Tanzania worship Experience washindi wanne wagongana na Kugawana Millioni 12

 Wikiendi hii kulikuwa na Tamasha Kubwa Jijini Dar es salaam liile shindano lililokuwa likirushwa na kituo cha Tv Tbc 1 "Tanzania worship Experience lilifikia mwisho siku ya Jumapili katika ukumbi wa Diamond Jubilee ambapo washindi wa nne walifungana kwa kura hivyo kupelekea majaji kutoa shilingi milioni 12 kwa washiriki wote walio gongana kwa kura.

Mchuano ulikuwa mkali sana hivyo mpaka mwisho wa shindano washiriki 4 waligongana kwa kura za watazamaji wa Tbc 1 hivyo shilingi milioni 12 iligawanywa kwa washiriki wote wa nne,na kila mmoja alipata milioni Tatu tatu.

Mkurugenzi wa shindano hili Mr Bilionea alisema washiriki wote walio ingia kumi bora watapata nafasi ya kutengeneza albam chini ya Tanzania worship Experience mwakani 2013.Shindano hili mwakani lina tarajia kuzunguka mikoa 3 kwa mujibu wa Mkurugenzi Bilionea.

 Upendo Nkone alikuwepo kuhudumu katika Event hiyo.
 Ambwene pia alikuwepo katika Event hiyo.
Meza kuu ya Majaji katika Event hiyo.
Jaji Luis Jonas akitoa matokeo ya washindi wa nne.
Washindi wa nne walio gongana kwa kura wakiwa wameshikiria hundi ya shilingi milioni 12 waliyo gawana.
Upendo Nkone akiwa na Mc wa Event hiyo Jimmy Temu
Wadau mbalimbali walijitokeza katika  Event hiyo

Source:http://unclejimmytemu.blogspot.com

No comments:

Post a Comment