TAG Mwanga Lamtegemeza Mchungaji Gari la Sh. 15 Mill

“Kweli kumtumikia Mungu kuna faida, kama utakubali na kutii sauti ya wito wake na kwenda kumtumikia mahali ambapo amekutuma, ukamtumikie lazima akubariki” ukatumikie lazima akubariki hayo ni maneno ya Askofu  wa Kanisa la TAG, Jimbo la Kigoma , Omary Mulenda, akishukuru Mungu baada ya kukabidhiwa gari aina ya Noah yenye thamani  ya shilingi milioni 15 na Kanisa lake la Msifuni Mwanga, wakati wa ibada wiki moja imepita.

 Akiendelea kushukuru akiwa pamoja na familia yake, mtumishi huyo wa Mungu alisema, Mungu aliwaita katika utumishi wakaitika na mwaka 1993, yeye na mke wake walijiunga na chuo cha Biblia Dodoma kusoma masomo ya theolojia.

 Alisema kuwa katika kipindi walichoanza huduma yao, walikuwa na kipindi kigumu sana wakiwa chuoni wakiwa na swali kujua Mungu aliwaita wamumikie wapi.Lakini baadae wakapata kujua wapi wameitwa na kuanza kutumika na sasa kuona matunda ya kumtumikia Mungu.

No comments:

Post a Comment