VHM (Voice Of Hope Ministry) yatambua mchango wa Living Water Centre Kawe


VHM (Voice Of Hope Ministry) imesema inatambua mchango wa huduma Living Water Centre kawe   katika kufanikisha huduma zake vijijini ambako Injili imefika kwa kiasi kidogo,maneno hayo yalisemwa na Kiongozi wa huduma hiyo Mch.Peter Mitimingi.

Timu nzima hiyo ya VHM ikiongozwa na Mch.Peter Mitimingi walikuwepo kanisani Living Water Centre Kawe jumapili iliyopita kutoa shukrani zao jinsi ya Living Water Center livyowahi kuwawezesha kifedha katika safari zao za kuhudumu vijijini ambako Injili imefika wa kiwango kidogo sana  pengine haijafika.
Ibada hiyo iliongozwa na  Kiongozi wa huduma hiyo Mch.Peter Mitimingi.

VHM (Voice Of Hope Ministry) ni huduma inayofanya kazi ya kuhudumu Injili vijijini maneo ambayo yametelekezwa au Injili imefika wa kiwango kidogo sana,Kwa muda wa miaka 6 iliyopita VHM wamekuwa wakihubiri Injili katika ukanda wa Pwani upande ambao Jamii ya kiislam inakaa wa wingi.

VHM Wamesema wamekuwa wakimwona Mungu katika huduma yao akifanya kazi ya kuwakomboa maelfu watu wagonjwa na nguvu za giza pia akushuhudia waganga wa kienyeji na wachawi wengi wakisalimisha silaha zao na maisha yao kwa Yesu.

Sambamba na Injili huduma ya VHM imekuwa ikijihusisha na kutoa huduma za afya kwa jamii huko vijijini bure ikiwa ni sehemu ya huduma yao pale wanapokutana na watu wenye uhutaji wa matibabu kiafya maana si wote wanao jiweza kwenda kulipia gharama hospitali 

1.VHM kabla ya kwenda ufanya huduma huwa inatuma watu kwenda kufaya utafiti katika vijiji husika vitakavyokuja kufanyiwa huduma wanachobaini huwa uchawi na ushirikinana ngome za ibilisi katika kuwaonea watu.

2.VHM hatua ya pili huwa wanatuma wana maombi kikosi kazi ili kuangamiza nguvu zote za giza na mapepo

3.VHM wanatuma timu ya Kufanya uinjilisti nyumba kwa nyumba kwa ajili ya maandalizi ya mkutano wa nje

4.Baada ya hayo wanafanya mkutano wa injili ili kuwahubiria watu injili ya Yesu Kristo iletayo wokovu na kuwafundisha mafundisho ya awali ya kuukulia wokovu.

Huduma ya VHM chini ya tumishi wa Mungu Mch.Mitimingi mafanikio ambayo waeyapata mpaka sasa ni watu wengi weokoka na kumpa Bwana Yesu maisha yao,Mabadiliko katika jamii zilizohudumiwa,Umoja wa Makanisa umeimalika,Watu wengi hata wapagani weuona upendo wa Yesu kwa uhalisia kupitia huduma ya VHM hasa hasa katika huduma za kijamii matibabu ya afya za wale wanao umwa pia uwagawia watu wenye kuhitaji vitu kama nguo na chakula

Huduma ya VHM inayomikakati mbalimbali ya kuzunguka mikoa yote ya Tanzania kupeleka Injili vijijini maeneo ambayo yaetelekezwa au Injili imefika wa kiwango kidogo sana
Kwasasa wanatarajia upeleka Injili ikoa ya Iringa,Njombe,Mbeya,Sumbawanga,Katavi,Kigoma,Kigoma,Tabora,SingidaMorogoro,Lindi na Pwani

Huduma ya VHM inaomba kujumuika a wewe katika huduma anayofanya kwa kweda nao kwa hali na mali ilikufanikisha na kuvuruga kazi za bilisi na nguvu za giza na kusimamisha Nguvu na utawala wa Yesu Kristo huko vijijini ambako maeneo ambayo yaetelekezwa au Injili imefika wa kiwango kidogo.
                











 
Ofisi za VHM ziko mwenge zmetazamana na Hospitali ya Mama Ngoma
Mawasilano: +255713183939     +25568866662      +255767563939  
Kwa sadaka yako kusapoti huduma hii  Tigo Pesa 0713183939    Airtel money 068866662     Mpesa 0767563939  

No comments:

Post a Comment