Waimbaji Muziki na Waigizaji wazidi kuminika Kumrudia Mungu

Vincent Kigosi (Ray).
Siku za hivi karibuni kumetokea wimbi kubwa la waimbaji na waigizaji nje ya kanisa wa ndani na nje ya nchi kuamua kuachana na mambo waliyokuwa wakifanya kinyume na mapenzi ya Mungu na kuamua kurejea makanisani.

Hilo limedhihirika nchini kwa waimbaji na wanamuziki kumrudia muumba kama ilivyo huko nchini Malawi ambako tunaambiwa waimbaji wengi wameamua kurejea kanisani kumuimbia muumba wao kama lilivyoripoti gazeti la Nyasa Times kwamba waimbaji muziki zaidi ya watano wameokoka na kuamua kumwimbia Mungu wao huku wengine wakianzisha na bendi zao kabisa za gospel.

Kati ya waimbaji hao maarufu waliokoka ni pamoja na Sam Sambo, Mlaka Maliro, Phungu Joseph Nkasa, Bon Kavalasanza, Evans Meleka na wengine, ambapo wengi waliozungumza na gazeti hilo wameeleza ninamna gani walivyokutana na Mungu nakuamua kumkabidhi maisha yao.

Kwa upande wa Tanzania waimbaji na waigizaji ambao wameamua kumkabidhi maisha Yesu ni pamoja na Dotnata Posh ambaye ameshatoa wimbo wa gospel na sasa yupo katika masomo ya biblia na kuahidi kufungua kanisa pia aliweka bayana kwamba anampango wa kuwachukua mwimbaji Rehema Chalamila(Ray C), Aisha Madinda ambao amesema wameokoka kwasasa.

Wengine ni Stara Thomas ambaye pia tayari ametoa album ya gospel, wengine ambao walitangaza kuokoka miaka ya karibuni ni pamoja Vincent Kigosi (Ray), Mwanaidi Suka ( Mainda), K- Bazil ambaye kwasasa yupo mkoani Iringa kama mchungaji( kwa mujibu wa taarifa ambazo GK imezipata), Emanuel Mgaya a.k.a Masanja Mkandamizaji ambaye ndoto yake ya kuwa mchungaji amekwishaianza kwa kuhubiri katika mikutano mbalimbali pamoja na wengine wengi.

Swali ni kwa wale waliopo kanisani je wanapokeaje taarifa hizi za wapendwa hawa, je wanachukua jukumu la kuwaombea ama wanachukua jukumu la kuwahukumu?..


Stara Thomas.
Dotnata Posh

Aisha Madinda.    
Kashumba Bazil (K-Bazil).




Mwanaidi Suka (Mainda).


Source http://gospelkitaa.blogspot.com/                                                                                                                                                          
 

No comments:

Post a Comment