Utajili wa Madini unavyohusishwa na mauwaji.

Kuna madai kuwa kwa kadiri madini yanavyozidi kugundulika katika mikoa kadhaa ya Tanzania ndivyo na mauaji ya kinyama ya watu yanavyozidi, hii ni kutokana na kile kinachoelezwa kuwa wateja wengi wa waganga wa kienyeji na walozi ni wachimbaji wa madini.

Mmoja wa wachimba migodi aliyeguswa na Yesu akaokoka aliwahi kushuhudia  katika kanisa moja mjini Morogoro kuwa, wakati akiwa katika uchimbaji madini huko Mererani mkoani Arusha, walikuwa wakienda kwa waganga huko Tanga kutengenezea hirizi za ulinzi na baraka na kuagizwa kupewa masharti magumu ikiwa ni pamoja na kushiriki tendo la ndoa na ndugu wa karibu, watoto au wanyama.


“Nakumbuka niliambiwa nitembee na Punda ndipo nitakapopata madini ya Tanzanite, ilikuwa kazi kubwa tulilazimika kumkata miguu mnyama huyo kwa kuwa ni mkali sana, ndipo nilipofanikiwa kutembea naye na  kwa kweli nilipata hayo madini lakini ulikuwa ni utajiri wa kitambo tu, ukatoweka na kuniacha katika hali mbaya,”alisema kijana huyo.

Kisha aliongeza: “Niliporudi kwake aliniambia safari hii ni lazima nishiriki tendo hilo na binti yangu wa miaka mitatu. Kwa kweli hilo lilikuwa gumu na katika mahangaiko  na mkanganyiko wa  mawazo nikasikia mkutano wa Injili, nilipoenda niliguswa na  nguvu za Yesu nikaokoka. Nikasahau uchafu wote niliofanya ikiwa ni pamoja na kunywa maji yaliyooshewa maiti ambayo tuliinunua katika hospitali ya Maunt Meru.”

No comments:

Post a Comment