Kanisa La FGBF Lamfanyia Maombi Mbunge Deo Filikunjombe

SIKU moja baada ya mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe kupokelewa jimboni na wapiga kura wake kama mfalme Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship(F.G.B.F) linaloongoza na askofu Zacharia Kakobe wilayani Ludewa lamfanyia maombi maalum .

Huku mwenyewe akiahidi kuendelea kupambana na Vitendo vya ufisadi kwa Taifa bila kuogopa na kuwaomba Waumini wa Kanisa hilo na madhehebu mengine pamoja na wapiga kura wake wote kuzidi kumwombea zaidi Kwani kazi iliyopo mbele yake ya kupambana na ufisadi ni nzito yahitaji maombi.Kanisa hilo limfanyia mbunge Filikunjombe maombi hayo jana katika ibada maalum ambayo iliandaliwa na uongozi wa Kanisa hilo kama njia ya kuungana na vyama vya siasa na wananchi wa jimbo hilo kuutambua mchango na kazi nzito ya mbunge huyo katika kupambana na vitendo vya ufisadi nchini.

Katika maombi idaba hiyo Mchungaji wa Kanisa hilo Faustin Sambilanda.alisema kuwa kazi ilinayofanywa na Filikunjombe katika kulipigania Taifa ni kubwa na hivyo kila mtanzania na kila kiongozi wa dini wanaowajibu wa kuendelea kumwombea mbunge huyo na wengine ambao wapo kwa maslahi ya watanzania .


Alisema kuwa uamuzi wa mbunge Filikunjombe kuwemo katika orodha ya wabunge wasio na imani na waziri mkuu Mizengo Pinda na kupelekea Rais Jakaya Kikwete kubadili baraza baraza lake na mawaziri na kuwaondoa wale waliotuhumiwa kwa ufisadi si jambo dongo na kuwa wananchi wa Ludewa wanaungana na watanzania katika kuunga mkono uamuzi wa wabunge wapambanaji wa ufisadi akiwemo Filikunjombe.Hata hivyo alisema wanaweka utaratibu wa kuendelea kumfanyia maombi maalum kwa ajili ya kazi nzito anayoifanya ambayo silaha pekee ni maombi na si vinginevyo .
                                               Filikunjombe akiombewa Siku Ya Leo.

Kwa upande wake mbunge Filikunjombe mbali ya kuupongeza uongozi wa kanisa hilo la )F.G.B.F) kwa kuutambua mchango wake katika Taifa bado alisema kuwa anatambua kazi nzuri inayofanywa na viongozi wa dini katika jimbo hilo na kuwa yeye ni kiongozi wa makanisa na misikiti yote katika jimbo hilo.Alisema yeye ni mbunge wa wote na wakati wote atawatumikia bila kuwabagua hivyo wakati wote ataendelea kuwakutanisha Waumini na wananchi wote bila kuwabagua .


Mbunge Filikunjombe alisema kuwa matumaini yake ni kuona yeye na wananchi wake wataendelea kushirikiana na kuwa yeye alitakiwa kuwa Paroko kutokana na awali kujikita zaidi kusomea uparoko ila sasa amekuwa mwanasiasa.Japo alisema kuwa kazi zote ni za kijamii na kuwa siku zote amekuwa akiwaombea wanananchi wake wa Ludewa na kuwa lazima na wao wazidi kumwombea ili kuendelea kuifanya kazi hiyo kwa kuongozwa na Mungu.

No comments:

Post a Comment