Love Tanzania Festival kufanya maajabu Viwanja vya Jangwani.

Kipeperushi cha mkutano cha Andrew Palau ambavyo vimezagaa Tanzania kila kona
Love Tanzania Festival ikiongozwa na Mwinjilisti wa Kimataifa Andrew Palau wameandaa tamasha kubwa la injili lenye lengo la kukutanisha zaidi ya makanisa 800 kwa ajili ya kumsifu na kumwabudu Mungu katika Jiji la Dar es Salaam kwenye viwanja vya jangwani.

Tamasha hilo ambalo litafanyika Jumapili ijao litasindindikizwa na waimbaji maarufu wa nyimbo za Injili Tanzania Christina Shusho, The Voice na Massanja Mkandamizaji ambaye atakuwa akitoa ushuhuda wa maisha yake na jinsi alivyompekea Bwana Yesu kuwa Mwokozi wa maisha yake pamoja na waimbaji wa nje ya nchi akiwemo Don Moen, Dave Lubben na Nicole Mollen.

Akiongea na Blogs, Prosper Mwakitalima ambaye ni miongoni mwa wafanikishaji wa tamasha hilo alisema kuwa tarehe 11-12/08/2012 Jangwani patakuwa hapatoshi kutokana na tamasha hilo la Love Tanzania Festival ilivyojipanga katika kuhakikisha kila mtu atakayehudhulia mahali hapo anakutana na Bwana Yesu kwa njia tofauti tofauti bila ya kuwasahau watoto.

Tamasha hilo lenye lengo la kuwakutanisha watu wa dini,kabila, rika zote kwa lengo la kumtukuza Kristo Yesu litakuwa .ni kusanyiko kubwa la kihistoria ambalo inaweza ikawa haijawahi kutokea katika nchi ya Tanzania kutokana na kwamba watu wamejiandaa kwa maombi na kumtumikia Bwana kwa muda huo wa siku mbili.
Kwa mujibu wa Prosper Mwakitalima kabla ya shughuli ya tarehe 11 na 12 kuna shughuli mbalimbali ambazo Love Tanzania Festival itakuwa ikizifanya kwa jamii ya Tanzania.
Mmoja wa waimbaji kutoka USA, Nicole Molen ambaye naye atashiriki kwenye tamasha hilo la Jangwani

Ifuatayo ni Ratiba ya shughuli nzima za LOVE TANZANIA FESTIVAL.

Tarehe 5 August  7:00Asbh – 10.00 Asbh Mbeba maono wa Love Tanzania Festival  Mtumishi Andrew Palau atahubiri ibada zote mbili katika Kanisa la Upanga City Christian Centre (UCC)
Kutafanyika Mkutano wa waandishi wa habari(Press Confference) Tarehe 7 August 10Asbh katika Ukumbi wa TBD ambapo Andrew Palau akiambatana na wachungaji, Maaskofu,waimbaji na kikundi cha waonyesha michezo ya Baiskeli watakuwa wakiongea na waandishi wa habari.
Usiku huo wa Tarehe 7 kuanzia saa 11.30 jioni katika ukumbi wa KARIMJEE  kutafanyika WOMENS DINNER ambapo kamati imewakaribisha zaidi ya wamama 600 nao watapata nafasi kusikiliza na ya kubadilishana mawazo na Andrew Palau.
Muimbaji wa Kimataifa wa Nyimbo za Injili Don Moen ambaye naye atashiriki katika Viwanja vya Jangwani

Love Tanzania Festival Katika Ukumbi wa Karimjee Hall Tarehe 8 August  12:00 jioni kutafanyika hafla ya chakula cha jioni ambapo viongozi mbalimbali wa serikali na wafanyabiashara wakubwa watapata nafasi ya kukutana na Palau ambapo mtumishi huyo atatumia nafasi hiyo kumtangaza Kristo kwa tabaka hilo la watanzania ambao kwa namna moja au nyingine limekuwa ni vigumu kufikiwa na Injili ya Yesu Kristo.

Tarehe 10:August 8:00 Mchana – 9:00 Jioni Kutafanyika maozoezi (Rehearsal) ya michezo ya Baiskeli ambapo kikundi cha JUNGLE RUSH FMX  kutoka Afrika ya Kusini kitakuwa kikifanya mazoezi hayo ili kujiweka sawa.Baada ya mazoezi hayo kutafanyika MAOMBI rasmi kwa ajili ya kuuweka wakfu uwanja wa Jangwani kwa ajili ya shughuli nzima ya tarehe 11-12.

Baadhi ya Michezo itakayoambatana na Mkutano mkubwa wa Injili

Love Tanzania Festival siyo tu itahusisha kuponya ROHO za watu kupitia Neno la Mungu, pia watakuwepo Madaktari maalumu wa macho kutoka Marekani na watashirikiana na madaktari wa ki-Tanzania ambapo watakuwa wakipima watu mbalimbali wenye matatizo ya macho BURE, wale wenye matatizo ya kutoona vizuri maandishi watapewa MIWANI za kusomea BURE.Jumla ya miwani zipatazo elfu kumi(10,000) zipo kwa ajili ya kugawiwa kwa watanzania ambao watabainika na matatizo hayo, Ratiba ya Clinic hiyo itakayokuwa na vituo vinne ni kama ifuatavyo.               
                 
Pia Huduma ya upimaji Macho na kutoa Miwani itafanyika kwenye vituo vilivyotajwa hapo chini
                                     
Kituo cha 1:St Nicholaus Anglican Church –ILALA
Kituo cha 2:Tanzania Assemblies of GOD (TAG-Mbagala)
Kituo cha 3:Lutheran Chuch – Vingunguti
Kituo cha 4: Baptist Mission Church – Magomeni




No comments:

Post a Comment