Kesi ya bomoabomoa nyumba ya Mchungaji Rwakatare yasogezwa

Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi imeahirisha kusikiliza pingamizi la kesi ya kubomoa nyumba ya Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Mchungaji Dk. Getrude Rwakatare, dhidi ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) hadi  Desemba 10, mwaka huu.
 

Mchungaji Dk na MB wa Viti Maalum(CCM), Getrude Rwakatare

 Kesi hiyo namba 70 ya mwaka 2012, iliyofunguliwa ili kuizuia NEMC kubomoa nyumba hiyo ilitajwa juzi katika mahakama hiyo chini ya Jaji Hamisa Kalombola.
 
 Baada ya kusikilizwa kwa  kesi hiyo, Mwanasheria wa NEMC,  Manchare Heche, alisema  kesi hiyo imehairishwa ili pande zote mbili kuwasilisha hoja za mwisho kwa maandishi na baada ya hapo mahakama itatoa uamuzi.
 
“Kesi imehairishwa ili tuwasilishe hoja za mwisho kwa maandishi halafu baada ya hapo sasa mahakama itatoa uamuzi,” alisema Heche.
 
 Pingamizi ya Kesi hiyo ilifunguliwa na  Mbunge huyo kupinga NEMC kubomoa nyumba yake iliyojengwa kando ya mto Mbezi Beach eneo la Mndumbwe, jijini Dar es Salaam katika eneo la hifadhi ya mikoko

No comments:

Post a Comment