Waandishi wa habari nchini leo waandamana, Waziri Nchimbi atimuliwa Jangwani na Waandishi

Waandishi wa habari nchini leo wameandamana nchi nzima kwa amani kulaani kuuawa kwa mwandishi mwenzao, Daud Mwangosi aliyeuawa Septemba 2, mwaka huu katika Kijiji cha Nyololo, Iringa.

Maandamano hayo ambayo yalikuwa ya kimyakimya yamefanyika katika mikoa yote nchini kuanzia saa 3:00 asubuhi, Maandamano hayo yalioanzia katika ofisi za Channel Ten hadi Jangwani ambayo yalikusanya waandishi wote wa mkoa wa Dar es Salaam kwa ajili ya kupinga tukio hilo.
 
 Katika hali ambayo haikutegemewa Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emenuel Nchimbi amefukuzwa kwenye maandamano ya waandishi wa habari ya kupinga kitendo cha Jeshi la Polisi kwa mauji ya kinyama kwa Mwandishi wa Chanel Ten, Daudi Mwangosi mkoani Iringa kilichotekea hivi karibuni.
Baadhi ya Waandishi wa habari wakiwa katika maandamano leo wamevalia nguo nyeusi kwa ishara ya msiba na picha ya mwenzao Marehemu Daud Mwangosi.

Ilikuwa ni katikati ya mitaa ya Jiji la Dar es salaam mapema leo asubuhi kuelekea viwanja vya Jangwani

Wengine ujumbe wao waliufikisha kwa njia ya mabango waliyokuwa wabeba
Waziri Nchimbi akizungumza na waandishi wa habari kabla ya kukutwa na lililomkuta huko katika viwanja vya Jangwani mapema leo asubuhi.
Baadhi ya wadau wa habari wakiongea kwa msisitizo na uchungu kwa kulaani jambo la mauaji ya mwenzao.





No comments:

Post a Comment