Pastor Carlos Kirimbai,Kutabiliwa na Kutamkiwa 101

Pastor Carlos Kirimbai Manna Tabernacle Bible Church
Naona siku hizi kumezuka sana kutamkiwa baraka na mema ambayo inaambatana na kutakiwa kusema amen na kulike na mengineyo kama hayo. Mimi am just curious. Kutamkiwa baraka ni sawa na kutamkiwa kinabii or which ever other way ni sawa pia. Ila sasa:

2 PET. 1:20-21 SUV

Mkijua neno hili kwanza, ya kwamba hakuna unabii katika maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani tu. Maana unabii haukuletwa po pote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu.

Huwezi kutabiri au kutamka utakavyo wewe bali unasema yale ambayo Mungu anakupa kusema.

Kutamka au kudecree ninavyoelewa mimi huja baada ya neno kuvuviwa alafu ukisha kutafsiri anavyokuongoza Roho unalitamka kwa mamlaka ya kudecree juu ya msikilizaji. Kwangu na uelewa wangu mdogo, nabii wa agano jipya ni mtu anayefundisha na kuhubiri kwa uvuvio huku akiziweka wazi siri na mafumbo ya Mungu katika maandiko. Neno la Mungu ndo msingi wa kila decree.

2 PET. 1:19 SUV

Nasi tuna lile neno la unabii lililo imara zaidi, ambalo, mkiliangalia, kama taa ing’aayo mahali penye giza, mwafanya vyema, mpaka kutakapopambazuka, na nyota ya asubuhi kuzuka mioyoni mwenu.

Ili niweze kutoa matamko kiusahihi inabidi kwanza nidake alichosema ndipo niweze nami kusema.

AMO. 3:8 SUV

Simba amekwisha kunguruma, ni nani asiyeogopa? Bwana MUNGU amenena, ni nani awezaye neno ila kutabiri?

EBR. 13:5-6 SUV

Msiwe na tabia ya kupenda fedha; mwe radhi na vitu mlivyo navyo; kwa kuwa yeye mwenyewe amesema, Sitakupungukia kabisa, wala sitakuacha kabisa. Hata twathubutu kusema, Bwana ndiye anisaidiaye, sitaogopa; Mwanadamu atanitenda nini?

No comments:

Post a Comment