Wakristo Nigeria waendelea kuuawa kwa risasi kanisani

Wakristo nchini Nigeria wameendelea kuuawa kwa kuvamiwa makanisani na watu wanaoaminika kutoka katika kundi la Boko Haramu lisilotaka kuona chembe ya ukristo nchini humo. Mbali na kufanya mauaji ya mamia ya wakristo, wiki jana walivamia kanisa la kiptrostant na kuua wakristo 11 likiwaacha majeruhi 30.

Shirika la Habari la AP lilieleza kwamba watu 11 waliuawa na wengine 30, kujeruhiwa vibaya Kaskazini mwa Nigeria
ndani ya kambi ya Jeshi ya  Jaji, katika Jimbo la Kaduna, la Mt. Andrew Military.  

Mkurugenzi wa Uhusiano katika Jeshi la Nigeria, Brig. Gen. Bola Koleoso, alisema gari lililokuwa limejaa milipuko liliingia eneo hilo na kulipuka, wakati hilo bado likiwasha masikioni mwa watu gari lingine aina ya Toyota Camry, iliyokuwa imeegeshwa  nje ya kanisa hilo lililipuka.



Alisema eneo la Jaji ni alama ya kijeshi kwa taifa hilo, na ndipo yalipo makazi ya makamanda wengi na kipo chuo cha maofisa wa Jeshi kinachotegemewa, pia ni mahali vilipo vikosi vya majini, angani na vya ardhini.

Shambulio hilo limetokea siku mbili tu, baada ya Jeshi hilo kutangaza hadharani kuwa watatoa dola za kimarekani 1.8 milioni, kwa yeyote atakayemkamata kiongozi wa kundi hatari la Boko Haramu.
Mbali na hilo, milipuko hiyo pia imekuja, mwezi mmoja baada ya kanisa moja mjini Kaduna kushambuliwa maili 25 kutoka Jaji.

Makanisa nchini Nigeria, yamekuwa yakishambuliwa na kuleta machafuko miongoni mwa watu katika maeneo mengi ya nchi hiyo ikiwemo Kaduna. Katika mji wa Kaduna hadi sasa uvamizi huo umepelekea watu zaidi ya 50 kupoteza maisha yao.




No comments:

Post a Comment