Raisi Kikwete azindua utoaji wa Vitambulisho vya Taifa


Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Askofu Malasusa wa KKKT kitambulisho cha taifa.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete siku ya jana azindua rasmi mfumo wa usajili na utambuzi wa watu na utoaji wa vitambulisho vya taifa uliofnyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam jana

Uzinduzi huo ulioudhuliwa na viongozi mbalimbali wa serikali na Dini mbalimbali kama Rais Mstaafu awamu ya pili Mzee Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa, Mstaafu wa Zanzibar Amani Abeid Karume, s wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad, Mzee Kingunge Ngombale Mwiru, Askofu Malasusa wa KKKT,Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Dkt.Emmanuel Nchimbi,Mkurugenzi Mkuu wa NIDA Bwana Mwaimu,Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Bwan Said Meck Sadik.Mkurugenzi Mkuu wa PPF,Mkurugenzi Mkuu wa NSSF na wengine wengi viongozi wote hao walipata vitambulisho vyao hapo hapo katika uzinduzi  huo
  
Akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa mfumo wa usajili na utambuzi kwa wa watu na utoaji vitambulisho vya taifa, Rais Kikwete alionya juu ya utoaji vitambulisho kwa watu wasiostahili na kusema kwamba Serikali yake haitavumilia kuona hali hiyo ikitendeka.
Alisema suala la vitambulisho vya taifa ni nyeti na linapaswa kuendeshwa kwa kufuata miiko na sheria za nchi, hasa kwa kuzingatia kuwa vitambulisho hivyo vitatumika wakati wa uchaguizi mkuu ujao.

Kama sehemu ya kuimarisha utendaji kazi, mamlaka hiyo ya vitambulisho vya taifa imeanzisha ushirikiano na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec),ambayo inakusudia kuvitumia vitambulisho hivyo katika uchaguzi mkuu ujao. Mkurugenzi Mkuu wa Nida, Dickson Maimu alisema ushirikiano huo itasaidia kuboresha kazi za utoaji vitambulisho na kwamba utakamilika kwa wakati. Hata hivyo alisema bado ofisi yake inakabiliwa na tatizo la vitendea kazi na kuiomba serikali kuongeza bajeti. 

Vitambulisho hivyo vitaanza hivi karibuni kutolewa kwa watumishi wa umma, kwani taarifa zao pamoja na alama nyingine zilikwisha chukuliwa. Hatua hiyo inakuja katika wakati ambapo taifa liko kwenye mchakato wa uandikwaji wa katiba mpya, ambayo nayo pia imepangwa kupatikana kabla ya uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015.

Kuhusu Zanzibar ambayo inatumia vitambulisho vya mkazi vilivyoanza kutumika tangu mwaka 2006, kumeelezwa kuwa, wananchi wa eneo hilo nao watajumuishwa kwenye zoezi hilo.


No comments:

Post a Comment