Askofu,Dr Moses Kulola aagwa na wakazi wa Jiji la Mwanza siku ya jana.


Wakazi wa Jiji la Mwanza siku ya Jana wa lijitokeza kwa wingi katika uwanja wa CCM Kirumba  katika katika kumuaga Babu Askofu,Dr Moses Kulola kabla ya mazishi yake siku ya leo katika Kanisa la EAGT Bugando

Shughuli hiyo iliudhuliwa na viongozi mbalimbali wa Kikristo na Serikali kwa ujumla,siku ya jana serikali iliwakilishwa na mkuu wa mkoa wa Mwanza Injinia Evarist Ndikilo kwa kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Askofu Dr. Moses Kulola.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Dr Jakaya Kikwete anategemea kuhusika katika ibada ya mazishi siku ya leo akiwa ameongoozana na viongozi wengine wa Serikali,Ibada hiyo inategemewa kuanza saa 3:00 asubuhi hadi saa 7:00 mchana.


Mch. Dastan Mboya akieleza namna alivyomfahamu Askofu Mosses Kulola

Mkuu wa mkoa wa Mwanza Injinia Evarist Ndikilo akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Askofu Dr. Moses Kulola

Mwili wa Marehemu ukiwa Uwanja wa CCM Kirumba tayari kwa watu kuaga


Ndugu wa marehemu wakiwa katika hali ya majonzi wakati wa kuaga mwili wa marehemu CCM Kirumba Mwanza.

No comments:

Post a Comment