Wapiga kura kuchagua Mungu au shetani.

Wazazi wenye kufuata maadili wameingia katika hofu kubwa baada ya Mataifa ya Magharibi kuingia katika hatua mpya kupiga kura ya maoni ili kuidhinisha kila mwanafunzi hata wale wa shule ya msingi kufundishwa somo la ushoga na kuzuia haki ya mzazi kuamua mwanaye ajifunze nini?

Kura hiyo ya maoni imepitishwa ili kuunga mkono hukumu ya Mahakama moja ya Marekani iliyoamua kuwa Wazazi hawana haki ya kuhoji wala kuchagua vipindi ambavyo wanataka watoto wao wasome.

Wakati kura zikipigwa, tayari muelekeo unaonesha kuwa wapiga kura wengi watachagua upande wa ndoa za kishoga ambao ni wa shetani kwa kuwa jamii kubwa inaona mfumo huo ndio bora .

Waandaaji wa kura hiyo wanasema kuwa uhalalishwaji wa somo la ndoa za mashoga utaanza mara moja na somo hilo muhimu litafundishwa katika shule zote ikiwa ni pamoja na zile za kawaida (kata ) ambapo hakutokuwa na ridhaa kwa wazazi kuamua watoto wao wakae chini kufunzwa au laa.

Mchakato wa kura hizo unafanyika kupitia Luninga, na tangazo limetolewa likionesha vijana wawili waitwao  David na  Tonia Parker, ambao ni wachumba waishio  huko Massachusetts, eneo ambalo ndoa za mashoga hutambulika na kuheshimika kisheria.

Katika tangazo hilo, David anaonekana akisema hivi: “Baada ya Mahakama ya Massachusetts kutoa tafsiri ya ndoa, shule zetu zimekuwa zikifundisha watoto wetu, somo la ndoa linalogusia mambo ya ushoga ni la hatari kupita kiasi.”

Lakini mwenzake akisema: “Wazi kufunzwa ushoga ni haki yao kila mmarekani na lazima ufundishwe vyema kwa kila mtu, wazazi hawana haki ya kuingilia uhuru huo hasa katika faragha, waacheni waishi wanavyotaka.

katika hukumu ya Mahakama hiyo, ambayo  iligeuka mzigo mzito kama  gunia la misumari kwa wazazi wanaochukia mchezo mchafu wa ushoga, iliamriwa kuwa wazazi hawana haki ya kuwatoa watoto wao darasani wakati waalimu wakiwafundisha masomo ya ndoa yenye kuhusisha uhuru wa mtu kuwa shoga au kuwa na uhusiano na shoga.

Katika kupigilia rungu, mahakama hiyo pia iliamua kuwa Mwalimu au uongozi wa shule haulazimiki kumjulisha mzazi wakati mafunzo hayo yanapokwenda kufanyika.

Katika ufafanuzi wao kwenye tangazo la jimbo la Maryland, Tonia  alisema:
 "Ikiwa Somo la sita linalohusu ndoa za jinsia moja litafundishwa kwa lazima mashuleni ni vyema shule za Maryland zikajua kuwa zinapanda mbegu ambayo inawaathiri hata wao wenyewe.”

kura hiyo itatoa mwanga mpya wa kuamua kuidhinishwa kwa sheria ya ndoa ambapo wale wasiotaka kufungisha ndoa za watu wa jinsia moja au wanaojaribu kuwabagua wale waliochagua ndoa hizo watakumbana na mkono wa sheria.

Jimbo la Washington, nalo pia lipo mbioni kupiga kura ya kuamua ikiwa wahalalishe ndoa za mashoga au laa. Jimboni Minnesota, familia nyingi zimepingana na hoja hizo za kutaka wanafunzi wawe na somo la ndoa za mashoga, wao wanabainisha kwamba ndoa ni baina ya mwanamume na mwanamke na si vinginevyo.

Hata hivyo wakati hayo yakiendelea, Rais Barrack Obama ambaye amekuwa akiunga mkono suala zima na ndoa za mashoga aliruhusu mashoga waruhusiwe na kutambuliwa kuwa ni wanandoa.
"Rais amekuwa akitaka haki za watu wote zitambulike na kuheshimiwa.” hiyo ni kauli ya  msemaji wake kwa vyombo vya habari iliyokaririwa na Shirika la Habari la Reuters limeeleza.

Pande zote za malumbano katika Jimbo la Maryland, zimetaka waafrika na wamarekani kupiga kura ili kuamua ni njia ipi ya kushika kwa sasa.

No comments:

Post a Comment