Waliofariki katika Mlipuko wa Bomu Kanisani Arusha wazikwa

Misa ya Mazishi ya wahanga wa mlipuko wa bomu la Jumapili iliyopita kwenye parokia teule ya Olasiti ilianza katika eneo lile lile mlipuko ulipotokea siku ya jana Jijini Arusha.Misa hiyo iliongozwa na Muadhama Polycarp Kardinal Pengo, Askofu Mkuu wa Dar es Salaam.

Maandamano yalianzia toka chumba cha kuhifadhia maiti, miili ikapelekwa makao makuu ya Asofu Mkuu, Burka na baadaye ikawasilishwa kanisani

Kardinali Pengo alisema Ndugu zangu nafasi hii inaunganisha mawazo ya furaha na uchungu kutokana na kilichotukutanisha leo,mazingira haya yanaweka ugumu wa kupata cha kusema.Ila sisi ni watu wa imani. napenda kueleza imani yetu kama tunavyopaswa kuwa kwenye mazingira haya.

Tumejumuika ili kuwaweka kwenye nyumba ya milele hawa marehemu, lakini pia tunatumia nafasi hii kubariki Kanisa.

Kila mbatizwa ni kiungo cha mwili wa Kanisa. Kila kiungo cha mwili kinapaswa kuungana na kichwa cha Mwili ambae ni Yesu Mwenyewe,Kristo akipitia kwa mdomo wa mtume Paulo anatufundisha kuwa “Msijaribu kushindana na uovu kwa uovu, lakini shindeni uovu kwa wema”.

Nawauliza waumini: “Wale waliotekeleza ubaya huu, akija mbele yetu akasema ni mimi ndiye, tungefanya nini kama waumini kwa kufuata mfano wa Yesu?”

Mimi nawaambia “Tujifunze kutoka kwa Bwana wetu Yesu Kristo: ‘Tusidiriki kulipia uovu kwa uovu, lakini tutende mema ili kushinda uovu’.”

Amemalizia kwa kusema: Tukio hili na tukio la mauaji ya Padre Mushi, isiwe sababu ya kuacha amani ya nchi yetu isambaratike.Lakini ni jukumu la wananchi wotte kuhakikisha nchi yetu haisambaratiki.

Wenye mamlaka watimize wajibu wao.Sisi wakristo tusamehe, tusijibu uovu, tudumishe amani na upendo katika taifa letu,alimaza kwa kusema!



source:arusha-yetu.blogspot.com

No comments:

Post a Comment