Maaskofu wakataa ushoga Uingereza

Maaskofu wakuu nchini Uingereza wamewaambia viongozi wa dini kwamba hawataruhusiwa kuingia katika ndoa za jinsia moja.

Pia walisema kwamba hawatakubali kuona viongozi wa dini kwenda kinyume na maagizo hayo nchini humo.
Viongozi wa dini wa kanisa la Ki-Anglikana wanakubaliwa na kanisa hilo kuingia katika uhusiano wa kimapenzi lakini kwa maelewano kwamba hawatashiriki ngono.
Katika mwelekeo wao, maaskofu hao pia walipiga marufuku maombi yoyote maalumu kwa wanandoa wa jinsia moja licha ya ripoti rasmi ya kanisa hilo kupendekeza kwamba viongozi wa dini wanaweza kufanya hivyo iwapo wanajihisi.
Hata hivyo walidai viongozi wa dini wanapaswa kutoa maombi yasiyo rasmi kwa wanandoa walio katika uhusiano wa jinsia moja.
Uganda
Kwa upande wa Rais Yoweri Museveni wa Uganda alisema atasaini muswaada tata unaopinga ushoga na kuwa sheria kamili.Hatua hiyo inaelezwa kuwa ni onyo kwa wanaotetea vitendo vya mahusiano ya jinsia moja kuwa watashughulikiwa vikali nchini humo.
Mwezi uliopita kiongozi huyo alipanga kuachana na mswada huo ambao umekuwa ukikosolewa vikali na wahisani kutoka mataifa ya Magharibi na wanaharakati wa haki za binaadamu tangu ulipowasilishwa mwaka 2009.Mapenzi ya jinsia moja ni mwiko katika mataifa ya Afrika na kinyume cha sheria kwa mataifa 37.
Wasiwasi wa mashoga wa Afrika
Wanaharakati wa haki za binaadamu wanasema Waafrika wachache waliojitangaza kuwa mashoga, wanahofu ya kufungwa, kukabiliwa na vurugu na kupoteza ajira zao.

Source:Mwananchi

No comments:

Post a Comment