Waumini wapiga kura kuingia na bunduki kanisani.


 Kukithiri kwa mashambulizi katika makusanyiko ya watu wengi nchini Marekani kumepelekea  baadhi ya wamarekani kupiga kura na kuamua kubeba silaha za moto kama bunduki wakati wa Ibada ili kujilinda.

Kwa mujibu wa utafiti uliosimamiwa na taasisi iitwayo, “Public Religion Research Institute (PRRI), ya Marekani kura hiyo ilihusisha watu 1006 waliochaguliwa kwa kuzingatia makundi yote na asilimia 55 walieleza kufurahishwa na utaratibu wa kubeba bunduki na bastola zenye risasi za moto makanisani, wakati wa ibada.

Miongoni mwa asilimia  55 waliopendekeza ubebaji silaha wakati wa kumuabudu Mungu, asilimia 38 wanatoka katika chama cha Republican kinachowakilishwa na Mitt Romney, anayechuana vikali na Rais Barrack Obama wa Democratic katika kinyanganyiro cha urais, kwenye Uchaguzi Mkuu wa nchi hiyo unaotarajiwa kufanyika mwezi Novemba, mwaka huu.

“Unajua tumeamua kufanya utafiti huu, ili kupata maoni tofauti baada ya mahakama katika Jimbo la Georgia kuruhusu watu kuingia na bunduki katika nyumba za ibada, kutokana na kuwepo kanuni kuwa kuna baadhi ya maeneo ambayo mtu hapaswi kuingia na silaha kama bunduki,” alisema Mkurugenzi wa PRRI Bw. Daniel Cox.

Alisema kuwa utafiti huo uliofanyika kati ya Agosti 8 na 12, uliainisha maeneo mbalimbali ambayo watu wanaweza kuwa huru kwenda na bunduki na yapi yasiyofaa; na hayo ni pamoja na kutokuwa na silaha kwenye vyuo vikuu na maeneo ya huduma za serikali.

Sambamba na hilo, utafiti pia ulichanganua kuwa, asilimia 68 ya wamarekani walifurahishwa na sheria ya uhuru wa kuwa na silaha. 


“Licha ya utafiti huu juu ya udhibiti wa silaha, watu wengi nchini Marekani wanasema kwamba kama ulivyo uhuru wa kikatiba wa kutumia silaha , basi hilo nalo ni jambo la muhimu kama ulivyo uhuru wa kuongea bila kuvunja sheria,” alisema Mkurugenzi mtendaji wa PRRI, Dk. Robert  Jones, na kuongeza:

“Lakini hakuna cha ajabu kwa kuwa wanaounga mkono suala zima la kuwa na uhuru wa bunduki ni wamiliki wa bunduki

Julai 20, 2012 kijana mmoja alivamia ukumbi wa sinema na kukuta watu wakiendelea kuangalia sinema ya The Dark Knight Rises, akawafyatulia risasi waliokuwa wakishuhudia tukio hilo, jambo lililosababisha watu 12 kupoteza maisha na wengine 58 kujeruhiwa.

Kama hilo halitoshi Agosti 5, 2012 kanisa moja Sikh Temple la Oak Creek, lilimiminiwa risasi za moto na watu sita waliuawa huku wengine wanne wakijeruhiwa.

  

No comments:

Post a Comment