Upendo Kilahilo kuhudumu Tamasha la Pasaka Disemba

Upendo Kilahilo

Baada ya msanii Upendo Nkone kuthibitisha kushiriki Tamasha la Krismas litakalofanyika Desemba 25 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, msanii Upendo Kilahiro naye amejitosa kushiriki.

Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama alisema jana kuwa tayari wamefikia makubaliano na msanii huyo na wanafurahi kwamba tamasha litaenda vile wanavyotaka.
“Kilahiro tutakuwa naye, naamini mwaka huu tamasha hili litakuwa bora zaidi kutokana na kushirikisha waimbaji wengi wakali.

“Mpaka sasa Watanzania wawili tumeshakubaliana nao, yaani Kilahiro na Upendo Nkone,” alisema Msama na kuongeza kuwa bado wanaendelea na mazungumzo na wasanii wengine wa nje na ndani ya nchi.

Baadhi ya nyimbo za msanii huyo ni Zindonga alioimba kwa Kizulu), Unajibu Maombi na Ni Salama Rohoni. Pia anatamba na albamu mbalimbali ikiwemo Ficho Langu.

Tamasha la Krismas linaandaliwa na Kampuni ya Msama Promotion ya jijini Dar es Salaam, ambayo pia huandaa Tamasha la Pasaka kila mwaka.

Waandaaji hao wamepanga tamasha hilo lifanyike Desemba 25 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na siku inayofuata Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

No comments:

Post a Comment