Jukwaa wa Wakristo Tanzania lamtaka JK kutoa msimamo wa kisheria kwa Uislamu,Ukristo

Jukwaa wa Wakristo Tanzania limemtaka Rais Jakaya Kikwete kutoa msimamo wake kisheria ambao utaleta upatanisho kati ya waumini wa dini ya Kiislamu na Kikristo.

Jukwaa hilo limesema kauli iliyotolewa na rais juzi wakati wa sherehe za Mei Mosi, Mbeya ya kutaka Watanzania waishi kama zamani ina utata kwa sababu imetafsiriwa tofauti na baadhi ya Watanzania.

Hivi karibuni Rais Kikwete wakati akizungumza kwenye sherehe za Mei Mosi alisema Serikali bado inaendelea kuzungumza na viongozi wa dini wa pande zote na kuwaunganisha ili kuona maelewano yanarejea kama ilivyokuwa zamani na kuwataka Watanzania waendelee kuishi bila kubaguana au kuchukiana kwa dini zao.

Akizungumza jana, Mwenyekiti wa jukwaa hilo, Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa ambaye pia ni Rais wa Baraza la Maaskofu wa Kikatoli Tanzania (TEC), alisema licha ya maneno hayo kuwa mazuri lakini bado kuna utata kwa sababu baadhi ya raia wameingiwa na wasiwasi.

Alisema maeneo mengine wakristo hawali nyama kwa sababu hawataki kulazimishwa kula nyama zilizochinjwa kwa ibada za kiislamu na kwamba suala hilo siyo dogo kama wengine wanavyofikiri kwa sababu limegharimu maisha ya watu.

Alisema licha ya kuwapo kwa kauli za uchochezi wa kuwaua viongozi wa dini ya kikristo,kuchoma makanisa na mauaji ya viongozi wa kikristo bado hazijafutwa wala waliozitoa hawajakamatwa na kwamba hawajui kinachoendelea.

Mwenyekiti huyo alisema madai ya msingi ya waislamu yaliyosababisha waanzishe vurugu na mauaji hayajajibiwa na Serikali huku maswali yaliyoulizwa na wakristo kutokana na madai hayo na vurugu hizo nayo yakiwa hajayajibiwa.

Alisema licha ya kukutana na Rais Kikwete Aprili 23, mwaka huu ambaye alihimiza viongozi wa wakristo na waislamu wakutane ili kuondoa tofauti zao zisizo za kiimani lakini bado wanasubiri maelekezo toka serikalini kwani ajenda ya uvunjifu wa amani viongozi wa dini hawawezi kuizungumzia kwa sasa bila majibu ya Serikali kwa madai yaliyozua uvunjifu huo wa amani.

Allen Mwamwaja na Uzinduzi wa Album ndani ya Kijitonyama













Kiingilio ni Bure

AFLEWO TANZANIA 2013 YAFANA

Mkesha Mkubwa Tanzania wa Kusifu na Kuabudu AFLEWO (Africa Lets Worship) umefanyika vizuri katika kanisa la BCIC likiudhuliwa  na Maelfu ya watu kutoka maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es salaam na Mikoa ya Jirani kama Moshi,Mwanza na Mingine,

Mkesha wa AFLEWO ulifunguliwa kwa Maombi na Askofu Silvester Gamanywa wa Wapo Mission International akifungua kwa maombi na kuwa ameufungua rasmi ukianza Kwa sifa na Kuabudu.

Watumishi wa Mungu kutoka Makanisa Mbalimbali walikuwepo katika Mkesha huo kuhakikisha wanaumuika na Kufanya kitu kimoja kwa ajili ya mwili wa Kristo katika Taifa la Tanzania.

Bishop Silvester Gamanywa wa Wapo Mission International akifungua Mkesha wa AFLEWO kwa maombi.BCIC Mbezi Beach
Pastor Ferdie Kyara akihubiri Neno katika Mkesha wa AFLEWO TANZANIA


Fullshangwe....


Pastor Gal with Kagaruki






AFLEWO Patron Pastor Abel Orgenes
Tanzania Shall never Be the Same,,,,







Majembe ya Bwana Ma MC wa Event

Praise Team Kutoka Moshi


Dance
The Voice



AFLEWO Tanzania kuomba kwa ajili ya Viongozi wa Serikali na Dini

Katika kuelekea Mkesha Mkubwa wa AFLEWO Tanzania ikiwa imebaki siku moja kufanyika Baadhi ya viongozi wamezungumza mbele ya waandishi wa habari kuhusianana Mkesha huo pale DPC Kinondoni.

 Maandalizi yamekamilika kwa asilimia 90 mpaka sasa kuanzi Mass Choir hadi mambo mengine,hivyo kilicho baki ni kuanza Mkesha huo Kesho saa 3:00 kamili usiku BCIC Mbezi Beach
(Kituo cha Jogooo) katika kanisa la Bishop Gamanywa wa Wapo Mission International 

Katika Mkesha huo kunategemewa kuwa na wageni kutoka Nchi za jirani na mikoa ya jirani kama Mwanza,Moshi,Arusha na mahala pengine nje ya Jiji la Dar es salaam.

Mkesha Mkubwa wa AFLEWO utakuwa na kusifu na Kuabudu na Maombi kwa Taifa na Viongozi wa Nchi pia kuomba kwa ajili ya Viongozi wa Dini zote ukizingatia kama Taifa tunapitia katika changamoto na tofauti za kidini,hivyo tuna hitaji kwenda mbele za Mungu kwa mambio katika Mkesha wa AFLEWO Tanzania,Alisema hayo Pastor Fredie Kyara alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

Walio Pichani Kushoto ni Samuel Sasali, Mkurugenzi wa Habari Aflewo, Bishop Freddie Japhet Kyara Mlezi Wa Aflewo Tanzania, Pastor Paul Safari Mlezi wa Aflewo Tanzania, Samuel Rodin Mwangati Music Director wa Aflewo.


 Bishop Freddie Japhet Kyara Mlezi Wa Aflewo Tanzania akizungumza na waandishi wa kwa msisitizo na kuhusu Mkesha huo
Samuel Sasali, Mkurugenzi wa Habari Aflewo, Bishop Freddie Japhet Kyara Mlezi Wa Aflewo Tanzania, Pastor Paul Safari Mlezi wa Aflewo Tanzania, Samuel Rodin Mwangati Music Director wa Aflewo.

Serikali kutunga sheria kudhibiti uhalifu mtandaoni

Serikali inatarajia kuwasilisha bungeni,muswada wa sheria itakayodhibiti na kulinda taarifa za watu binafsi wanapowasiliana kwa simu za mkononi na kwenye intaneti.

Akifungua mkutano wa mwaka wa benki na wadau wa kupambana na uhalifu kwa kutumia mitandao, Mkurugenzi wa Teknolojia wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Dk Zaipuna Yonah, alisema kuwapo kwa sheria hiyo kutasaidia kuzuia watu kufuatilia mawasiliano binafsi katika mitandao ya simu na hata mawasiliano ya njia ya baruapepe.

Hivi karibuni kumekuwa na matukio kadhaa ya watu kuweka hadharani na hata kuchapisha mawasiliano ya watukatika magazeti na mitandao ya kijamii, kitendo ambacho kimelalamikiwa.

Miswada inayoandaliwa ni pamoja na sheria ya kulinda mawasiliano ya mtu binafsi, sheria ya kusimamia uhamishaji wa fedha kwa njia ya simu na sheria ya kushughulikia wale wanaofanya uhalifu kwa kutumia kompyuta.

Yonah alisema wanataka kuona sheria hizo zikipitishwa katika kipindi cha mwaka mmoja.
“Mapendekezo haya, hata hivyo, yana changamoto zake kwa kuwa sheria hizo zinaingiliana na utendaji wa vyombo vya habari.

“Kuna tatizo kwa kuwa unavyotaka kuzuia habari, vyombo vya habari navyo vinataka habari,” aliongeza.

Alisema mbali na kupendekeza kuwapo kwa sheria zitakazoratibu huduma ya mitandao nchini, Serikali pia inatarajia kuunda chombo kitakachokuwa kikisimamia watoa huduma wa mitandao kwa kuwapa vyeti vya utambuzi wa kazi zao.

“Tunatarajia kuwa na timu ya wataalamu wa kompyuta ambao watakuwa wanashughulikia iwapo kuna matatizo ya uhalifu wa kimtandao,” alisema.

Dk Yonah alisema Serikali imechukua hatua hizo kutokana na kupokea malalamiko mengi ya watu walioathirika na uhalifu wanaofanyiwa kupitia kwenye mitandao ya kompyuta.

Pia katika siku za karibuni kumejitokeza tatizo la wizi kwa njia ya ATM na hata kwenye uhamishaji fedha kwa njia ya simu za mikononi.

Akizungumzia mada juu ya mwelekeo wa malipo kwa njia ya teknolojia kwenye masoko yanayochipukia, Makamu wa Rais wa VeriFone kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati, Martin Holloway, alisema asilimia 10 ya watu wa eneo hili wanamiliki akaunti za benki wakati asilimia 60 wanamiliki simu za mkononi hivyo yanahitajika marekebisho ya haraka katika kudhibiti uhamishaji holela wa fedha kwa njia ya mtandao.

Alisema kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Taasisi ya Data Breach ya mwaka 2011, asilimia 78 ya uhalifu uliofanyika duniani kote ulihusu kuhamisha malipo kwa njia ya kompyuta au kwa njia ya simu za mikononi

Rais Kikwete awaongoza watanzania Katika Maadhimisho ya Miaka 49 ya Muungano










Makanisa matatu yavamiwa Kilimanjaro

Watu wasiojulikana wamevamia makanisa matatu mkoani Kilimanjaro na kuvunja milango, kuharibu mali mbalimbali zikiwemo kompyuta na samani za kanisa na kuiba fedha.

Tukio hilo limetokea katika jimbo la Kilimanjaro Mashariki, Dayosisi ya Kaskazini, Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT).

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Mkuu wa jimbo hilo, Mchungaji Winford Mosha, alisema kuwa tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia jana.

Mosha aliyataja makanisa yaliyovunjwa kuwa ni usharika wa Kimbowo, Mseroe  na Mrienyi na kwamba watu hao walivunja kwa lengo la kutafuta fedha.

Mchungaji Mosha, alisema katika usharika wa Mseroe watu hao waliiba shilingi laki mbili na katika sharika nyingine waliharibu mali za kanisa na kuondoka baada ya kukosa vitu vya kuiba.

Hata hivyo, Mosha alisema tukio hilo ni mfululizo wa matukio ya wizi yaliyotokea mwanzoni mwa mwezi huu katika jimbo hilo ambapo makanisa mengine matatu yalivunjwa na mali zake kuharibiwa vibaya.

Aliongeza kuwa makanisa ambayo yaliyovunjwa ni Msae, Kiruweni na Ashira, hata hivyo katika matukio hayo, pia wezi hao walifanya  uharibifu wa mali mbalimbali za makanisa na kuiba fedha.

Kufuatia tukio hilo, mchungaji huyo aliwataka wakristo pamoja na wachungaji kusimama imara katika maombi ili kuimarisha ulinzi katika maeneo ya makanisa katika kipindi hiki cha sikukuu.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz, alisema watu hao waliovunja makanisa hayo walikuwa na lengo la kuiba na si vinginevyo.

Maaskofu waijia juu Serikali

Wakristo wamesema Serikali ya Rais Jakaya Kikwete imeshindwa kuwasaidia ili waishi kwa amani na utulivu katika nchi yao.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Dodoma, Amon Kinyunyu, wakati akisoma tamko la Maaskofu wa madhehebu ya Kikristo Tanzania katika ibada ya Ijumaa Kuu iliyofanyika katika Kanisa lililopo eneo la Jamatini.
Katika tamko hilo alilolisoma kwa niaba ya Maaskofu wote, Kinyunyu alisema kuwa umefika wakati ambao Wakristo wamechoka na vitendo wanavyofanyiwa na baadhi ya waumini wa dini zingine.

“Tatizo ni kuwa Serikali inashindwa kuchukua hatua mapema, makanisa yanachomwa, migogoro inazidi, lakini hakuna hatua zozote ambazo Serikali inachukua katika kunusuru hali hiyo, tumechoka,” alisema.
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Dodoma, Amon Kinyunyu 
“ Serikali imeshindwa kuchukua hatua kwa muda mwafaka kwa kila jambo ambalo linatokea kwa Wakristo na hata inapoonyesha kuwa imechukua hatua haionyeshi sana kujali juu ya yale wanayofanyiwa Wakristo. Askofu huyo alisema kuwa matokeo yanayotokea Zanzibar mathalan, Wakristo wanaoishi huko yamewasababishia hofu hivyo wengi kuanza kuvikimbia visiwa hivyo na kukimbilia Tanzania Bara.

Kwa mujibu wa Askofu Kinyunyu, suala la uchomaji wa makanisa hadi sasa limeshindwa kupatiwa ufumbuzi na kila kukicha bado makanisa yanaendelea kuchomwa moto akahoji Serikali kukaa kimya maana yake nini.
Aidha, tamko hilo limeitaka Serikali kuweka utaratibu mzuri na ufafanuzi wa kina kuhusu uchinjaji wa nyama ambao umekuwa ni tatizo kubwa hapa nchini. “Hapa litolewe tamko kila mtu kwa imani yake achinje mwenyewe siyo kuanza kulaumiana au kumpa haki mmoja akachinja na mwingine akaachwa. Tunaomba sana ufafanuzi wa kina juu ya suala hilo ili kuondoa mgogoro baina yetu na wenzetu.”
wamekuwa wakifanyiwa, lakini akasisitiza kuwa wanatakiwa kupigana kwa maombi na ndiyo silaha kubwa ya ushindi.

Katika hatua nyingine, wakati Wakristo wakiwa na hofu ya kusherehekea Sikukuu ya Pasaka watu wasiofahamika wamevamia makanisa matatu ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Dayosisi ya Kaskazini na kuvunja ofisi za wachungaji na wainjilisti.