Askofu.Dr Moses Kulola Baba wa Wengi afariki Dunia



Msiba huo wa umetokea  leo muda wa saa 5 asubuhi  katika hospitali ya AMI (African Medical Investments) iliyopo Slipway jijini Dar es Salaam,Msiba huo umetokiea kama mwezi mmoja baada ya Askofu Kulola kutoka Nchi India alikuwa ameenda kutibiwa ugonjwa uliokuwa unamsumbua.

Alipio kuwa nchini India kwa matibabu hali yake kiafya alipata nafuu ndio akawa amerejea nyumbani Alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa ini na moyo.

Msiba kwa sasa uko Kanisa la EAGT Temeke na kusuburi utaratibu mwingine wa Kanisa la EAGT kwa siku ya Jumamosi saa 2 asubuhi kanisani hapo ili kuweza kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Askofu Kulola baada ya hapo kuwa tayari kuelekea Jijini mwanza kwa mazishi alipo agiza mwenyewe azikwe,Ndugu,jamaa na washirika wako Kanisani EAGT Temeke

Bwana alitoa Bwana emtwaa,Jina lake lihimidiwe.
Source:Willy  Kulola

Historia ya Askofu .Dr Moses Kulola kwa ufupi.
Alizaliwa mwezi Juni 1928 katika familia ya watoto kumi na kufariki mwezi Agosti 2013 katika hospitali ya AMI (African Medical Investments) iliyopo Slipway jijini Dar es Salaam. Alisomea shule ya msingi ya Ligsha Sukuma, halafu taasisi ya usanifu. Alibatizwa kikristo mwaka 1950 katika Kanisa la AIC Makongoro. Alimwoa Elizabeth wakawa na watoto kumi.

Alifanya kazi ya uchungaji wa kanisa la AIC miaka ya 1961-1962 akaendelea na masomo ya kitheolojia. Baada ya kujiunga na dhehebu la kipentekoste alifanya kazi ya uchungaji ndani ya kanisa la TAG miaka ya 1966-1991. Akajitenga na kanisa hilo na kuanzisha kanisa jipya mwaka wa 1991, kanisa la EAGT (kwa Kiingereza Evangelistic Assemblies of God) akawa askofu wao wa kwanza tangu mwaka uleule.
Source: wikipedia

No comments:

Post a Comment