujie? Kwanini Mchungaji wako amjue Mungu zaidi kupitia changamoto zako wewe?
Daudi anatuambia kwenye Zaburi 34: 10.
10Wana-simba hutindikiwa, huona njaa;
Bali wamtafutao BWANA hawatahitaji kitu cho chote kilicho chema.
Tafuta kumjua Mungu. tafuta kumsogelea wewe na sio mwingine amsogelee kwa niaba yako.
Rais Kikwete afungua Kongamano la Viongozi wa Dini Kuhusu Matumizi ya rasilimali za Nchi, Gesi,Mafuta na Madini kwa Maendeleo ya Tanzania
HOTUBA YA MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS WA
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, WAKATI UFUNGUZI WA
KONGAMANO LA VIONGOZI WA DINI KUHUSU MATUMIZI YA
RASILIMALI ZETU ZA GESI ASILIA, MAFUTA NA MADINI KWA
AMANI NA MAENDELEO YA TANZANIA, WHITESANDS HOTEL,
TAREHE 20-22 JANUARI 2014
Waheshimiwa Viongozi wa Dini;
Waheshimiwa Mawaziri;
Waheshimiwa Wakuu wa Mikoa;
Ndugu Makatibu Wakuu;
Wageni Waalikwa;
Mabibi na Mabwana;
Naomba nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema,
kwa kutujaalia uzima na kutuwezesha kukutana hapa siku ya leo kujadili
matumizi
ya rasilimali zetu za gesi asilia, mafuta na madini kwa amani na
maendeleo ya nchi
yetu. Kwa namna
ya pekee nawashukuru viongozi
wa dini kwa
kunishirikisha
kwenye Kongamano hili
muhimu na la
aina yake. Mmenipa
heshima kubwa
ambayo sikuitegemea. Asanteni
sana.
Nawapongeza sana kwa uamuzi wenu wa busara wa kuandaa Kongamano
hili. Mmedhihirisha kwa
vitendo uhodari wenu wa kutekeleza
jukumu lenu la
msingi la kulea taifa letu kiroho na kushiriki kikamilifu katika
masuala mengine
muhimu yahusuyo maendeleo na ustawi
wa Tanzania na watu wake. Ninyi
ni
wazalendo wa kweli. Ni matumaini
yangu na ya Serikali ninayoingoza kuwa ubia
wa aina hii utaimarishwa na kudumishwa kwa faida ya nchi yetu.
Najua mlianza kwa kukereketwa na athari za matumizi
makubwa ya miti
kwa matumizi ya nishati jambo ambalo linachangia sana kuharibika kwa mazingira
duniani. Mmeishia kwenye
Kongamano hili. Lina uwiano kabisa kwani
tunakata
miti kwa ajili ya kuni na mkaa.
Tukitumia gesi itatoa huko. Ni
dhamira yetu hiyo.
Ndugu Viongozi wa Dini;
Kongamano hili linafanyika
katika kipindi mwafaka
kabisa, kipindi
ambacho ugunduzi mkubwa wa gesi tayari umefanyika na dalili za
kugunduliwa
zaidi zipo. Kipindi ambacho
hazina ya madini mbalimbali inazidi kugunduliwa na
makampuni ya utafiti yanatupa moyo kuwa mambo huenda yakawa mazuri
zaidi.
Pia, ni kipindi
ambacho rasilimali zetu za
wanyamapori na misitu
zinatishiwa
kutoweka. Ni kipindi ambacho
wakulima na wafugaji na wafugaji na wahifadhi
wa misitu na wanyamapori wanashindania ardhi ya kufanyia shughuli
zao.
Sasa
hivi ni kipindi mwafaka kabisa kukaa chini na kutafakari jinsi gani
rasilimali hizi
zinaweza kulindwa na kutumika kwa manufaa ya nchi yetu na watu wake
wote
zikiwanufaisha kule ambako rasilimali hizo zipo na hata kule ambako
hazipo.
Ni ukweli usiopingika kuwa Mwenyezi Mungu ameijalia nchi yenye utajiri
mkubwa wa rasilimali za asili.
Ametujaalia ardhi kubwa yenye rutuba, madini ya
aina mbalimbali, misitu na
mbuga za wanyama wa kila aina, hali ya hewa nzuri,
bahari, maziwa makubwa, mito mingi, watu wengi na kadhalika. Rasilimali hizi,
kwa tabia yake,
inatakiwa zitumiwe vizuri
ili kuboresha hali
na maisha ya
Watanzania wote sawia na kwa miaka mingi na hata milele. Vinginevyo rasilimali
hizi zinaweza kugeuka
kuwa chanzo cha
mifarakano, magomvi na
mauaji.
Zinaweza kuwa balaa na kuleta maangamizi nchini
badala ya kuwa baraka na
neema.
Mifano ipo ya nchi mbalimbali
duniani zilizojikuta zina migogoro na vita
vya wenyewe kwa wenyewe kutokana na kugombania utajiri wao wa
rasilimali za
asili. Watu wa nchi hizo
wanajuta kuwa na rasilimali ambazo zimekuwa chanzo
cha kuhatarisha amani, utulivu,
usalama na hata uhai wao. Kwa hapa
Tanzania
tunashukuru Mungu rasilimali hazijageuka kuwa balaa na tunaomba hilo
lisitokee.
Tangu Tanganyika ipate
uhuru na Zanzibar
kufanya Mapinduzi Matukufu
na
hatimaye nchi zetu mbili kuungana
na kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Serikali za awamu
zote zimesimamia kwa
makini rasilimali za
nchi yetu ili
ziwanufaishe Watanzania wote.
Tumetunga sheria na sera mbalimbali kuhakikisha
kuwa lengo letu hilo linatimia.
Hata hivyo, usimamizi
wa sheria hizo na
utekelezaji wa sera
zetu nzuri
umekuwa unakabiliwa na
changamoto mbalimbali kwa
nyakati mbalimbali.
Mpaka hapa tulipofika ni umahiri wa viongozi wetu ndiyo uliotuwezesha
kuzuia
mambo yasiharibike na kugeuka kuwa matatizo makubwa. Tumefanikiwa kiasi
chake ingawaje hatujaweza kuzuia kabisa matatizo yasitokee hapa na
pale. Taarifa
za kugombea rasilimali zimekuwa
zinasikika na nyingine zikiwa zimesababisha
watu kupoteza maisha, kujeruhiwa na mali kuharibiwa. Tutafanya nini kukomesha
hali hiyo isijitokeze, ni jambo ambalo sisi kama taifa, yaani
Serikali, wananchi na
wadau mbalimbali, wakiwemo
viongozi wa dini hatuna, budi kulizungumza
na
kulipatia ufumbuzi.
Ndugu Viongozi wa Dini;
Nimefarijika sana na uamuzi wenu wa kufanya mkutano huu kuzungumzia
rasilimali ya mafuta na
gesi. Juhudi za kutafuta mafuta na
gesi imeanza tangu
ukoloni, zikaendelea katika awamu zote baada ya Uhuru. Shirika la
Maendeleo ya
Petroli (TPDC) lilianzishwa
mwaka 1969 kuongoza juhudi hizo na kusimamia
sekta ya mafuta nchini kwa manufaa ya Watanzania wote. Hatujajaaliwa kupata
mafuta mpaka sasa lakini tumefanikiwa kupata gesi. Ugunduzi wa kwanza wa gesi
asilia ulifanyika Songosongo mwaka 1971 na baadae Msimbati, Mtwara mwaka
1982. Utafutaji na ugunduzi huo
uligharimiwa na Serikali yetu na hivyo gesi hiyo
ni mali ya Serikali. Baada ya
ugunduzi huo makampuni binafsi yalipata shauku ya
kutafuta mafuta na gesi nchini.
Mwaka 1980 ikatungwa Sheria ya Utafutaji wa Uzalishaji wa Mafuta kwa
nia ya kuweka masharti na utaratibu wa makampuni kushiriki katika
utafutaji na
uzalishaji wa mafuta na
gesi nchini. Pia unatoa mwongozo wa mgawanyo wa
mapato baina ya
makampuni na Serikali.
Sheria hiyo imeendelea
kufanyiwa
maboresho kwa nyakati
mbalimbali kulingana na
mahitaji ya wakati
husika.
Kuanzia mwaka 2007 shughuli za utafutaji wa mafuta na gesi asilia
ziliongezeka
kwa nguvu na
kasi kubwa. Juhudi
hizo zilizaa matunda
mwaka 2010 kwa
uvumbuzi wa kwanza
wa gesi katika
Bahari Kuu uliofanywa na
Kampuni za
Orphir na British Gas. Baada ya
hapo ugunduzi umeendelea hadi kufikia futi za
ujazo trilioni 46.5 za rasilimali ya gesi nchini mpaka sasa. Utafiti unaendelea na
matumaini ya kupata gesi zaidi
yapo. Kufuatia ugunduzi huo, Tanzania
sasa ni
moja ya nchi zimazohesabiwa kuwa na gesi nyingi duniani na ni nchi
inayovutia
wawekezaji wengi katika sekta
ya gesi. Kwa sababu hiyo, tukaamua
kuifanyia
mapitio Sheria ya
Utafutaji na Uzalishaji
wa Mafuta na
Gesi. Mwaka 2013
tumetunga Sera ya
Gesi na kurekebisha
masharti ya Mkataba
wa Kugawana
Mapato yatokanayo na gesi
(Production Sharing Agreement) na
kuongeza mgao
wa Serikali.
Ndugu Viongozi wa Dini;
Sera ya Gesi
Asilia iliyopitishwa mwezi
Oktoba, mwaka jana
(2013)
imeeleza wazi, tena
kwa lugha nyepesi,
kuwa gesi ya
Tanzania ni mali
ya
Watanzania wote na itatumika kwa manufaa ya Watanzania wote – wa
kizazi hiki
na kijacho. Katika
matumizi ya gesi, kipaumbele kitakuwa matumizi ya ndani.
Msingi wa hoja yetu ni ule ukweli kwamba ukiuza nje gesi yote, unapata mapato
peke yake lakini unakosa faida nyinginezo. Ukiitumia ndani unapata mapato na
faida nyingine nyingi, kwa mfano, uzalishaji wa umeme, matumizi ya
majumbani,
kwenye magari na
viwandani kuzalisha bidhaa
mbalimbali. Hivyo basi
mnapoitumia ndani gesi inakuwa kichocheo kikubwa cha maendeleo ya nchi
yetu.
Vilevile tupo katika mchakato
wa kuandaa sera
ya kuwashirikisha zaidi
Watanzania (Local Content Policy) ili wanufaike zaidi na
rasilimali yao ya gesi.
Kwa sasa nimewaagiza
TPDC wajiandae kushiriki
katika utafutaji wa
gesi,
uzalishaji wake mpaka
inapofika sokoni. Wasiwe
wagawaji vitalu tu
pekee.
Katika sera hiyo
mpya pia tunaangalia
shughuli zinazoweza kufanywa
na
Watanzania ili tuone njia bora
ya kuwawezesha kushiriki. Kwa sasa
tunadhani
wanaweza kushiriki kwa urahisi katika
utoaji wa huduma
kwa kampuni
zinazofanya utafiti na
uzalishaji wa gesi
na mafuta. Wapo
walioanza na
wanafaidika. Nia yetu ni kuona
idadi yao inaongezeka.
Mabibi na Mabwana;
Tumeanza pia mchakato
wa kuiboresha TPDC ishiriki
katika uwekezaji
kwenye sekta ya mafuta na gesi kwa niaba ya Watanzania. Katika utaratibu huo,
baadaye TPDC itauza hisa zake kwenye Soko la Mitaji ili Watanzania
washiriki
moja ka moja katika kumiliki rasilimali hii muhimu.
Ndugu Viongozi wa Dini;
Mambo yote hayo yanafanyika ili kuhakikisha masilahi ya taifa
yanalindwa
na Watanzania wote
wananufaika na rasilimali
zao kwa usawa.
Changamoto
kubwa tunayoiona kuhusu ushiriki wa Watanzania kwenye utafutaji na
uzalishaji
wa mafuta na gesi ni uwezo
mdogo wa fedha, utaalamu na teknolojia tulionao.
Fedha zinazohitajika kwenye shughuli ya utafutaji mafuta na gesi, kwa
mfano, ni
nyingi mno na Watanzania wenzetu hawanazo na hakuna uhakika wa benki
iliyo
tayari kumkopesha mtu asiyekuwa nacho.
Namna nyingine ni
kuwapa maeneo ili
wao watafute wabia
wawekeze.
Lakini, mnapokuwa mnasheria
inayoshirikisha ubia baina
ya Serikali na
mwekezaji, kuamua kuacha
Serikali ili badala yake apewe Mtanzania binafsi si
uamuzi rahisi sana kuufanya. Mtu binafsi ananufaika mwenyewe wakati
Serikali
inanufaisha wengi. Ninachokiona
nafuu kufanya ni kutumia mwanya wa ushiriki
wa TPDC ili tuone baadhi ya hisa ziuzwe kwa Watanzania. Hapa kunakuwa na
ubia wa TPDC na wananchi upande mmoja na Serikali upande mwingine.
Jambo lingine tunalolifanya
ni kuhakikisha kuwa
rasilimali ya gesi
inatumika vizuri, kwa manufaa ya kizazi cha sasa na vizazo
vijavyo. Tutaanzisha
mfuko maalum wa kuhifadhi mapato ya gesi na kuwekewa masharti ya
matumizi
yake. Tutatunga sheria maalum
kwa ajili hiyo na tutafanya hivyo kwaka huu.
Mabibi na Mabwaba;
Kwa upande wa rasilimali
ya madini mabadiliko makubwa ya kiuchumi
yaliyoanza miaka 1980 katikati, Serikali ilijitoa katika uwekezaji na
ikabaki kuwa
mhamasishaji na kuweka
mazingira mazuri ya
uwekezaji. Kufuatia hali
hiyo
wawekezaji wengi walianza kuja kuwekeza katika maeneo mbalimbali
pamoja na
utafutaji na uchimbaji wa madini.
Serikali ikaweka Sera (1997) na Sheria (1998)
ya madini kusimamia sekta hiyo.
Ni kweli mapato ya Serikali na fedha za kigeni
ziliongezeka kutokana na uzalishaji wa madini. Lakini palikuwa na manung’uniko
mengi kutoka kwa wananchi kuwa hawafaidiki sana na rasilimali zao.
Kamati mbalimbali ziliundwa
kuangalia tatizo lipo wapi ili
jawabu lake
litafutwe.
Nilipochaguliwa kuwa Rais
wa nchi yetu
mwaka 2005 niliyakuta
manung’uniko hayo na kuamua tuyatafutie jawabu. Mwaka 2006 nikaunda Kamati
ya Jaji Bomani
ili ichambuwe mapungufu
yaliyopo na kutoa mapendekezo ya
hatua za kuchukua. Matokeo ya
taarifa ya Kamati ile ni Sera Mpya ya
Madini
(2009) na Sheria Mpya ya Madini (2010). Sera
na Sheria hii inalenga kuongeza
faida zaidi kwa Serikali na jamii, bila kuwasahau wale wanaozunguka
migodi.
Faida hizo ni
pamoja na kuhimiza
kampuni za uchimbaji
wa madini
kufungamanisha uchumi kati ya sekta ya madini na nyingine. Vilevile tumewataka
waongeze nafasi ya ajira kwa Watanzania na ununuzi wa huduma na bidhaa
nchini.
Aidha, tumeamua Serikali
iwe inapata hisa
katika migodi mikubwa
itakayoanzishwa siku za usoni.
Ndiyo maana tunaendelea kufanya mazungumzo
na kampuni zitazochimba uranium na
nickel. Hatujamaliza lakini
tunakwenda
vizuri.
Halikadhalika, Sheria na Sera vimeweka mkazo wa kuendeleza wachimbaji
wadogo ambao ni
Watanzania tu. Katika
kutekeleza hilo, tumeanza
kutenga
maeneo kwa ajili yao.
Changamoto kubwa inayowakabili ni
ukosefu wa mitaji,
vifaa na utaalamu. Kuhusu fedha,
tumeanzisha mfuko wa kuwasaidia na mwaka
huu wa fedha tumewatengea jumla ya shilingi bilioni 2.5. Vile vile tunakamilisha
taratibu za kuanza kuwakodisha vifaa kupitia ofisi zetu za madini za
Kanda.
Jambo lingine kubwa ambalo tunajiandaa kulifanya ili kunufaisha
wananchi
na nchi yetu
ni kutunga Sheria
itakayohakikisha kuwa madini
mengi
yanayochimbwa nchini yanaongezewa
thamani hapahapa nchini.
Hatua hii
itachangia sana kuongeza mapato na fursa ya ajira kwa watu wetu.
Nduvu Viongozi wa Dini;
Nimeyasema haya yote
kuwaonesha kuwa Serikali
haina mchezo katika
usimamizi wa rasilimali zetu za asili.
Tunafanya hayo kwa vile tunafahamu kuwa
zinaweza kutuletea maendeleo ya haraka. Lakini pia zinaweza kusababisha nchi
yetu kuingia kwenye dimbwi la migogoro inayotokana na rasilimali. Yote mawili
yanaweza kutokea kutegemea tutasimamiaje na kuzitumiaje rasilimali
zetu.
Jambo la muhimu
ni kusaidiana kuelimisha jamii
ya Watanzania namna
tulivyojipanga kusimamia rasilimali
zetu za gesi
asilia, mafuta na
madini.
Waelewe kuwa utajiri
huu ni mali
yao na hivyo
ni haki yao
kunufaika nao.
Wafahamu kuwa ni wajibu wao kulinda na kuzitunza rasilimali hizo ili
zisipotee.
Ninyi mnayo dhamana ya kuelimisha jamii waelewe nia hiyo njema ya Serikali.
Pia napenda kusema kuwa siyo kweli kwamba Serikali haijali rasilimali
za nchi au
haitaki Watanzania wafaidike nazo; siyo kweli eti Serikali inapendelea
wawekezaji
wageni kuliko wazawa na hakuna mkoa au eneo linapuuzwa au kubaguliwa. Mimi
na Serikali ninayoiongoza
tutakua watu wa
mwisho kupuuza wazawa
na
kupendelea wageni au kupuuza watu wa maeneo ambako rasilimali zinapatikana
au hazijapatikana.
Ndugu Viongozi wa Dini;
Naomba muendelee kutekeleza jukumu lenu la msingi la kulea taifa
kiroho.
Mhimize waumini wenu wawe waadilifu na wazalendo. Waache kujihusisha na
vitendo viovu vya wizi,
ubadhilifu, matumizi mabaya ya madaraka na rushwa.
Mkifanikiwa hilo, rasilimali zetu zitakuwa salama. Vile vile muendelee kuhubiri
upendo miongoni mwenu, miongoni mwa waumini wenu na miongoni mwa watu
wote. Watu wakumbushwe kuwa
sisi wote ni viumbe wa Mungu na mbele yake
sisi wote ni
ndugu na inabidi kuheshimiana
na kuvumiliana kwa
tofauti zetu.
Tukifaulu kwenye hili nchi yetu itabaki salama daima milele.
Nafahamu kuwa wapo
baadhi ya watu
ambao wanafanya vitendo
vya
kuhujumu rasilimali zetu. Wapo wanaoingia mikataba isiyozingatia
maslahi ya
taifa katika uvunaji
wa rasilimali zetu.
Wapo wengine wanaokula njama
na
wawekezaji ili Serikali
ipunjwe mapato yake. Watu wa aina
hiyo wapo katika
jamii ye yote ile na sisi kuwa nao si ajabu. Napenda mfahamu kuwa Serikali
inapinga vitendo vya aina yoyote vya kuhujumu rasilimali zetu.
Ndiyo maana
watu wa aina
hiyo wanapobainika, wanachukuliwa
hatua na vyombo
vinavyohusika. Ninyi pia
msichoke kuwafichua, wapo miongoni mwa waumini
wenu.
Mabibi na Mabwana;
Kabla ya kumaliza,
napenda kumshukuru Waziri wa
Nishati na Madini,
Profesa Sospiter Muhongo na timu yake Wizarani kwa kushirikiana na
viongozi
wa dini katika jambo hili
muhimu. Naamini hatua hii ya kuwapa taarifa sahihi
viongozi wa dini
kuhusu matumizi ya
rasilimali zetu hususan
gesi na madini
itasaidia kuongeza uelewa
wa waumini wenu
na wananchi kwa
jumla.
Watafahamu fursa zilizopo na jinsi ya kuzitumia ili wafaidike
nazo. Nakushukuru
pia kwa kusimamia vizuri utekelezaji wa sera na mipango ya Serikali
katika sekta
ya nishati na madini. Kazi yenu
nzuri inaonekana na sisi wote ni mashahidi.
Mwisho, nawashukuru viongozi
wa dini kwa
kunishirikisha kwenye
Kongamano lenu. Naamini mkitoka
hapa mtakuwa mabalozi wazuri wa kueneza
ujumbe kuwa rasilimali za Watanzania zipo kwenye mikono salama.
Baada ya
kusema hayo, napenda kutamka kuwa Kongamano la Viongozi wa Dini
kujadili
matumizi ya rasilimali
zetu za gesi
asilia, mafuta na
madini kwa amani
na
maendeleo ya nchi yetu limefunguliwa rasmi. Nawatakia kila la heri na mafanikio
katika mwaka huu wa 2014.
Asanteni sana kwa kunisikiliza.
Subscribe to:
Posts (Atom)