Nabii ataka Maaskofu Matajili wachunguzwe

Askofu na Nabii Nicolaus Suguye (pichani) wa Huduma ya Neno la Upatanisho (WRM), Matembele ya Pili- Kivule, Dar ameitaka serikali kuchunguza uhalali wa mali za watumishi wa Mungu hasa wale wenye utajiri wa kutisha.

Nabii Suguye alitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita alipokuwa akihubiri kwenye huduma hiyo na kusema anasikitika kuona baadhi ya watumishi wa Mungu wanamiliki utajiri mkubwa kama nyumba, magari na mali nyingine lakini hawasemi fedha walizitoa wapi.

“Naiomba serikali ichunguze mali za watumishi wa Mungu kwani wanazipata kwa njia isiyo sahihi. Wengi wamekuwa wakiagiza vitu kutoka nje ya nchi kwa mgongo wa kanisa na vikifika nchini vinakuwa mali zao,”…

Nabii Suguye alisema watumishi wa Mungu watakaobainika kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu wafutiwe usajili wa huduma zao ili kuwa fundisho kwa wengine wenye lengo la kutaka kufanya hivyo.
“Katika kazi ya Mungu hakuna biashara, watumishi hao wenye utajiri wa kutisha wanaupata wapi? Mbaya zaidi fedha wanazopata wanashindwa kuwasaidia yatima na wajane badala yake wanazitumia kwenye mambo ya anasa kama kununulia magari ya kifahari,” alisema Suguye.

Askofu na Nabii Nicolaus Suguye wa Huduma ya Neno la Upatanisho (WRM)



No comments:

Post a Comment