Mume na Mke wasalimisha tunguli.

Mganga wa kienyeji maarufu kwa jina la Hassan Kihumba, wilayani Lushoto, na mke wake, wamelazimika kusalimisha tunguli zao za kichawi walizokuwa wakizitumia kuwapa watu wengine uchawi, katika mkutano wa Injili uliofanyika mjini humo, baada ya kukutana na nguvu za Mungu.

Mganga huyo ambaye hakuwa na dhamira ya kufanya lolote katika mkutano huo, alijikuta akishindwa kuelewa ni nini kimeingia mwilini kwake, baada ya kushindwa kuendelea na safari zake alipokuwa akipita kando ya Kanisa la Evangelistical Assemblies of God Tanzania (EAGT).

Akielezea tukio hilo mara baada ya kukutana na nguvu hizo ambazo hakuwahi kuzijua kamwe, Bw. Hussein alisema alikuwa akipita kando kando mwa mkutano huo na wakati huo watu walikuwa wakiombewa na Mchungaji aliyekuwa akiongoza na hapo ndipo aliposhindwa.

“Nilipokuwa napita wala sikuwa na haja ya kusikiliza kile kilichokuwa kikiendelea kwenye mkutano, ghafla nilishtukia niko chini na baadaye nilikuta nimezungukwa na watu ambao pia sikuwafahamu, wakaniambia nilikuwa na mapepo, lakini yametoka, na wakaniambia Yesu anakupenda na kama niko tayari basi nimkubali ili anitoe kwenye vifungo nilivyokuwa navyo,” alisema na kuongeza:

“Nilijihisi mwepesi sana na niliona niko huru kweli kweli, nikaona haina haja ya kuendelea kumsikiliza shetani wakati siku zote kwangu ilikuwa ni mateso, nilikubali kumpokea Bwana Yesu na sasa niko huru, nilienda nyumbani, nilipomwambia mke wangu alikubali tuchome kabisa zana tulizokuwa tukizitumia.”

Hata hivyo wakati hilo likiendelea, katika viwanja vya mjini Lushoto, wakazi wa mji huo hawakuamini kile walichokuwa wakikiona kutokana na umaarufu wa Bw. Hussein kwa kazi za kichawi na wakaliambia Jibu la Maisha kuwa, alikuwa ni tishio lakini walishangaa nguvu iliyoingia ndani yake na kubadilisha  kabisa muelekeo wa maisha yake kabisa.

Katika mkutano huo watu 153 walimkabidhi Yesu maisha yao na wengine kuponywa magonjwa, na kuwekwa huru, baada ya nguvu za giza zilizokuwa zikiwasumbua kukimbia katika mkutano mkubwa wa injili uliofanyika katika uwanja wa sabasaba wilayani Lushoto.

Awali akifungua mkutano huo, Mchungaji mwenyeji wa kanisa hilo, Peter Shetuli alisema watu watarajie kufunguliwa na kuponywa katika siku zote za mkutano huo, Pia alisoma Neno kuu la kutoka katika kitabu cha Mathayo1:18-21 kikielezea   hail
Bwana Yesu alivyokuja kuokoa na kuponya.

Muhubiri wa mkutano huo alikuwa ni Mwinjilisti kutoka Pangani mkoani Tanga, Mchungaji Naftari Msoloka ambaye pia ni mtunza hazina wa Jimbo la Tanga, EAGT.

Mkutano huo ulihudhuriwa na waimbaji maarufu kutoka ndani na nje ya wilaya ya Lushoto ikiwa ni pamoja na George Rungu maarufu kama Rungu la Yesu toka Dar es Salaam, anayetamba na wimbo wa “Ulokole sio fashion na Bwana Yesu asifiwe

No comments:

Post a Comment