Rebecca Malope ndani ya Uwanja wa taifa Tamasha la Pasaka!


RebeccaMalope akijulikana kama Malkia wa muziki wa injili Africa amezaliwa 1968 katika kijiji cha Lekazi karibu na mji wa Nelsprut, Mpumalanga. Malope hakuendelea sana katika elimu na ni mambo machache sana yanafahamika kuhusiana na enzi za utoto wako. Akiwa katika umri mdogo Malope alipata ugonjwa uliopelekea kutoweza kutembea na madaktari walidhani asingeweza kutembea tena katika maisha yake.
Familia yake ilikuwa masikini sana na ndipo yeye na dada yake(Cynthia) waliamua kumbilia katika jiji la Johannesburg kitongoji cha Evaton kwa ajili ya kutafuta kazi kujikimu na maisha.
Mwaka 1986,Malope alishirika kwenye mashindano ya kutafuta vipaji vya uimbaji “Shell Road to Fame,(Music talent search) lakini hakufanikiwa kufika mbali. Malope hakukata tamaa ndipo mwaka uliofuata alishiriki tena na kuibuka mshindi(Best Vocalist) na wimbo Shine on. Ushindi huu ulimsogeza mbali sana kimuziki na ndipo alipokutanishwa na muandaaji(producer) mashuhuri Sizwe Zako na akapata meneja wake wa kwanza akijulikana kwa jina la Peter Tladi.
Dr. Rebecca Malope
Album yake ya kwanza  ilikuwa na nyimbo za kawaida za kijamii,album haikufanya vizuri sokoni na ndipo alipoamua kujiingiza moja kwa moja kwenye muziki wa injili. Alipata sapoti kubwa sana kutoka katika radio mbalimbali kwa nyimbo zake za gospel kitu ambacho hakikuwa kawaida sana Africa Kusini.
Mwaka 1990 Rebecca alishinda tuzo ya mwanamuziki bora wa kike wa Afrika Kusini,na mwaka 1993 ilikadiriwa watu zaidi ya milioni moja walimpigia kura kama mwanamuziki bora wa kike kwenye Coca Cola Full Blast Music Award Music Show, na alishinda kwa mwaka huo na 1994 pia. Kwenye mauzo, Album zake zote kumi za kwanza ziliingia kwenye hadhi ya dhahabu(gold). Katika kipindi hiki kopi zaidi ya milioni 2 zilikuwa zimeshauzwa sokoni. Mwaka 1995 kwenye CD yake ya Shwele Baba, kopi zadi ya milioni moja zilikuwa zimeshauzwa ndani ya wiki tatu toka uzinduzi wake,na hii iliweka rekodi ya aina yake katika historia ya soko la muziki Africa kusini.
Dr. Rebecca Malope
Mwaka 1996 haukuwa mwaka mzuri sana kwa Rebecca,alipoteza baba yake mzazi, kaka yake na dada yake. Wote walifariki katika mazingira ya kutatanisha wakifuatana. Lakini hili halikumfanya Rebecca kukata tamaa na kuacha huduma bali alisonga mbele na kazi hii ambayo yeye anaamini ni kutoka kwa Mungu mwenyewe na hataacha kumtumikia. Kati ya mwaka 1995 na 2004 Rebecca amezunguka ulimwenguni akiwa na band ya Pure Magic akimtukuza Mungu kwa njia ya uimbaji.
Mwaka 2003 Malope alitunukiwa udaktari wa heshima kutoka chuo kikuu cha Natal kwa mchango wake mkubwa kwa jamii na muziki nchini Africa kusini. Na Desemba mwaka huo huo alishinda tuzo ya Kora(Kora music award) mwanamuziki bora wa Injili.
Katika wanamuziki ambao alishirikiana nao kwa karibu sana na wamekuwa na mchango mkubwa kwake ni pamoja na marehemu Vuyo Mokoena.

Mwaka 2004 Malope alianza TV show yake “Gospel time” ambayo inafanya vizuri sana. 
Mwaka huu wa 2012 tarehe 25,February ,Malope  amefanya Live recording katika jiji la Pretoria, na hii ni album ya 31. 

Msama Promotions waandaaji wa matamasha ya makubwa ya injili Tanzania,Katika Tamasha la Pasaka la mwaka huu wanamleta Malkia wa muziki wa injili Africa, Dr.Rebecca Malope katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam tarehe 08/04/2012.siku ya pasaka.
Rebecca Malope ataongozana na band yake ya wanamuziki 13. Ameahidi kufanya makubwa siku hiyo katika uwanja wa Taifa.

Baadhi ya Tuzo ambazo Dr. Rebecca Malope amewahi kutunikiwa.

Music awards
1994 – Best Gospel Singer

1997 – Best Selling Album for Uzube Nam’

1998 - Best African Gospel Artist & Best Selling Album for Angingedwa

1999 – Best Female Artist and Best African Gospel for Somlandela

2002 – Best Gospel Artist for Sabel Uyabizwa

2003 – Best African Gospel Artist for Iyahamba Lenqola

2004 – Best African Gospel Artist for Hlala Nami

No comments:

Post a Comment