Living Water Center Yaiteka Shinyanga

Huduma ya Living Water Centre Ministry chini ya mtumishi wa Mungu Apostle Onesmo Ndegi yenye makao yake makuu Kawe Jijini Dar es salaam wikiendi iliyokwisha ilikuwa ikihitimisha Mkutano wa Injili katika Kanisa lake Mkoani shinyanga. 

 Semina hiyo ilidumu wa siku 5 na Apostle Ndegi aliye likaribishwa na Mwenyeji wake Mch.Nazareth Manase wa Living Water Centre Shinyanga, Mkutano huo ulio uliohudhuliwa na watu wengi kutoka katika kila kona za mji wa shinyanga kuja kusikiliza Neno la Mungu.  

   Katika Mkutano huo waimbaji wa Nyimbo za Injili kama Bahati Bukuku,Mwanakondoo Kwaya wenyeji,St.Joseph Kwaya RC,Gosheni kwaya toka Mwanza na Emmanuel Mganya maarufu kama Masanja Mkandamizaji alikuwepo kuhudumu, kitu kilichotokea kuhusu uwepo wa Masanja Mkandamizaji ni pale watu walikuja kwa wingi kumwona Masanja lakini ndipo mahala Bwana Yesu alipo wakamatia na Kumpa maisha yao kuokoka.  

   Kwa siku tano za mkutano huo waliokoka watu wengi wadogo kwa wakubwa, wake kwa waume  Pia maombezi na ushauri vilifanyika katika wale waliokuwa wanahitaji msaada zaidi maana ilionekana kwa asilimia kubwa watu wengi wamevamiwa na nguvu za giza hasahasa watoto wadogo  

  Kitu ambacho kimeonekana mkoani ni kuwa watu wanauhitaji na kiu na Mungu sana maana wanasumbuliwa na mambo mengi ya kishirikina na mapepo,hivyo naomba kuwatia moyo na kuwapa changamoto watumishi wenye huduma mijini au wanaotaka kufungua huduma






Add caption









No comments:

Post a Comment