Hezbollah kushambulia Galilaya, wasema ndicho kiini cha silaha.

"Vita ijayo baina yetu na Israeli itakuwa pana zaidi na makombora yetu yataelekezwa kwenye mji wa Galilaya ambao ni kiungo muhimu cha miundombinu ya kijeshi, baina ya kambi kubwa na maeneo ya kiulinzi ya milima ya Golani,”alikaririwa akisema Bw. Benedetta Berti. Mmoja wa wasemaji wa Hizbollah.

Kiongozi mwingine wa wa Hezbollah, Sayyed Hassan Nasrallah anaelezwa kwamba amekuwa akisikika akiongelea namna ya kujiimarisha kwa vita ijayo mara baada ya vita ya mwisho ya mwaka 2006 ambayo hawakufanya vizuri,  lakini sasa wanakwenda kufanya vizuri zaidi.

Amekuwa akitoa maelekezo juu ya rockets katika milima ya Golan na wanajitahidi kutengeneza mipango kamilifu na sasa wana nguvu zaidi za kupambana safari hii.

Mkurugenzi mtendaji wa kundi la mijadala ya Mashariki ya Kati,  Daniel Pipes alisema kuwa  anaamini maneno yao yanayosikika ni zaidi ya hatari.

Baadaye katika taarifa kwenye mtandao alisema: “hiyo itakuwa mara ya pili kwetu kuulenga mji wa Galilaya, wakati wa vita na Lebanon tulijaribu kufanya hivyo lakini hatukupata mafanikio makubwa, safari hii hatuna mdhaha,”alisema Hassan Nasrallah. 

Alisema kinachoonesha kuwa Israeli haina nia ya kujenga nyumba za walowezi wa ki- Yahudi kusini mwa Labanon katika mpaka ambao mikataba ya nyuma ilionesha kuwa haipaswi kuendelea kusogelewa.

Mchambuzi wa mambo ya kivita Berti, alisema kuwa  inawezekana kuwa kutumwa kwa utisho huo kwenye mtandao ni kama kujaribu kuitisha Israeli kisaikolojia ilikuwa kama ikianzisha mashambulizi haitasalia salama.

 “Ni vyema sasa tukatenganisha propaganda za kivita na uhalisia wa mambo. Propaganda za kivita zimekuwepo tangu mwaka 2006,” alisema Berti na kuongeza:
“Ninachomaanisha hapa ni kuwa hatakama Hizbollar watashambulia na kuchukua mji wa Galilaya, bado hawawezi kujivunia kulitikisa jeshi lenye nguvu la Israeli.”

 Alisema kuwa tangu mwaka 2006, Hizbollar walijifunza mbinu mpya ya vita vya maneno badala ya halisia, kila wakishambulia kidogo hupaza sauti na kuongeza ukubwa wa madhara ya mashambulio yao.

Lakini Mkurugenzi wa zamani wa shirika la ujasusi la  Israeli Mossad, Meir Dagan, alionya kuwa kundi la Hizbbollar limejijenga vya kutosha na haipaswi kubezwa kwani mwanzoni mwa mwezi Oktoba ilirusha ndege ya upelelezi isiyo na rubani ambayo ilinaswa na rada za Israeli na kuangushwa.

No comments:

Post a Comment