Maandalizi ya Mpinga Kristo........., Umoja wa Dini 5O wazua Balaa!

Papa Benedict, Lutheran wahusika,Makanisa Mengine yajiweka kando pia Quran na Biblia zasomwa kwa pamoja

Wakati wengine wakiendelea kubishania uhalali wa ibada za mafuta na vitambaa, hatua kubwa ya kufikia umoja wa kidini yaani United Religious, utakaokuwa na nguvu kuzidi Umoja wa Mataifa (UN) imefikiwa hivi karibu, baada ya dini zaidi 50 kuandaa ibada siku ya Jumapili na kutumia Bibilia na Qura’n.

Taarifa iliyonukuliwa na Gazeti la New York Times, ilisema: “Mihimili mikuu mitatu kuelekea mfumo mpya wa dunia ambayo ni Umoja wa kiuchumi duniani, Serikali moja na Dini moja. Masikio ya wengi yameelemea kwenye mihimili miwili zaidi kuliko ule wa tatu ambao wameupuuzia. Lakini huu wa tatu ambao ni dini ya pamoja (kwa maana ya imani moja) ndio usukani na sasa unakaribia kufikiwa. Huu ndio unaojulikana kama ‘Interfaith.’ 
Papa Benedict XVI
 Makongamano na mikutano inaendelea kuongezeka kwa kasi siku hadi siku duniani, huku viongozi wakuu akisisitiza kuwepo kwa ushirikiano wa pamoja. Imani ya kuwa na dini moja "Interfaith" imekuwa ikisisitizwa kote duniani na viongozi wa dini mbalimbali wakitumia mashirika (NGOs), mashirika ya misaada, na taasisi mbalimbali, wanasisasa wakubwa wametumiwa kuipa msukumo kwa fedha nyingi katika sayari hii.”
Kisha taarifa hiyo iliongeza: “Hivi karibuni baadhi ya makanisa katika Amerika yamekwenda mbali zaidi katika suala hilo. Juni 26, mwaka huu, Kathedral ya Kitaifa (National Cathedral) katika Jiji la Washington D.C. iliandaa ibada ya pamoja  na zaidi ya makanisa 50 yalishiriki kusoma Quran wakati wa Ibada ya Jumapili.”
Wachambuzi wa siasa dini wanaeleza kuwa hiyo ni hatua katika mkakati mkubwa wa kuundwa kwa shirikisho kubwa la kidini katika kipindi cha mpito kuelekea kuzaliwa rasmi kwa umoja wa kidini  ulimwenguni, ukishinikizwa kwa kipengele cha haki za Binadamu.
Somo kuu katika Jumapili hiyo lilikuwa “Kushirikishana imani, Kushirikiana maombi na kuelewana.” Lengo likielezwa kuwa ni kuonesha upendo wa Wakristo kwa Waislamu waishio Amerika.
Miongoni mwa makanisa yaliyoshiriki ni: Christ Church lililopo jijini New York City,
All Saints Church lililopo Pasadena California, Park Hill Congregational huko Denver,
Hillview United Methodist lililopo Boise, Idaho First United Lutheran, katika mji wa San Francisco, St. Elizabeth's Episcopal Church, huko Honolulu, Makanisa makubwa (dini mbalimbali) yapatayo 26 katika Amerika yamehusika na mpango huo.
Interfaith logo
Imeelezwa kuwa usomaji huo wa Quran ni mpango maalumu wa kulainisha dini zenye misimamo mikali ili kuonesha kuwa upo uwezekano wa kufanya ibada pamoja na kumaliza tofauti zilizowatenga zamani.
Mpango huo mkubwa unatarajiwa kua endelevu ukijumuisha Wakristo, Wayahudi na Waislamu kwa njia ya kusikia na kusoma aya kadhaa, za Qur'an mara kwa mara ili watu wazoee kuwa pamoja na mwisho waunganishe mioyo yao pamoja na kuabbudu pamoja.
Kwa mujibu wa waandaaji wa mpango huo, Interfaith, Waamerika wana uhuru wa kusoma Quran popote wanapotaka. Lakini kwa Wakristo hawana nafasi ya kusoma na kujifunza kitabu hicho, hivyo kuwepo kwa utaratibu wa kuisoma kila Jumapili wanapokutana kanisani kwenye Ibada na kutawafanya waielewe na kuwa na ‘umoja’ na Waislamu na kuonyesha kutowabagua; jambo ambalo linaonesha dalili ya kuzaliwa kwa kitu kipya duniani.
Wakati huo huo, baadhi ya viongozi wa Kikristo duniani hawako radhi na muendelezo huo. Brannon Howse, mmoja wa viongozi mashuhuri alisema: “Watu hao wamekana uungu wa Yesu Kristo; wamekana ukweli wa maandiko matakatifu; wamekana uvuvio wa Biblia, ni vipi tushirikiane nao na kusoma kitabu chao kwenye ibada zetu?”

Qur'an

Kisha aliendelea: “Inasikitisha, hii siyo mara ya kwanza. Ukweli ni kwamba umoja huo umepata nguvu miongo kadhaa na baadhi ya wakuu wa dini ulimwenguni wamehusika.
Kwa mfano; habari zilizopatikana kupitia CNS zinaeleza kuhusu muungano mkubwa ‘interfaith’ wakati Papa alipotembelea jiji la Washington 2008.”
Alisema kuwa wakati Papa Benedict XVI alipofika kituo cha, Pope John Paul II Cultural Center kilichopo Washington kwa mkutano wa jioni wa dini zote ‘interfaith’ zilikuwepo dini mbalimbali ambazo hapo awali isingekuwa rahisi kukutana na kuabudu pamoja. Waislamu, Wahindu, Wayahudi na dini nyingine zilipata nafasi zilishiriki; isipokuwa Assemblies of God,hii haikuthubutu hata kusogelea.
Viongozi wa Dini kubwa katika Amerika wanahusika sana na umoja huo "Interfaith movement," kwa mfano; Brian McLaren, mmoja wa viongozi wa juu wanaoendesha umoja huo, inasemekana kuwa mwaka 2009 alisherehekea Ramadhan na hata kuvaa mavazi yanayovaliwa na wahusika.
Katika sherehe hiyo; Rick Warren, mshirika wa Baraza la Uhusiano wa Nje, alikuwa Mgeni rasmi na mnenaji kwenye Kongamano la kitaifa la Waislamu huko Amerika ya Kaskazini, (Islamic Society of North America).
Baadhi ya viongozi wa makanisa wakiwemo Rick Warren, Robert Schuller, Brian McLaren, Richard Cizik na Bill Hybels walitia sahihi barua kwa Jumuiya ya Kiislamu iliyokuwa na kichwa kisemacho;  ‘Kumpenda Mungu na jirani yako’
Barua hiyo iliweka bayana kuwa viongozi wa Kikristo wanamtambua Allah kuwa sawa na Mungu wa Wakristo.
Barua hiyo ilisema:“Kabla hatujashikana mikono; katika kukubaliana na barua yetu, tuwatake radhi kwa kuomba msamaha kwa Muumba wa wote. Kwa Waislamu muumbaji ni Allah.
Kwa barua hii, baadhi ya viongozi wa Kikristo wanamuomba na wanatubu kwa jina la Allah, na wanamtambua kuwa ndiye Mungu.”
Kama tulishindwa kurejesha amani na kuwa pamoja, sasa tumesahihisha mawazo yetu na kwamba tunaweza sasa kutakasa nafsi zetu.”
Barua hiyo ndiyo iliyozua hofu duniani kuwa  huenda wakati sasa umewadia wa baadhi ya viongozi kudhihirisha hali ya vuguvugu  na kukosa msimamo wa kiimani.
“Kwa kweli  huu ni usaliti wa hali ya juu, kuandika barua na kueleza kuwa Allah ndiyo Mungu anayeabudiwa na Wakristo  ni mwanzo wa kuelekea katika  dini moja na utawala wa Mpinga Kristo,” alisema Mchungaji Jonathan Emmanuel, wa Nigeria.
Alisema kuwa anautazama mwelekeo huo kama jambo la hatari kwa kuwa Biblia katika  kitabu cha
Yohana 14:6 , Yesu anasema: “...Mimi ndimi njia, na kweli na uzima; mtu haji kwa baba ila kwa njia ya mimi.”
Kiongozi huyo alisema kuwa ukweli wa ki-Biblia uko wazi na wala hauna kificho kuwa Yesu ndiye njia pekee ya kufika mbinguni. Ikiwa unaamini hivyo  ni vipi uandike tena barua ya hatari kama hii ya  kumhusisha Allah na ufalme wa Mungu?
Kisha aliongeza: “Katika amri kumi; awali kabisa tunakutana na maandiko yasemayo; “Usiwe na miungu mingine ila mimi. Usifanya sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu chochote kilicho juu mbinguni , wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia. Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, BWANA, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukizao, nami nawarehemu maelfu  wanipendao, na kuzishika amri zangu.”
 (Kutoka 20:3-6) 

Source Jibu La Maisha

No comments:

Post a Comment