Usiku wa Tanzania Praise and Worship Team.

Ulikuwa ni usiku wa watofauti katika wa kusapoti maono Mungu aliyoyaweka kwa mtumishi wake Bwana Paul Mwangosi, Paul Mwangosi alipata maono ya umuhimu wa kumsifu na kumwabudu Mungu aliye hai mnamo mwaka 2008.Mwaka huo ikiwa mjini mwanza Mungu alisema naye  kuwa hajapata Heshima ya kutosha ile hali miungu isiyo hai ikiheshimiwa

Mnano mwaka 2011,Mungu aliachilia kibali cha kufanya mkesha kwa ajili ya kumsifu na kumwabudu.Mwaka huu ndipo Bwana Paul Mwangosi alipo washilikisha ndugu katika Kristo kuhusu maono haya ambao waliunda kamati ya kuandaa Mkesha wa Kumsifu na Kumwabudu Mungu aliye Hai.Kamati kwasasa ndio inayojulikana kama ya Tanzania Praise and Worship  Team,

Mkesha wa Kumsifu na Kumwabudu Mungu kwa mwaka jana katika Kanisa City Christian Centre Upanga (CCC).

Dhima ya ya Tanzania Praise and Worship  Team ni kutoa fursa kwa ajili ya watu wote kwa pamoja pasipo kujali tofauti za kidhehebu,kisiasa na kiuchumi Kumsifu na Kumwabudu Mungu kwa ajili ya Taifa la Tanzania.

Madhumuni ya Tanzania Praise and Worship  Team Kuandaa,kuhamasisha na Kuratibu Mkesha/Mikesha ya Kitaifa kwa kumsifu na Kumwabudu Mungu

Mkesha wa Kumsifu na Kumwabudu Mungu mwaka huu utafanyika tarehe 07/12/2012 katika Kanisa City Christian Centre Upanga (CCC)

Ilikufanikisha mkesha huu zinahitaika sh.Mill 18, Katika usiku wa Ibada ya jana zilipatatikana jumla ya sh.Millioni 4,642,000/ zilizopatikana tasirimu ni ash.mill 1,199,000/=


 Tanzania Praise and Worship Team madhabahuni wakihudumu katika usiku wa jana
















No comments:

Post a Comment