Watoa Mil. 100 kulipia maisha baada kufariki

Kitendawili cha nini hatima ya maisha ya mwanadamu baada ya kufariki dunia, kinaendelea kuutesa ulimwengu wa wasomi tena waliotukuzwa kwa ubingwa wa kufikiri,safari hii kimewatatiza mabingwa wa falsafa  na utafiti wa maisha ya wanadamu katika Chuo Kikuu cha  Oxford, wakalazimika kulipa zaidi ya Milioni 100 ili miili yao itunzwe kitaalamu kwa kuwa wanaamini kuwa watarejea baadaye duniani.

Wasomi hao wakiongozwa na Profesa Nick Bostroma wamelazimika kutoa milioni 100, na kutia saini mkataba,na kampuni moja ili watakapokufa miili yao itunzwe kitaalamu hadi hapo roho zao zitakaporejea tena duniani.

Wataalamu hao katika utafiti wao wanadai kubaini bila shaka kuwa baada ya mwanadamu kufariki hukaa kwa muda na baadaye hurejea duniani na kuvaa miili kisha kuishi tena.Kwa sababu hiyo, walihofia kuwa kama watazikwa na miili yao kuoza basi watakaporejea wanaweza kujikuta katika miili ya ovyo na wakaishi maisha ya tofauti na walivyo sasa, jambo litakalowatesa na kuwanyima kufaidi uwezo walionao sasa.

Habari kutoka nchini humo zimeweka kuwa, tukio hilo la kwanza kufanywa na wabobevu wa elimu ya dunia, zimetokana na imani inayolenga kuwahakikishia wafu kurudi tena duniani, ingawa utafiti wao  unaokinzana na Biblia hauitaji kipindi cha marejeo ya miili.

Mbali na Profesa Nick Bostroma, ambaye pia ni Mkurugenzi wa taasisi inayojishughulisha na Maisha baada ya kifo, katika chuo hicho maarufu duniani, waliomuunga mkono ni wanataaluma wenzake ambao ni pamoja na  Anders Sandberg na Stuart Armstrong.

Prof. Bostman ametia sahihi mkataba wa kisheria  ili mwili wake uhifadhiwe kwa teknolojia maalum ambayo inahusisha kemikali zenye uwezo mkubwa wa kutunza miili isiharibike baada ya kufa,  huku Sandberg na Armstrong, wakisaini kuhifadhiwa kwa vichwa vyao pekee.

Wanaowadhihaki wanadai kuwa wamefanya hivyo kwa kuwa kwao vichwa vilivyonolewa vyema vyuoni, kuwa na maarifa mengi ndio vya thamani na sehemu zingine za miili wanaweza kuvaa vyovyote.Katika mikataba hiyo, wataalamu wameeleza kuwa, wakati wakisubiri kurejea tena duniani miili yao iwekwe kwenye kumbukumbu za kihistoria kwenye mji wa Michgani  ili vizazi  vijavyo viweze kubaini hali ya watu wa sasa.

Familia za wasomi hao wa falsafa zimeunga mkono mpango huo  wakiuelezea kuwa ni wenye heshima kubwa ndani ya jamii zao.Wataalamu wa kampuni iliyojitangaza kuwa na uwezo wa kuunda  mfumo wa kuhifadhi miili ya waliokufa, yenye makao yake katika Jimbo la Arizona, wanabainisha kuwa, wamekubaliana na hoja za wasomi hao na wamesema watavipulizia na kuvitunza vichwa hivyo kwa kemikali maalumu na kuwekwa katika eneo lenye baridi kwa manufaa ya vizazi vijavyo na tumaini la wahusika.

Profesa Bostrom kiongozi wa mpango huu ni miongoni mwa watu watukuka katika elimu ya falsafa akiwa tayari ametoa machapisho 200  yaliyozua mijadala  miongoni mwa wasomi na kumjengea heshima kubwa.
Miongoni mwa machapisho yake yaliyorejewa sana na wasomi katika mijadala ya kitaaluma ni Anthropic Bias (Routledge, 2002), Global Catastrophic Risks (ed. OUP, 2008), na Human Enhancement (ed.OUP, 2009). Kitabu chake kilichopo mbioni kuchapishwa kinachoitwa Super intelligence, kinasubiriwa kwa hamu huku vionjo vyake vikijikita kwenye imani ya wafu kurejea duniani.

Licha ya kujinyakulia tuzo ya (Eugene R. Gannon Award) inayotolewa kwa mtu mmoja anayechaguliwa kutoka duniani kote kutoka katika fani ya  Sanaa, Falsafa na hesabu katika  mwaka  2009, ametwajwa kuwa miongoni mwa mabingwa 100 wa kufikiri, wenye uwezo wa kutoa majibu ya yale yanayowatesa wengine.

Ni msomi ambaye amepata uwanja mpana wa kuzitambulisha kazi zake kupitia radio, magazeti na luninga, hivyo kuaminika sana na kujulikana katika ulimwengu wa waliosoma, hali inayowapa hofu wale wanaopinga imani yake ya kufa na kurejea baadaye kuvaa miili ya kibinadamu.

Kwa upande wake,Sandberg ni miongoni mwa watafiti kwenye taasisi hiyo ndani ya chuo cha Oxford, aliyejikita katika utafiti wa mustakabali wa sayansi na Teknolojia.

Bw.Anders ni mbobevu wa elimu ya Sayansi ya  Compyuta na uchunguzi wa ubongo wa mwanadamu na pia ni Injinia wa vifaa vya matibabu. Alipata shahada ya uzamivu  (Ph.D)  katika Chuo Kikuu cha Stockholm nchini Sweden,akijishughulisha haswa na mifumo ya kumbukumbu ya mwanadamu.

Dhana hiyo ya kuwa mwanadamu akifa atafufuka mwenyewe na kurejea tena duniani kuingia katika mwili inapingana na kweli ya Neno la Mungu  inayoeleza wazi kuwa baada ya mwanadamu kufa anasubiri kufufuliwa  na Bwana Yesu kwa ajili ya hukumu ya moto jehanamu kwa watenda dhambi na kuurithi  ufalme wa mbinguni kwa wale waliopokea wokovu.

No comments:

Post a Comment