The Drive Season One ndani ya Kanisa la City Harvest Jijini Dar es Salaam.


Timu ya ‘THE City Shakers’ kutoka Kanisa la City Harvest la jijini Dar es Salaam, imeandaa tukio maalumu linalotengeneza picha halisi ya ‘safari’  ya maisha ya wanavyuo tangu wanapodahiliwa vyuoni hadi siku ya mahafali. Tukio hilo linajulikana kama  The Drive Season One, likibainisha changamoto zilizo mbele yao na mbinu za kuzishinda.

Akiongea na na chanzo cha blog hii, kuhusiana na Safari hiyo, Mwenyekiti wa timu ya maandalizi, Bw. Augustine Chavala, alisema kuwa wanavyuo wengi mara wanapodahiliwa chuo wanajikuta katika makundi  ambayo mwisho wa siku huzima ndoto za maisha yao.

“Wanavyuo wengi kabla ya kujiunga na vyuo vikuu huwa na njozi mbalimbali, lakini makundi wanayojiingiza kwayo hupotoa kabisa ufahamu wao na wakizinduka miaka mitatu imefika wanaondoka kama walivyoingia,” alisema na kuongeza:

“Makundi huharibu maisha ya wanafunzi wengi, huanza kwenda klabu, hufeli mitihani, wengine huishia kufukuzwa vyuo na kuambukizwa magonjwa yasiyotibika, tunatarajia kufanya safari hiyo kuwaasa na kuwapa mbinu za kujihami.”

Dhumuni lingine la safari hiyo, Mwenyekiti Chavala alibainisha kuwa ni kuonyesha upendo kwa wanavyuo hao na kuwadhihirishia kwamba ni wa muhimu sana mbele ya jamii inayowazunguka.

“Tunaomba wanafunzi wengi wajitokeze siku hiyo (Ijumaa ijayo tarehe 23) kuanzia saa tatu usiku, pale City Harvest, Mabibo Garage, karibu na Victoria Petrol Station,” alisema na kuongeza:

Usiku huo utapambwa na team nzima ya The City Shakers, World alive, ambapo wanavyuo watapata wasaa wa kucheza muziki kuona Sarakasi, maigizo, Vichekesho, filamu na vitu vingine vingi.

No comments:

Post a Comment