Safari ya kinabii Misri na Israeli chini ya kampuni ya Gombo Tour

Siku chache zilizopita  Safari ya kinabii Nchini Misri na Israeli iliyokuwa ikiongozwa na Askofu Gamanywa chini kampuni ya Gombo Tours ilirejea nchini ikitokea Israeli katika safari nyingine maalumu iliyoongozwa na watumishi wa Mungu, waliojifunga mkanda kumlilia Mungu aliponye taifa lao.


 Maeneo yaliyoonekana kuwa kivutio na kufanya watu kupiga picha katika maeneo hayo 
  
 Askofu Mkuu wa Huduma ya Kimataifa ya BCIC, Sylvester Gamanywa aliongoza kundi la Wakristo wa Tanzania kwenda nchini Israeli pamoja na mambo mengine kuiombea nchi.Akielezea safari hii Mkurugenzi Mtendaji wa Gombo, Bw. Willy Kulola alisema: “Safari yetu ya kinabii ilianzia Misri, tulifika salama na Mungu alikuwa pamoja nasi.Tukatembelea kila eneo kama lililopangwa, isipokuwa Gosheni kutokanana mabadiliko ya ratiba za ndege. Tulivuka bahari ya Shamu eneo walilovuka wana wa Israel wakiongozwa na Musa pakiwa pakavu! Maeneo yote ya Jangwa la Sinai walimoishi wana wa Israel miaka 40 wakirejea nyumbani, tulilala St. Catherine jirani kabisa na Mlima Sinai, ambapo siku iliyofuata tulifika katika kichaka cha Musa ambacho kiliwaka moto, bila kuteketea! Kipo mpaka leo na kinatoa majani ya kijani kibichi hadi sasa! Tulifika eneo la Haruni mahala ambapo wana wa Israel walitengeneza ndama na kumwabudu.
Baadhi ya team ya watu waliokwenda katika picha mmoja wao akiwa na Askofu Gammanywa  
Hakika Mungu aliukubali msafara huu maana ulikuwa kwa utukufu wake.Tulielekea nchi takatifu kupitia mpaka wa TABBA. Tuliporuka tu kila mmoja alionekana kujawa na furaha kubwa sana nyimbo zilitawala ndani ya basi letu! Watu waliimba kwa shangwe na furaha kukanyaga ardhi takatifu nyumbani kwetu.Msafara uliweka kambi katika mji mzuri sana wa bahari kuu ya nchi 4,yaani Israel Jordani, Misri na Saudia. Huduma ilikuwa nzuri sana, vyamwilini walivipata na kuvikubali na siku hiyo tulikuwa na ibada nzuri sana usiku.
Safari yetu ilianzia katika maeneo ya Tarbenacle, lililopo eneo la kumbukumbu ya mfano wa hema ya kukutania, hakika kila mmoja alishangazwa, na hata Askofu Mkuu Gamanywa alisikika akisema:“Nimepata picha mpya isiyoweza futika katika ufahamu wangu wa utumishi.”
Tulipita Masada, dead Sea na tukaenda Jericho, jirani kabisa na mlima wa majaribu ambao Yesu alikaa huko akiomba na kufunga kwa siku 40, na hata shetani kumjaribu. Tulilala Jerusalemu katika Hoteli nzuri,tulipata chakula kizuri sana, vyumba vizuri kiwango cha juu sana kila mmoja alikiri HAKIKA HII NI NCHI YA ASALI NA MAZIWA.

Askofu Gamanywa na Mtume Nyaga walipokuwa Israel 
Apostle Nyaga alitamka wazi kuwa ufahamu wake umebadilika kwa vile alivyoelewa mwanzo na alivyoona sasa.Tumefika katika jumba la makumbusho ya mauaji ya Wayahudi milioni 6,wakiwamo watoto Milioni 1.5 haya kama jasiri ukifika mahala hapo lazima machozi yatatiririka tu! Tumetembea Galicantu eneo ambalo Yesu Kristo alifikishwa kwa Kayafa na Petro kumkana mara tatu. Tumefika Golgotha alikosulubiwa Yesu Kristo akafa na kufufuka, wapendwa waliingia ndani ya kaburi la Yesu na kuliona na baadaye kufanya ibada nzuri sana. Pia meza ya Bwana iliyoongozwa na Mkuu wa msafara Askofu Sylvester Gamanywa na kumalizia kwa kutoa sadaka kubwa nzuri ya kuibariki Israeli na kusaidia kulitunza eneo hilo. Tulienda pia chumba cha juu mahala ambapo Yesu alikula chakula cha mwisho na wanafunzi wake na mahala walipojazwa Roho Mtakatifu kwa mara ya mwisho MAOMBI YA NGUVU.

Mtendaji wa Gombo Tours, Bw. Willy Kulola aliyekuwa mratibu wa safari nzima,akiwa katika kibao kinachaoonesha njia inayokwenda katika mlima ambao Yesu alijaribiwa na shetani.   
Katika eneo hili “upper room” chumba cha juu! Ni mahala ambapo watu walimlilia Mungu kwa nguvu zote, hata ikawafanya wazungu wa makundi kutoka mataifa mbalimbali kushangaa jinsi watanzania walivyokuwa wamejiachilia mbele za Mungu. Maombi yaliwafanya wazungu hao kushindwa kukaa eneo hilo maana tayari ulikuwa ni mpasuko wa anga, Roho Mtakatifu alikuwa ameshuka isivyo kawaida.
Maombi mengine ya kushtua ambayo mpaka viongozi wa Dini ya Kiyahudi naaskari wa ulinzi na Wayahudi walistaajabu ni katika ukuta wa maombi na maombolezo! (Wailing wall) Apostle Nyaga na Mchungaji Amasi walinena kwa lugha za mbinguni, kwa utukufu mkubwa sana, nguvu ya maombi na kunena iliwashukia kiasi Wayahudi walikuwa wanashangaa na kujikusanya wakiwazunguka kushangaa ni kitu gani, maana kwa kipindi kirefu haijatokea.Ilikuwa safari ya kipekee.

Baadhi ya watu aliokwenda wakiwa kwenye maombi.        

Gombo Tours – Experience The wonder of God!
gombotours@hotmail.com
SIMU: 0713 -304984; 0767 -  304984; 0717 – 798991; 0754 – 333125.
TUPO KARIAKOO ROUND A BOUT jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment