Maznat Bridal anakuleta 10th Anniversary

Maaznat ni mdau wa blog hii ambaye kazi yake ni kupamba maharusi na saluni aliyebobea katika kufanya kazi hiyo kwa muda mrefu hivyo ameandaa event katika kutimiza miaka 10 ya kazi hiyo anayotegemea kuifanya siku za baadae ikiwa ni namna ya kumshukuru Mungu kwa hatua  aliyomtoa na kumfikisha hatua aliyofikia mpaka sasa.


Katika kusherekea event hiyo ya 10th Anniversary itakayofanyika 5-5-2013 Diamond Jubilee mahususi kwa wale waliowahi kuwa wateja wake au kuhudumiwa naye,wanaotegemea kuwa wateja wake wapya na pia wajasiliamali wa aina zote kuanzia watu wa mapambo,urembo,washehereshaji katika Events na harusi mbalimbali wanakaribishwa.

Katika kuhudhulia event hiyo unatakiwa kuchangia Elfu 50,katika gharama hiyo utapata kitenge ambacho kitakuwa sare ya kuvaa siku hiyo katika ukumbi wa Diamond Jubilee Chakula,Vinywaji,Zawadi na burudani mbalimbali zitakuwepo siku hiyo kama Bahati Bukuku,The Voice na wengine wengi

Maaznat akizungumzia mafanikio yake mpaka sasa katika kazi yake hiyo amesema mafanikio ni makubwa mpaka sasa tofauti na alikotoka na Kusema Mungu amekuwa mwaminifu na Kumpigania siku hadi siku,akiongeza kuwa ameweza kudumu na kuhimili mikikimiki katika kazi yake akizunguza na kusema alianzia kazi zake kufanyia nyumbani mpaka leo ameweza kumiliki eneo kubwa ambalo amefungua bihashara mbalimbali kama kuuza vifaa vya urembo,nguo za maharusi,vifaa vya urembo na saluni ya kike kubwa yenye kuhudumia maharusi wengi kwa wakati mmoja.

Maaznat tofauti na kazi ya kupamba maharusi na saluni kwa taaluma ni mwanasheria ngazi ya uzamili ila ametokea kubobea katika kazi yake hiyo ya Urembo na Upambaji wa maharusi na saloon zaidi tofauti na tahaluma yake.
Shughuli zake na ofisi ilipo anafanyia Mikocheni jirani na njia ya kwenda Mikocheni B kwa Mama Rwakatare

                 Maaznat  

wadau wa media walioudhulia mkutano huo ofisini kwake maeneo ya Mikocheni 
Kitenge kinachotegewa kuvaliwa siku ya Event hiyo hapo siku za baadae 
Sehemu ya mwonekano wa ndani ya ofisi ya mdau Maaznat maeneo ya Mikocheni 

wadau wa habari wakiwa kazini kumsikiliza Maaznat kuelezea kahusu Event hiyo 
Baadhi ya wafanyakazi saluni kwake


Kwa mawasiliano zaidi kuhusu Event hiyo.
0752444470
0783444470
0718818999


No comments:

Post a Comment