Viongozi wa Kikundi cha Jumuiya ya Uamsho wafikishwa mahakamani.

Gari la Polisi ambalo liliwachukuwa Viongozi wa Jumuiya ya Uamsho ambao walishitakiwa kwa makosa ya kufanya fujo na uchochezi likiwa linasindikizwa na magari ya Polisi kuja Mahakama ya Wilaya ya Mwanakwerekwe.
Kikosi cha kutuliza ghasia wakiwa wanaimarisha usalama katika eneo la Mahakama ya Wilaya Mwanakwerekwe ambapo Viongozi wa Jumuiya ya UAMSHO walipelekwa kwenda kusomewa mashitaka yao.


Kiongozi wa Jumuiya ya Uamsho Shekh Farid Hadi Ahmed akishuka kwenye gari la Polisi kuelekea Mahakama ya Mwanakwerekwe kwenda kusomewa mashtaka yao yanayomkabili ikiwemo kusababisha fujo na uchochezi.

Askari wa kikosi cha kutuliza ghasiawakiangalia usalama mahakani hapo.

Baadhi ya Wananchi walioenda Mahakamani hapo kwenda kushuhudia kesi inayowakabili Viongozi wa Jumuiya ya Uamsho ambao walikosa dhamana na kurudishwa Rumande.

No comments:

Post a Comment