Wabunge wengine waguswa na swala la kukabili nguvu za giza.

Baadhi ya wabunge walioongea na chanzo kimoja cha blog hii wameeleza kuguswa na hatua  aliyochukua mwenzao na kuisifu kuwa italeta tumaini la kweli kama  ikifanyiwa kazi na taifa likaingia kwenye toba ya kweli na kumrudia Mungu kama ilivyofanyika nyakati za Biblia.

Akiongea katika mahojiano maalumu, Mbunge wa Iringa mjini, Mchungaji Peter Msigwa, alisema kuwa jambo hilo ni jema na anaimani litakuwa suluhisho la kweli  kwa kuwa, dawa ya kukabili nguvu za giza ni nguvu za Mungu pekee na si vinginevyo.
Mbunge wa Iringa mjini, Mchungaji Peter Msigwa


“Ukitaka kukabiliana na mapepo ni lazima uliitie jina la Yesu na bila hilo hakuna jawabu litakalopatikana. Hata hivyo nawasihi na watumishi wa Mungu nao kusimame imara na kutambua mamlaka na nguvu zao walizopewa na Mungu,  wawaambie watawala ukweli kuwa tiba ya kweli ya mambo hayo ni toba ya taifa zima. Watu watubu na kumlilia Mungu ili alete amani na tumaini la kweli,” alisema mchungaji huyo.

“Umefika wakati wa watumishi wa Mungu kusimama katika nafasi zao na kutambua mamlaka waliyonayo katika kumuwakilisha Mungu. Wao ndio wenye kubeba tumaini la taifa,”alisema Mbunge huyo.

Mbunge wa Muheza Mhe. Herbert James Mntangi, akizungumza katika mahojiano maalumu kuwa mauaji hayo sasa ni janga la kitaifa na lazima kila kiongozi achukue hatua kuanzia kwake yeye mwenyewe. Asikemee wengine kwanza bali aeleze hadharani kuwa yeye hahusiki na ushirikina na akemee kwa nguvu zote.

Alisema kuwa baada ya hatua hiyo, viongozi wa dini nao wajitokeze katika mapambano kwa kuwa wao ndio wenye mamlaka ya kukabili uovu huo na wanaouawa ni waumini wao au ndugu zao wakabiliane katika ulimwengu wa kiroho na wachawi na kuwashinda.

Mbunge huyo alibainisha mbinu ya tatu ya kukabiliana na ulozi kuwa, ni kulikabili tatizo katika koo kwa kuwa, kuna watu ni washirikina kwa kurithi na wanaamini sana mila za koo zao,  bila kuwasaidia huko kamwe hawawezi kuacha.

No comments:

Post a Comment