Jaji atoa hukumu mtoto abatizwe.


Jaji wa nchini Uingereza, John Platt ametoa hukumu ya mtoto wa miaka 10 abaki kuwa mkristo na ikiwezekana abatizwe kabisa, baada ya kuwepo kwa msuguano baina ya wazazi wake ambao mmoja alitaka awe mkristo.

Hukumu hiyo ilitolewa wiki iliyopita katika Mahakama ya Romford, baada ya wazazi wa mtoto huyo kusuguana tangu Novemba 2011 huku mama akipinga mtoto wake wa miaka 10 kubatizwa kwa maelezo ya kigezo cha umri huku akitaka tendo hilo lifanyike akiwa na umri wa mika 16.

Baada ya kutoelewana, mama ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja alifungua kesi mahakamani ili iweze kuruhusu mwanaye kutobatizwa kwa kigezo cha kutojua baya na zuri, huku baba naye akidai ni muda muafaka na hakuna ulazima wowote wa kusubiri miaka 16.

Malalamiko mengine aliyokuwa akidai mama huyo ni umri wa mwanaye huyo kuwa ni mdogo kiasi cha kubadilisha imani. Jambo lililopokelewa na baba kwamba anaweza kueleza kulingana na sheria za Mungu na kwamba hata nyakati za Biblia Mungu aliweza kumtumia Daudi aliyekuwa mdogo.

Hata hivyo mwisho wa siku mahakama hiyo haikukubaliana na mama huyo na kumuamuru kuwaachia watoto wawe wakristo na wabatizwe na kwa sasa wanapewa mafundisho yanayoelezea nini maana ya kubatizwa na watakapomaliza watakuwa huru kubatizwa.

Wazazi hao walifikia mafarakano hayo baada ya kugombana na hivyo kuamua kutengana na hapo baba aliamua kubadili dini na kuwa mkristo.

No comments:

Post a Comment