The Nextlevel; uzinduzi wa Album ulivyofana ndani ya CCC Upanga



Baada ya maandalizi ya muda mrefu katika kuandaa Album ya kundi la The Nextlevel lenye kujumisha maimbaji kutoka makanisa mbalimbali siku ya jana lilikuwa likizindua Album yake kwa kuiweka wakfu mbele za Mungu. 

Tukio hilo lililoudhuliwa na wakristo mbalibali kutoka sehemu mbalimbali za  Jiji la Dar es salaam pia watumishi wa Mungu  kutoka makanisa mbalimbali waliweza kuhudhulia uzinduzi huo katika kanisa la City Christian Centre.

Kundi hilo la the nextlevel linaloongozwa na Muongozaji wa muziki Nchini maarufu Samuel Mwangati  akishirikiana na viongozi wenzae katika kuifanikisha hudumai hiyo,nikizungumza na Administator wa kundi la nextlevel  alisema “tunamshukuru Mungu kwa hatua hii maana ametuwazesha tangu tunaanza kurekodi Album,maandalizi ya kuzindua hadi siku ya leo kuzindua ” alisea Neema Administator wa kundi la nextlevel.

Kundi la nextlevel wanategemea kurekodi DVD ya Album waliyozindua mwezi Desemba kanisani hapo City Christian Centre, taharifa tulizonazo ni kwamba maandalizi yanaada mapema ikiwa ni katika kutaka kurekodo Album yenye ubora na kiwango yenye kuleta utukufu kwa Mungu.





















No comments:

Post a Comment