Ilala TAG laandika Historia ya Miaka 40

Ilikuwa ni siku nzuri jumapili ya Desember 15 mwaka jana, kwa waamini wa kanisa la Tanzania Assemblies of God Ilala jijini Dar es salaam, wakiongozwa na shujaa wao Mchungaji Titus Mkama na Mke wake Mary, walipoadhimishwa miaka 40 ya kuzaliwa kwa kanisa hilo wakiwa na ushindi mkubwa.

Akihubiri katika ibada hiyo iliyohudhuriwa na maaskofu wachungaji na viongozi mbalimbali wa dini na serikali, Askofu Mkuu wa kanisa la Tanzania Assemblies of God Dk Barnabas Mtokambali  alisema kuwa,
Mchungaji Titus Mkama wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God Ilala Jijini Dar es salaam
Katika ibada hiyo iliyokuwa na mvuto wa hali ya juu, kutokana na historia  ya mtumishi wa Mungu  Mchungaji Titus Mkama kwa mambo mbalimbali pamoja na mapito makali aliyopitia kwa kipindi cha utumishi wake, Askofu mkuu wa TAG Dr Mtokambali aliongoza maombi mbalimbali ya kumuombea mtumishi huyo na mke wake huku wengine walitokwa na machozi.

Askofu Dk. Mtokambali alisema, kwa nini Mungu anatutaka tuwe na maadhimisho maalumu ya matukio ya maisha yetu, Mungu aliwaagiza watu wake kufanya maadhimisho kama hayo kama neno la Mungu linavyoeleza, kutoka katika kitabu cha kumbukumbu la Torati (16:9-17)

  Alisema kuwa, Mungu anatambulisha sherehe na maadhimisho siyo maonesho wewe ulivyo, bali ni kufanya kwa mapenzi ya Mungu na siyo vinginevyo.

 Aidha alisema kuwa maadhimisho yanawaletea watu wa Mungu kufurahi na kukomaza ushirika wao. Askofu huyo alisema kuwa maadhimisho pia yanatumika kama wakati wa matoleo ambapo alisisitiza watumishi wa Mungu waliohudhuria sherehe hiyo kufanya changizo la kiasi cha pesa zilizohitajika sh. Milioni 150, kwa ajili ya upanuzi wa jingo la ibada, ambapo wageni na watumishi wa Mungu walihudhuria ibada hiyo na kutuoa hadi mbalimbali .

  Naye mchungaji kiongozi wa kanisa Dk. Titus Mkama alitoa shukrani zake kwa Mungu na kwa watu wote waliohudhuria na kuwezesha kufanikiwa maadhimisho hayo ambapo kwa kukamilisha furaha yao Askofu pamoja na mtumishi huyo na wengine walilishana keki maalumu pamoja na ndafu iliyoandaliwa.

  Ibada hiyo ya maadhimisho ilipambwa na kwaya, waimbaji mbalimbali wa nyimbo za injili ambapo furaha, vifijo na vigelegele vilitgawala siku hiyo isiyo ya kawaida.

  Akisoma historia fupi ya Kanisa hilo, Mtumishi wa Mungu, Mchungaji DK. Titus Mkama alitoa shukrani zake kwa viongozi mbalimbali kwa Makanisa waliohudhuria na kwa watu alioanza nao pamoja huduna hiyo.

Dk. Mkama alisema kuwa wanamshukuru Mungu kuwa kanisa hilo limekuwa la kwanza kupewa kibali na Serikali ya Tanzania kuhubiri magerezani huduma ambayo waendelea nayo hadi sasa.
  Alisema kuwa katika huduma ya jamii wamekuwa wakiwatunza wazee, kuwalea watoto yatima ambao wengine wameweza kuwaendeleza hadi chuo kikuu.

  Pamoja na mafanikio hayo lakini pia wanazo changamoto kama vile upanuzi wa viwanja vya kuhubiria injili baada ya viwanja vya serikali kuzuiliwa.

  Kanisa la TAG ilala ilianzishwa mwaka 1973, shule ya uhuru kariakoo, na baadaye walihamia katika maeneo ya msimbazi Centre Ilala baada ya eneo la zamani kuonekana kuwa halitoshi kukidhi ongezeko la waumini kutokana na ufinyu wake.

No comments:

Post a Comment