Askofu Hotay wa Kanisa la Angilikana Dayosisi ya Mount Kilimanjaro akabidhiwa rasmi kiti chake cha Uaskofu.

Wakati zikiwa zimepita siku chache mara baada ya Mahakama kuu kanda ya Arusha kutupilia mbali pingamizi la waumini wa kanisa la Angilikana Dayosisi ya Mount Kilimanjaro juu ya Uaskofu wa Askofu wa kanisa hilo Stanley Hotay (Leo)kanisa hilo limemuweka rasmi kazini askofu huyo sanjari na kutangaza msamahaa kwa waumini hao watatu kwani wamechangia sana kanisa hilo kupoteza muda kwenye kesi hiyo pamoja na aibu kubwa kwenye masikio ya watu wengi

 Akiongea katika ibada maalumu ya kuweza kumpa nafasi ya kuongoza Dayosisi hiyo Askofu mkuu wa kanisa hilo la Angilican Tanzania Dkt Valentino Mokiwa alisema kuwa mpaka

Askofu Stanley Hotay
Akiongea katika ibada maalumu ya kuweza kumpa nafasi ya kuongoza Dayosisi hiyo Askofu mkuu wa kanisa hilo la Angilican Tanzania Dkt Valentino Mokiwa alisema kuwa mpaka sasa wameshatangaza Msamaha  kwa watu hao ambao walitia aibu kanisa hilo hivi karibuni

 Askofu huyo alisema kuwa hapo awali baadhi ya waumini akiwemo yeye mwenyewe walikuwa katika wakati mgumu sana kutokana na  kesi hiyo lakini kutokana na ukweli na haki  ya Askofu Hotay aliweza kupata haki yake kupitia mahakama  Septembe  tano mwaka huu huku waliofungua kesi hiyo wakishinndwa kusonga mbele

 Mbali na hayo alisema kuwa kuna masaa mengi sana ambayo yamepotea katika Kesi hiyo ambayo ilifunguliwa na waumini watatu lakini kanisa kama kanisa linapswa kuhakikisha kuwa linatoa msamaha wa kweli ambao unatoka ndani ya Mioyo yao kwani watu hao walidanganywa na hata kufikia hatua ya kutoka nje ya Kundi bila kujua kuwa hali hiyo inachangia sana hata mmonyoko wa Kanisa na aibu sana

 Katika hatua nyingine alisema kuwa kanisa hilo limempa Nafasi ya kuongoza jimbo hilo kwa mujibu wa katiba ya Kanisa hilo na kutokana na hali hiyo kiti hicho ambacho alikuwa hakitumii kutokana na kesi ambayo ipo mahakamani sasa anaanza kazi rasmi kwa kuwa sheria inamruhusu huku waumini wa  kanisa hilo nao wanatakiwa kumpa ushirikiano na kukumbuka Viapo mbalimbali ambavyo vinatumika na kanisa hilo

 Naye Askofu Stanley Hotay aliwaambia waumini wa kanisa hilo kuwa ili ufanikiwe ni lazima kwanza uhakikishe kuwa unatoa msamaha hata  kwa wale ambao wamekuwa ni vikwazo vya kushindwa kufikia katika malengo mbalimbali ambayo yanatakiwa kufikiwa ingawaje vikwazo ni vingi sana katika safari ya Ushindi

 Askofu huyo alifafanua kuwa pamoja na kuwa amepita katika wakati mgumu sana hasa wa kuwa na kesi ya kutotambulika na waumini wake lakini bado ana nafasi kubwa sana ya kuweza kuwatumikia hao hao na kuwafanya wabadilishe fikra kwani hapo awali hawakujua wanachokifanya hali ambayo ilizaa aibu kubwa sana mbele ya kanisa la Angilikana dayosisi ya Mout Kilimanjaro.

 Aliwataka waumini wa kanisa hilo kuhakikisha kuwa wanasahau hilo na kuanza kufikiria upaya kwani bado kanisa hilo lina muitikio mkubwa sana wa kuweza kuwasaidia waumini pamoja na jamii kwa kuweza kuhamasisha maendeleo ambayo ndiyo yana amani kwa maslahi ya Taifa la Tanzania

 Mkuu wa mkoa wa Arusha Bw Magesa Mulongo ambaye alikuwa ni mgeni rasmi katika ukabidhiwaji wa kiti hicho kwa askofu huyo ambaye hapo awali alikuwa ameshasimikwa kama askofu wa kanisa hilo alisema kuwa wakristo wanatakiwa kujua hakuna dhambi mbaya sana kama dhambi ya kutamani madaraka kwani dhambi hiyo ndiyo inayochangia kwa kiwango kikubwa sana kuwepo kwa migogoro sana

 Bw Mulongo aliongeza kuwa ni vema kama mtu anayetamani Madaraka hata kama ni ya Uaskofu basi kuomba Mungu kna wala sio kuwa chanzo cha kuanzisha Kesi ambazo hazina Tija na ambazo zinapotosha hata maana halisi ya Wokovu huku tamaa kama hizo zikiwa ni chanzo pekee cha kuweza kusababisha amani kutoweka



Source:fullshangweblog.com

No comments:

Post a Comment