Rev.Edward Amri asherehekea miaka 25 ya ndoa yake.

Siku kadhaa zimepita Rev. Edward Amri aliandaa  Jubilei ya miaka 25, ya ndoa yake na tukio hilo lilikuwa kielelezo cha jinsi wanandoa wanavyopaswa kuishi. Kwa maneno na matendo. Mbele ya hadhila, kiongozi huyo alikuwa kielelezo cha upendo wa Agape unaofaa kuigwa na wale waliompokea Yesu Kristo kuwa BWANA  na mwokozi wa maisha yao.

Umati mkubwa uliohudhuria Jubilei hiyo, iliyofanyika katika kanisa la AKUZAMU lililopo katika Jengo la IPS Gorofa ya pili, ambapo alipata wasaa wa kutamka Neno la Upendo na baadaye hafla fupi iliyofanyika Hoteli ya Serena iliyopo katikati ya jiji la Dar es salaam.
Rev. Rev.Edward Amri na Mke wake Mama Mchungaji Mary Amri waki furahi kwa kuitazama pete ya ndoa.
Akijawa na furaha  kiongozi huyo alisema: “Nimeamua kuonyesha kwa vitendo mbele ya Mungu na uma wa watu pale nilipotoa upya tamko langu la upendo kwa mke wangu, mpenzi  Mary Amri kuwa ‘NAKUPENDA MKE WANGU KAMA KRISTO ANAVYOLIPENDA KANISA LAKE.’
Pendo la kweli lililotoka ndani kabisa ya moyo wangu!

Itakumbukwa  kuwa somo la upendo wa Mungu ndio msingi halisi wa maono ya huduma yetu ya AKUZAMU nasi tukiwa tunalifundisha, tunahubiri na kutenda upendo wa Mungu, hii ni fursa ya pekee kwangu kudhihirisha upendo nyumbani kwangu kwanza, kama Neno la Bwana linavyosema:
“Kila mume anapaswa kumpenda mke wake kama Kristo anavyolipenda kanisa lake,” ( Waef 5:23).
 Rev. Rev.Edward Amri na Mke wake Mama Mchungaji Mary Amri katika pozi















Karibu  AKUZAMU tushirikiane Neno na Tendo kwa upendo wa BWANA wetu Yesu Kristo.
  



















Kwa maombezi piga: 0753-377776, 0782-377776, 0659-377776
Barua Pepe: info@akuzamu.org
Rev.Amri@facebook/twitter.com
Tovuti: www.akuzamu.org

No comments:

Post a Comment