Pengo awataka wanawake kuchangia Katiba mpya.

Askofu  Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Policarp Kardinali Pengo, amewahimiza wanawake wakatoliki washiriki katika mchakato wa mabadiliko ya Katiba yenye kukidhi matakwa ya Watanzania.

Akizungumza hayo juzi jijini Dar es salaam katika ufunguzi wa maonesho ya miaka 40 ya wanawake wa Katoliki Tanzania (Wawata) yaliyohusisha majimbo 34 ya kikatoliki nchini, alisema kutokana na changamoto wazipatazo wanawake hao katika shughuli zao za ujasiliamali, ni vyema wapewe elimu kuhusiana na ujasiliamali ili kupunguza tatizo la umaskini nchini.

Askofu  Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Policarp Kardinali Pengo,


“Dunia ya leo inahitaji sana upendo, imani na ushirikiano hivyo pandeni mbegu za upendo katika familia ili watoto waonje matunda ya mama na baba ili wakati wa kuandaa maonyesho mengine wazingatie malezi kwa watoto na vijana wao,” alisema Kardinali Pengo.

Pia, Pengo alisema mwanamke mkatoliki wa Tanzania anaelewa nafasi yake na wajibu wake wa kikristo kuanzia ngazi ya familia, jumuiya, kanisa, jamii na taifa kwa ujumla na kuwa na maendeleo ya kiuchumi ili kukidhi mahitaji ya familia.

Katibu Mkuu msaidizi wa Wawata Taifa, Sara Kessy, alisema changamoto zinazowakabili ni pamoja na wengi wao kutokuwa na elimu ya biashara, ubunifu na uzoefu, hali inayopelekea kuona ugumu wa kuendesha biashara zao.

Maonesho hayo yaliyohudhuriwa na wageni kutoka nchi mbalimbali pamoja na Balozi wa Baba Mtakatifu nchini, Askofu Mkuu Francisco Padella.

No comments:

Post a Comment